WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday, 7 December 2017

KUELEKEA MWISHO WA MWAKA TUNATEGEMEA MASHAMBULIZI MTANDAO ZAIDI

Nikizungumza na kundi maalum katika vikao vinavyoendelea nimewasilisha ujumbe wa Tahadhari ambapo Uma umetahadharishwa juu ya mashambulizi takriban Milioni hamsini (50 Milioni) duniani kote katika kipindi cha sikukuu yatakayo gharimu kati ya Dola 50 – Dola 5’000 kwa kila shambulizi.

Matarajio hayo ni kutokana na matumizi makubwa ya mtandao katika kufanya miamala mbali mbali ya manunuzi ya bidhaa katika kipindi hiki cha sikukuu ambapo watu wengi duniani kote wamekua wakinunua vitu mbali mbali kwa wingi kwa njia ya mitandao.

------------------------------
RELATED POST:
------------------------------

Kwa mujibu wa ripoti ya kitelijensia ya matishio mtandao, iliyo wasilishwa na NTT Security – Imeeleza uwepo wa takriban utengenezwaji wa tovutiMilioni moja na nusu zenye mlengo wa kurubuni  kila mwezi ambazo baadhi yao zinadumu kati ya masaa ma nne had inane na kutoweka. Hili niongezeko la asilimia 74 (74%) kulinganisha na takwimu za miezi sita iliyopita.




Maangalizo kadhaa ya muhimu ambayo watumia mitandao wanatakiwa kuzingatia ili walau kupunguza wimbi hili la uhalifu mtandao ni kama ifuatavyo:-

Jiepushe kutumia Wi-Fi za bure unapofanya miamala kwa njia ya mtandao.

Kua makini na program tumishi unazopakua mtandaoni – hakikisha zinatoka katika vyanzo vyenye sifa njema na kuaminika.

Usisambaze mtandaoni taarifa zako binafsi ikiwa ni pamoja na Nywila (neon siri)
Hakikisha unatumia neon siri (Nywila) madhubuti ili kujiepusha na udukuzi unaoweza kukukuta.

Upokeapo jumbe mtandaoni zenye mlengo wa ushawishi wa kukupatia zawadi na kukutaka ufungue viambatanishi, Usifungue viambatanishi hivyo kwani wahalifu mtandao wanatumia fursa hii kusambaza virusi vinavyoweza kukuletea athari mbali mbali ikiwemo kupelekea wizi mtandao.

------------------------------------
NEWS BRIEF:
"In the first half of 2017, 1.9 billion data records were either lost or stolen through 918 cyber-attacks. Most of the attacks used ransomware, a malware that infects computers and restricts access to files in exchange for a ransom"
------------------------------------

Kakikisha vifaa vyako unavyotumia kwa ajili ya mtandao (Simu, Tableti , Komputa yako na vinginevyo) vimewekwa Ant-Virus iliyo ndani ya wakati na pia una sakinisha (Install patches) mara tu zinapo tolewa.

 Jijengee tabia ya kupitia taarifa fupi za miamala (Bank statement) na unapo ona kuna muamala usio utambua utoe taarifa mara moja kwa hatua Zaidi.

------------------------------------
UPDATES:
" We have seen many incidents using anti-forensics tools and methods in an effort to erase signs of their presence and increase the time they are able to explore the network before they are detected, commonly known as “dwell time”.
------------------------------------

Aidha, Kwa Upande Mwingine - Baroness Shields (Mshauri wa waziri mkuu wa uingereza) ametoa wito kwa wabunge wa nchini humo kuacha mara moja tabia ya kuweka wazi maneno yao ya siri (Nywila) au kuwapatia wasaidizi wao.



Akizungumza nao, Aliwaeleza wakiona kuna umuhimu basi wasaidizi wao watapatiwa maneno siri yao (Nywila) pale wanapo wahudumia katika kazi zao.

23 comments:

  1. https://patheticnumber1.blogspot.com/2011/03/novel-landorundun.html?sc=1733829758603#c4090221365718515036 ZUe7aplQ4R

    ReplyDelete