WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Monday, 24 March 2014

MKUTANO WA MASWALA YA ULINZI MTANDAO WAKAMILIKA KWA KUPIGILIA MSUMARI KAULI MBIU “MWAKA 2014 NI MWAKA WA VITENDO”

mkutano wa “Cyber event conference” umekamilika salama ambapo mambo mbalimbali yalipata kujadiliwa yahusuyo ulinzi mtandao “Cyber security” na kupigilia msumari kauli mbiu ya mwaka 2014 kua ni mwaka wa vitendo.
Mwanzo wa mkutano bwana Craig Rosewarne (Mwenyekiti wa kundi linalojiuhisisha na maswala ya ulinzi mtandao (ISG) katika nchi za afrika ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni Wolfpack inayo jihusisha na maswala ya ulinzi mtandao na mkurugenzi wa SANS ukanda wan nchi za Afrika na mashariki ya kati) alianisha hali ilivyo sasa na kusema kumekua na wimbi kubwa la makosa mtandao ambapo kila mwaka yanaongezeka kasi huku akitolea mifano mbali mbali ya matukio ya hivi karibuni.
Aidha alipata kuanisha ukuaji wa teknologia ambapo inaendelea kukua kwa kasi na inavyo ongeza uwezekano wa kasi ya uhalifu mtandao kukua endapo jitihada za dhati hazitowekwa tayari ili kukabiliana na changamoto zinazo rudisha nyuma vita dhidi ya ulinzi mtandao. Akitolea mifano changamoto mbali mbalizinazopelekea ugumu katika  ulinzi mtandao alianisha changamoto hizo ikiwa ni pamoja na:-
1.      Uhaba wa programu za kompyuta salama kimtandao huku akitolea mifano baadhi ya program za komputa zinavyo tengenezwa kutoa mwanya kwa wahalifu kupa urahisi kuingilia komputa za watumiaji wa program hizo
2.       Kutokuwepo na makubaliano ya pamoja ya kisheria  katika mapambano dhidi ya makosa mtandao.
3.      Kutokuwa na ushirikiano wa kuunganisha nguvu kati ya serikali mbali mbali na sekta binafsi kutokomeza uhalifu huu ambao unaendelea kukua kwa kasi.
4.      Kutokua na elimu kwa jamii juu ya makosa mtandao na jinsi ya kukabiliana nayo katika ngazi ya ya mtu mmoja mmoja.
5.      Kutokuwepo na utayari kwa kuunda timu katka nchi mbali mbali zenye uwezo wa kukabiliana na uhalifu mtandao.
Kwa upande mwingine Bwana Martin Euchner kutoka ITU (International telecommunication union) wakala wa umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya mawasiliano alianisha hatua mbali mbali mbali ambazo hadi sasa ITU imekua ikizichukua ili kujaribu kuunganisha nchi zote za umoja wa mataifa ili kwapamoja ziweze kupambana kupunguza uhalifu mtandao.
Pia alipata kuzungumzia jitihada za dhati na mafanikio yaliyo patikana kupitia mpango wa COP (Child Online Protection) ambao umejikita kuhakiki watoto wanabaki salama mtandaoni, kauli iliyo ibua hoja nzito ya mchezo unao patikana kwenye simu hivi sasa ujulikanao kama “Talking angela” ambao umekua unachezwa na watoto wengi wadogo mtandaoni chezo ambao ume ukitiliwa shaka unaweza kuwa unatumika vibaya na wahalifu mtandao ili kukusanya sauti za watoto na picha zao zinazoweza kutumiwa vibaya baadae.
Aidha bwana Eucner, aliweza kuzungumzia mpango kabambe ambapo mapitio na kuangalia kwa karibu changamoto mtandao katika nchi mbali mbali katika mwaka huu wa 2014 zinategemewa kufanyika katika nchi takriban 16 Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zitakazo weza kufaidika na mpongo huo.
Kwa upande wa bwana Kileo, Aliweza kufafanua kwa kina uhaba mkubwa wa wataalam wa maswala mtandao katika ngazi ya kidunia kwa sasa na mahitajio ya wataalam imekua ni kubwa huku akitolea mfano katika nchi zilizo endelea kuwa na mikakati kabambe ya kuunda jeshi Mtandao ili kukabiliana na vita mtandao maarufu kama “Cyber war”.
Aidha bwana kileo aliasa washiriki kuendelea kufahamu yakua swala la mitandao ni swala lisilo na mipaka ya kijografia na linaweza kufanywa na mhalifu kutokea maeneo yoyote bila kujali anadhuru nchi gani hivyo nguvu ya pamoja ni muhimu sana ili kuweza kukabiliana na hali mbaya iliyo sasa.

Katika kusisitizia kauli hiyo ya bwana Kileo, Bwana Rosewarne alieleza ni swala lililo wazi kuwa kwa sasa tatizo lipo hakuna ubishi huku akianisha hatua mbali mbali zilizochukuliwa hadi sasa kukabiliana na uhalifu mtandao ikiwa ni pamoja na:-
1.      kuwepo na website maalum “ Alert website” ambayo itakua inatoa elimu kwa mwananchi dhidi ya makosa mtandao.


2.      Katuni (Animation Video) ambazo tayari zimefikia 12 zinazotegemewa kuendelea kutumiwa katika televisheni ili kutoa elimu kwa jamii dhidi ya maswala mtandao.3.      Upatikanaji wa “phishing Task force” ambapo itajikita kukabiliana na makosha ya udanganyifu mtandaoni maarufu kama “Phishing”

4.      Kuendelea kuangazia na kutengeneza “Action plan” kwa nchi za afrika na mataifa mengine kiujumla kuziwezesha kukabiliana na makosa mtandao, huku akitolea mfano wa kukamilika kwa zoezi hili katika mwaka huu kwa nchi ya Nigeria.