WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Saturday, 29 March 2014

CYBERCRIME AWARENESS - VIDEO

Kufuatia mpango kabambe wa kuelimisha jamii dhidi ya makosa mtandao tayari kumekua na video za katuni, Mchezo wa komputa “Computer gane”, majarida ya katuni pamoja na machapisho mengine yote yakiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya jinsi ya kujilinda dhidi ya makosa mtandao kuanzia ngazi ya mtu binafsi hadi kufikia ngazi ya kitaifa.Athari za makosa ya kimtandao ni kubwa sana endapo hatua za msingi za kudhibiti uhalifu mtandao hazitochukuliwa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi hadi taifa kwa ujumla. Mataifa makubwa tayari wamesha yaona haya na sasa kumekua na jitihada mbali mbali zenye malengo ya kukabiliana na uhalifu mtandao.


Monday, 24 March 2014

MKUTANO WA MASWALA YA ULINZI MTANDAO WAKAMILIKA KWA KUPIGILIA MSUMARI KAULI MBIU “MWAKA 2014 NI MWAKA WA VITENDO”

mkutano wa “Cyber event conference” umekamilika salama ambapo mambo mbalimbali yalipata kujadiliwa yahusuyo ulinzi mtandao “Cyber security” na kupigilia msumari kauli mbiu ya mwaka 2014 kua ni mwaka wa vitendo.
Mwanzo wa mkutano bwana Craig Rosewarne (Mwenyekiti wa kundi linalojiuhisisha na maswala ya ulinzi mtandao (ISG) katika nchi za afrika ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni Wolfpack inayo jihusisha na maswala ya ulinzi mtandao na mkurugenzi wa SANS ukanda wan nchi za Afrika na mashariki ya kati) alianisha hali ilivyo sasa na kusema kumekua na wimbi kubwa la makosa mtandao ambapo kila mwaka yanaongezeka kasi huku akitolea mifano mbali mbali ya matukio ya hivi karibuni.
Aidha alipata kuanisha ukuaji wa teknologia ambapo inaendelea kukua kwa kasi na inavyo ongeza uwezekano wa kasi ya uhalifu mtandao kukua endapo jitihada za dhati hazitowekwa tayari ili kukabiliana na changamoto zinazo rudisha nyuma vita dhidi ya ulinzi mtandao. Akitolea mifano changamoto mbali mbalizinazopelekea ugumu katika  ulinzi mtandao alianisha changamoto hizo ikiwa ni pamoja na:-
1.      Uhaba wa programu za kompyuta salama kimtandao huku akitolea mifano baadhi ya program za komputa zinavyo tengenezwa kutoa mwanya kwa wahalifu kupa urahisi kuingilia komputa za watumiaji wa program hizo
2.       Kutokuwepo na makubaliano ya pamoja ya kisheria  katika mapambano dhidi ya makosa mtandao.
3.      Kutokuwa na ushirikiano wa kuunganisha nguvu kati ya serikali mbali mbali na sekta binafsi kutokomeza uhalifu huu ambao unaendelea kukua kwa kasi.