WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday 27 March 2015

INDIA YADHAMIRIA KUKABILIANA NA WIZI KUPITIA MASHINE ZA ATM

Katika Mkutano uliofanyika Nchini India, Mbali na maelezo ya jitihada na dhamira kubwa katika kuwekeza katika maswala ya teknolojia kupitia kampeni yao ya DIGITAL INDIA, Pia nchi imepata kuelezea dhamira yao ya kuwekeza zaidi kwa kutoa misaada ya kimasomo ( Scholarships ) kwa wale watakao kuwa wakisomea masomo yatakayo wezesha kukuza na kufanikisha jitihada zao za Digital India.

Aidha, Kwa Upande mwingine – Wameweza kukubali tatizo linalo ambatana na ukuaji wa technolojia ni uhalifu mtandao huku ikielezwa watumiaji wa simu wamefikia asilimia 97% ya raia wa nchini humo, kitu ambacho kinapelekea matumizi mtandao kuingiwa na dosari ya kipekee.

Itakumbukwa India kupitia taarifa inayosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" waziri mkuu wan chi hiyo alihimiza wananchi wake kujikita zaidi katika kutengeneza namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao ambapo pia iweze kutumika kutoa misaada kwa nchi nyingine.

Katika Kikao cha siku mbili, Kubwa la kiusalama mtandao ni dhamira kubwa ya moja kati ya washiriki wa mkutano huo kuonyesha dhamira yao kubwa ya kukabiliana na tishio la uhalifu kupitia mitandao ( Hasa Wizi wa fedha kupitia ATM) linalo tikisa mataifa mbali mbali hivi sasa.

Katika mazungumzo yangu maalum yaliyo ambatana na mahojianao na vyombo vya habari katika kuangazia dhamira yao hii ya kukabiliana na uhalifu mtandao kupitia wizi wa ATM, Nilipata kuunganisha mawazo na kujua namna gani Taifa la Tanzania tunaweza kuwekeza zaidi kukabiliana na hali hii ambayo pia ni tishio katika Mabenki yetu.

Friday 20 March 2015

PROSECUTION CALLS FOR COOPERATION IN FIGHTING CYBERCRIME GLOBALLY

The prosecution has called for international cooperation in the fight against cybercrime globally, considering the increase of such crimes and advancement of Information and Communication Technologies (ICTs) in the world.

In the National Prosecutions Service Journal released by the Attorney General’s Chambers recently, the prosecution pointed out that, however, global initiatives made at regional and sub-regional level and guidelines to fight such foe were developed at different stages.

According to the document, Africa, which was regarded as backwards has been able to get a leap into the world of ICT and Tanzania among the sub-Saharan countries was not divorced from that though such leap could not come without its price.

“The rapid rate of diffusion of cybercrimes in Tanzania has been a wakeup call to put safeguards to combat these crimes (though) there is no specific legislation which deals with cybercrimes in Tanzania,” the prosecution states in the Journal.

It points out, however, that in 2010, the Parliament enacted the Electronic and Postal Communications Act Number 3 of 2010, which has some provisions that relate to cybercrimes.

“At the moment, the government is making efforts to enact laws to deal with cybercrimes. It is high time for the general public to become conscious of the use of computers and other related devices since any user maybe vulnerable to cybercrime,” the prosecution warns in the Journal.

The Journal points out that one of the most well-known guidelines in fighting cybercrimes is that of the Council of Europe Convention against Cybercrimes, 2001.

Tuesday 17 March 2015

HOLLYWOOD WAZINDUA TAMTHILIA MPYA YA USALAMA MITANDAO

Nilipata kuzungumzia mchango mkubwa unaopatikana kupitia vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na Tasnia ya filamu katika kutoa elimu ihusuyo maswala ya usalama mitandao. Hollywood wamekua wakiongoza katika kutengeneza vipengele mbali mbali vyenye kutoa ufafanuzi wa makosa mtandao yanavyo tendwa na namna ya kutambua na kujikinga.

Hatua yao hiyo imekua ikipongezwa sana na wataalam wa maswala ya mitandao duniani kote huku tukisistiza mataifa mengine yaweze kuiga juhudi hizo. Kuungana na wataalam wengine nilipata kuandika Makala ya kingereza inayosomeka kwa “KUBOFYA HAPA”, Makala iliyofanya vizuri na baadae kupatikana katika gazeti moja la ughaibuni linalotoka maramoja kila mwezi.

Mwezi huu wa tatu Hollywood wameamua kuzindua tamthilia maalaum iliyopewa jina la CSI: CYBER ambapo imejikita katika maswala ya usalama mitandao. Katika tamthilia hiyo inatoa mafunzo mbali mbali kwa kuonyesha makosa yanavyo fanywa na namna ya upelelezi wa makosa hayo unavyo fanyika pia.

Mwandaaji wa Filamu Hiyo Amekiri kua kilicho mvutia kuifanya si tu hamasa kutoka kwa wataalam wa usalama mitandao bali pia ni pamoja na uhalisia kua kila siku ni lazima habari za uhalifu mitandao zitengeneze vichwa vya habari huku akiamini wengi wata tamani sana kuona filamu ihusuyo mambo wanayosikia sasa katika vyombo mbali mbali vya habari yahusuyo uhalifu mtandao.

Tamthilia hiyo imepongezwa na wataalam wa maswala ya usalama mtandao ambapo katika forum za mijadala mbali mbali tunayoendelea nayo imekua ikipewa uzito wa pekee kwa kupongezwa na kuambiwa imekuja muda muafaka kwani tayari athari za uhalifu mtandao zimesha mgusa kila mmoja kwa namna moja au nyingine.

Tamthilia hiyo imemshirikisha mwanamziki maarufu “SHAD MOSS” – anaejulikana sana kwa jina la BOW WOW na wasanii wengine wenye uwezo mzuri wa kuigiza. Tamthilia hiyo inategemewa kufanya vizuri sana na kufanikisha malengo ya kufikisha ujumbe kwa idadi kubwa ya watu.

Wednesday 11 March 2015

THE RISKS OF GAMBLING WITH CYBER CRIME

I would like to emphasize on  "DAILYNEWS" article, I wrote –  CYBER crimes are a new type of occurrences in today’s digital age, different from the conventional crimes that we all are used to. Unfortunately, the crimes are rapidly increasing and have no borders.

Above all, the criminal techniques are swiftly changing. In Tanzania for example, more than 999 cybercrimes were reported, according to available data. However, only 212 cases were filed and 132 suspects were charged before a court of law.

This is clear indication that cyber-attack is a real threat and that the cyber space is not a safe environment. Moreover, there could be more than a thousand cybercriminal suspects out there who have not been reported, and the number could be rising.

Evidence may be derived from the social media where irresponsible individuals have been spreading propaganda such as publishing doctrines promoting violence, extremism, recruitment and training of potential terrorists, and transferring confidential information.

It is clear that if authorities fail to intervene immediately to halt any such move, this can be an opportunity for cyber criminals to advance. Combating cybercrime starts with the authority responsible for the country’s security, to establish a cyber-security policy.

This can be followed by regulatory and legal infrastructures, cybercrime units, organisational and institutions and public awareness. The more these strategies take time to be put in place, the faster the cybercrimes. To date, Tanzania has no policy or cyber security laws and this puts her cyber space at a greater risk.

It is hoped though that when a Bill is tabled in Parliament, the process would not take a long time before a law is passed. In addition, there should be sustainable public awareness programmes on cybercrimes. The previous cyber-attacks should serve as a wakeup call.

Cybercrime is also a global challenge. Its control needs joint judicial cooperation and Tanzania is, without doubt, part of it. However, the country needs to put an institutional framework first so as to be fully involved in the war against global cybercrime.

The cyber security policy for any country especially, those who have embarked on ICT development is very important. The policy protects information and builds the capability to prevent cyber-attacks through developing cyber security skill sets, cyber crisis management, critical infrastructure protection, public and private partnership security issues and other related policy issues.

Monday 9 March 2015

UMAKINI ZAIDI UNAHITAJIKA KWA WATUMIAJI MITANDAO.

Ukuaji wa Sekta ya TEHAMA umekuwa wa mafanikio na msaada mkubwa katika kuharakisha, kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia  kikamilifu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa letu. Kwa mfano, wananchi walio wengi sasa wanapata huduma mbalimbali za mtandao kwa kutuma na kupokea pesa; kulipia ankara za maji, umeme na tozo mbalimbali kama vile ada na leseni; na mawasiliano ya simu na intaneti pamoja na elimu mtandao na tiba mtandao.

Palipo na mafanikio hapakosi changamoto. Pamoja na kwamba tumeshuhudia manufaa na umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, biashara, miundombinu ya mawasiliano, pia kumekuwepo na changamoto ya matumizi mabaya ya mtandao katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya makundi ya watu na hata kutoka Taifa moja kwenda Taifa lingine kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni.

Baadhi ya mifano ni pamoja na  suala la wizi wa fedha kwa njia ya mtandao, matukio ya uhalifu kwa kutumia mtandao, uvujaji wa taarifa za siri, upotevu wa haki miliki na matumizi ya saini na ushahidi, mmomonyoko wa maadili, athari za makundi maalumu kama vile watoto na usalama wa miundombinu mbalimbali ya TEHAMA ambapo Serikali imeingia gharama kubwa kuiweka.

Wakati hayo yakijiri, Kwa sasa kumekua na wimbi kubwa la kurubuni watu kupitia mitandao ambapo majina ya wanasiasa, wanamuziki na wenye majina makubwa yameendelea kutumiaka vibaya katika mitandao ili kufanikisha urubuni wa kuwaibia watu pesa kwa kutumia jina la “VIKOBA” – Chakushangaza zaidi kurasa hizo zinazo onekana zaidi kupitia mitandao yakijamii zinaonekana zimedhaminiwa ili kuweza kusomwa na wengi kitu ambacho  kinapelekea kuonyesha jinsi gani wimbi hili na wahalifu hawa mtandao wamejipanga.

Wednesday 4 March 2015

WE NEED TO PROTECT OUR SOCIETY AGAINST CYBERCRIMES

The number of cyber-attacks has been increased and the need to extend effort to the fight against cybercrimes is strongly recommended. I have mentioned in one of the article that can be "READ HERE" advising companies to strengthen cybersecurity. We have seen India PM recently addressing loudly cybersecurity issues in one of the event taken place in India as it can be "READ HERE"

On Monday 2nd March 2015, security experts emphasized again the need for collaboration in order to protect society against cyber-attacks during the 6th annual Cyber Defense Summit in Riyadh.

“Cyber security is no longer just an information technology priority. It must be addressed at the broad level,” said Yesser Deputy Director General Ahmad Al-Khiary.
Al-Khiary, also the current CEO of (ITS) 2, noted the importance of protecting critical infrastructure and sensitive information in Saudi Arabia.

“We must address the issue collectively to arrive at feasible protective measures,” he said.

Another expert, Tareque Choudhury of BT Global Services, spoke on the occasion, defining critical assets and the role of chief security officers by giving examples of how private and public Saudi organizations can protect and preserve themselves.
He also shared some of the lessons learned from the BT cyber security team, which was deployed to defend the London Olympics in 2012 from any malicious cyber-attacks.

“A lack of cyber protection has had catastrophic results. For example, hackers stole 40 million debit and credit card numbers from retailer ‘Target’s’ data banks, as well as the personal data of as many as 70 million customers,” he said.

Monday 2 March 2015

WAZIRI MKUU INDIA ATAKA SULUHU ZA USALAMA MTANDAO KWA WANA TEHAMA

Baada ya miaka 25 ya mafanikio nchini india katika sekta ya TEHAMA, Waziri mkuu wa nchi hiyo amezitaka sekta za TEHAMA kuboresha usalama wa mitandao ili kukabiliana na wimbi la uhalifu mtandao kwa kuwa na ubunifu madhubuti wa njia sahihi za kukabiliana na uhalifu mtandao nchini India.

Waziri mkuu Huyo mhe. Narendra Modi, Ameyazungumza hayo alipokua akizungumza na wana TEHAMA Nasscom, Waziri mkuu huyo alizungumza na kusema dunia nzima imekua ikiangazia macho maswala ya usalama mitandao na kusisitiza toka alipopata wadhfa huo amekutana na wanasiasa takriban 50 na kati yao wanasiasa kati ya 25 – 30 wamekua wakionyesha hisia zao juu la wimbi kubwa la uhalifu mtandao unao kua kwa kasi.

Waziri mkuu huyo akauliza swali, Vijana wa Ki hindi wako tayari kufanyia kazi kupata suluhu la matatizo ya uhalifu mitandao? Huku akiongezea kua maswala ya usalama mitandao yana weza kuongezea sana kipato taifa hilo na kuishauri Nasscom kuangazia swala hilo ili baadae kutoa huduma stahiki za kiusalama mitandao katika mataifa mbali mbali duniani.

Katika kuongezea Waziri mkuu huyo alielezea TEHAMA inauwezo mkubwa sana wa kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya utalii nchini humo. Alitoa changamoto kwa wana TEHAMA wa india kwa kutofaninisha kupatikana kwa Google iliyotengenezwa nchi humo.

Akizungumza na Deccan Herald – Mkurugenzi mkuu wa Happiest Minds Technologies Ashok Soota, Waziri mkuu huyo alionyesha furaha yake kwa sekta ya TEHAMA kuweza kuzalisha Dola za kimarekani Bilioni 146 na kusababisha dunia kuitazama tofauti nchi hiyo.