WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Sunday, 3 June 2018

NAMNA BORA YA KULINDA VIFAA VYA TEHAMA VYA WATOTO



KWA UFUPI: Kutokana na ukuaji wa teknolojia pamoja na muunganiko wa vitu vingi katika mtandao (IoT) vifaa vingi vya watoto vimekua mhanga mkubwa wa uhalifu mtandao – Hii imepelekea kuchukuliwa kwa hutua mbali mbali za kulinda watoto mitandaoni. Andiko hili lina angazia namna bora ya kulinda vifaa vya watoto vya TEHAMA.
-----------------------------------------

Kumekua na matukio kadhaa yaliyo husisha kuingiliwa kimtandao (kudukuliwa) kwa vifaa vinavyo tumiwa na watoto huku wahalifu mtandao wakiunda program tumishi zenye nia ovu ya kukusanya picha na sauti za watoto.

Mfano, kampuni ya V-Tech ambayo inatengeneza vifaa vya TEHAMA vya watoto Ilipata kudukuliwa na wahalifu mtandao ambapo taarifa nyingi za watoto zilijikuta mikononi mwa wahalifu mtandao.

Shirika la umoja wa mataifa linalo husiana na TEHAMA (ITU) limekua na kampeni maarufu ya Kuwalinda watoto mtandaoni – Child online protection (COP) ambayo imeongezewa nguvu na Kampeni nyingine ya wanausalama mtandao ijulikanayo kama siku ya usalama mtandao “Safer internet day” ambazo kwa pamoja zinatoa msaada ingawa kuna kila sababu kwaa wazazi nao kuchukua hatua kuwalinda watoto wao kimtandao.


Taarifa zinaonyesha wazazi wengi wamekua wakinunua vifaa kama vile – midoli ya kimtandao (smart toys), Vifaa vya kuwafatilia wototo (baby monitors), na vifaa vingine vya kuchezea (high-tech swings na play pads) vyote vikiwa vimeunganishwa katika mitandao.


Ikumbukwe, vifaa hivi vyote pamoja na kuonekana kuwapatia watoto furaha pamoja na kuwaweka wazazi karibu na watoto wao pia vinaongeza hatari kubwa ya kuweza kusababisha uhalifu mtandao kwa watototo – tumeendelea kuwaasa wazazi kua makini kwenye haya.

Wazazi wengi wamekua wakieleza vifaa hivi vimekua vikiwasaidia kuweza kujua hali za watoto wao (Mfano: Kujua joto lao la mwili la mtoto, mapigo ya moyo ya mtoto nakadhalika) huku wakiweza kuwafatilia watoto wao kwa kuwaona kwa ukaribu ingawa wako mbali nao kupitia vifaa hivi vya kisasa – Ni sahihi kua hili si jambo baya kwa mzazi kwani inampa faraja kujua mtoto wake anaendeleaje mda wote hata kama yuko mbali.

Ifahamike kua, wahalifu mtandao wame endelea kuingilia vifaa hivi kwa nia mbali mbali – Wengine wanafatilia tu familia za watu na njia rahisi ni kupitia vifaa hivi vinavyo weza kudukuliwa kirahisi, na wengine ni katika kukusanya tu taarifa za watoto ambazo wamekua wakizitumia vibaya.

DONDOO:  Namna unavyoweza kulinda vifaa hivi vya watoto dhidi ya uhalifu mtandao.


Tafakari kabala ya kununua: Kabla ya mzazi kununua vifaa hivi ni vyema ukajiuliza maswali muhimu – Je, Unaulazima wa kua navyo, vinaathari gani kwenye taarifa za familia, unauwezo wa kuvilinda, vimeunganishwa kwenye mtandao kwa kiasi gani, vimeundwa na nani na vina ulinzi kiasi gani.

Badili neon siri (Nywila) linalo kuja na vifaa hivyo (Default password): Vifaa hivi vya ki TEHAMA vya watoto vinakuja na Maneno siri ambayo wahalifu mtandao mara nyingi wanakua tayari wanayajua au ni rahisi kuya pata – Inashauriwa kama umenunua ni vizuri ukabadili maneno siri hayo na kuweka mengine madhubuti ambayo utakua ukibadili mara kwa mara kama kifaa kitaruhusu ili kulinda vifaa hivyo.

Nunua vifaa vivi kutoka kwenye makampuni yenye sifa (Known brand – with reputation): Kumekua na makampuni mengi ambayo yamekua yakitoa vifaa pamoja na program tumishi zenye nia ovu ya kukusanya taarifa za watoto

Aidha, Kunayo makampuni ambayo yamekua na udhaifu katika kulinda vifaa wanavyo tengeneza kwa ajili ya watoto – Inashauriwa uhakiki unajiweka mbali na aina hizo za makampuni ili usijikute eidha, ulicho nunua kinapelekea taarifa za mtoto (Picha na sauti) kutumiwa vibaya au kampuni inadukuliwa mara kwa mara na kupelekea taarifa za watoto kua hatarini.

Boresha program (Update software): Kama ilivyo kwa program nyingine, panapo gundulika mapungufu watengenezaji hutoa maboresho ambayo yanamtaka mtumiaji kuyaongezea kwenye vifaa wanavyo tumia ili viendelee kua na ulinzi – Kwenye vifaa vya watoto pia inapaswa wazazi wawe na tabia ya kuboresha programu zake kila mara zinapo boreshwa na watengenezaji/ waundaji wa vifaa hivyo.

Zima kama hutumii: Vifaa hivi vinapokua vimezimwa vinapunguza mwanya kwa wahalifu mtandao kuvidukua au kuviathiri, hivyo inashauriwa kama kifaa cha mtoto cha kitehama ukitumii basi kizime – Hii itasaidia kupunguza wimbi la uwezekano wa kudukuliwa au kuingiliwa kwa faragha za watoto na familia kwa ujumla.



2 comments:

  1. Hallo mr kileo nimependa andiko lako safi sana kiongozi nipo nyuma yako boss

    ReplyDelete
  2. Great readinng your blog

    ReplyDelete