Baada
ya miaka 25 ya mafanikio nchini india katika sekta ya TEHAMA, Waziri mkuu wa nchi
hiyo amezitaka sekta za TEHAMA kuboresha usalama wa mitandao ili kukabiliana na
wimbi la uhalifu mtandao kwa kuwa na ubunifu madhubuti wa njia sahihi za
kukabiliana na uhalifu mtandao nchini India.
Waziri
mkuu Huyo mhe. Narendra Modi, Ameyazungumza hayo alipokua akizungumza na wana
TEHAMA Nasscom, Waziri mkuu huyo alizungumza na kusema dunia nzima imekua
ikiangazia macho maswala ya usalama mitandao na kusisitiza toka alipopata
wadhfa huo amekutana na wanasiasa takriban 50 na kati yao wanasiasa kati ya 25 –
30 wamekua wakionyesha hisia zao juu la wimbi kubwa la uhalifu mtandao unao kua
kwa kasi.
Waziri
mkuu huyo akauliza swali, Vijana wa Ki hindi wako tayari kufanyia kazi kupata
suluhu la matatizo ya uhalifu mitandao? Huku akiongezea kua maswala ya usalama
mitandao yana weza kuongezea sana kipato taifa hilo na kuishauri Nasscom
kuangazia swala hilo ili baadae kutoa huduma stahiki za kiusalama mitandao
katika mataifa mbali mbali duniani.
Katika
kuongezea Waziri mkuu huyo alielezea TEHAMA inauwezo mkubwa sana wa kuleta
mabadiliko makubwa katika sekta ya utalii nchini humo. Alitoa changamoto kwa
wana TEHAMA wa india kwa kutofaninisha kupatikana kwa Google iliyotengenezwa
nchi humo.
Akizungumza
na Deccan Herald – Mkurugenzi mkuu wa Happiest Minds Technologies Ashok Soota,
Waziri mkuu huyo alionyesha furaha yake kwa sekta ya TEHAMA kuweza kuzalisha
Dola za kimarekani Bilioni 146 na kusababisha dunia kuitazama tofauti nchi
hiyo.
Taarifa
zaidi juu ya Hafla hiyo na aliyo zungumza waziri mkuu huyo unaweza kuyasoma kwa
"KUBOFYA HAPA"
No comments:
Post a Comment