Nilipata
kuzungumzia mchango mkubwa unaopatikana kupitia vyombo vya habari ikiwa ni
pamoja na Tasnia ya filamu katika kutoa elimu ihusuyo maswala ya usalama mitandao.
Hollywood wamekua wakiongoza katika kutengeneza vipengele mbali mbali vyenye
kutoa ufafanuzi wa makosa mtandao yanavyo tendwa na namna ya kutambua na
kujikinga.
Hatua
yao hiyo imekua ikipongezwa sana na wataalam wa maswala ya mitandao
duniani kote huku tukisistiza mataifa mengine yaweze kuiga juhudi hizo.
Kuungana na wataalam wengine nilipata kuandika Makala ya kingereza inayosomeka kwa
“KUBOFYA HAPA”, Makala iliyofanya vizuri na baadae kupatikana katika gazeti
moja la ughaibuni linalotoka maramoja kila mwezi.
Mwezi
huu wa tatu Hollywood wameamua kuzindua tamthilia maalaum iliyopewa jina la CSI:
CYBER ambapo imejikita katika maswala ya usalama mitandao. Katika tamthilia
hiyo inatoa mafunzo mbali mbali kwa kuonyesha makosa yanavyo fanywa na namna ya
upelelezi wa makosa hayo unavyo fanyika pia.
Mwandaaji wa Filamu Hiyo Amekiri kua kilicho mvutia kuifanya si tu hamasa kutoka kwa wataalam wa usalama mitandao bali pia ni pamoja na uhalisia kua kila siku ni lazima habari za uhalifu mitandao zitengeneze vichwa vya habari huku akiamini wengi wata tamani sana kuona filamu ihusuyo mambo wanayosikia sasa katika vyombo mbali mbali vya habari yahusuyo uhalifu mtandao.
Mwandaaji wa Filamu Hiyo Amekiri kua kilicho mvutia kuifanya si tu hamasa kutoka kwa wataalam wa usalama mitandao bali pia ni pamoja na uhalisia kua kila siku ni lazima habari za uhalifu mitandao zitengeneze vichwa vya habari huku akiamini wengi wata tamani sana kuona filamu ihusuyo mambo wanayosikia sasa katika vyombo mbali mbali vya habari yahusuyo uhalifu mtandao.
Tamthilia
hiyo imepongezwa na wataalam wa maswala ya usalama mtandao ambapo katika forum
za mijadala mbali mbali tunayoendelea nayo imekua ikipewa uzito wa pekee kwa
kupongezwa na kuambiwa imekuja muda muafaka kwani tayari athari za uhalifu
mtandao zimesha mgusa kila mmoja kwa namna moja au nyingine.
Tamthilia
hiyo imemshirikisha mwanamziki maarufu “SHAD MOSS” – anaejulikana sana kwa jina
la BOW WOW na wasanii wengine wenye uwezo mzuri wa kuigiza. Tamthilia hiyo inategemewa
kufanya vizuri sana na kufanikisha malengo ya kufikisha ujumbe kwa idadi kubwa
ya watu.
Naomba
nirudie tena kusema, Imefika wakati sasa kwa Tanzania kuihusisha tasnia ya
filamu nchini kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na maswala
ya uhalifu mtandao, jinsi ya kugundua na kukabiliana nayo ili kuongeza wigo wa
uelewa kwa jamii nchini kwani inaaminika kupitia filamu darasa linaeleweka
zaidi kwani wana filamu wananafasi kubwa sana katika kutoa elimu mbali mbali
katika jamii.
Vita
dhidi ya uhalifu mtandao si vita ya kundi fulani la watu au aina fulani ya watu
bali ni swala linalo anzia katika ngazi ya mtu binafsi na kuonganisha nguvu ili
kuhakiki taifa na dunia kwa ujumla inakua salama kimtandao.
Kwa
kuzingatia Hili natoa wito kwa jamii ya kitanzania kutambua hali hii ya uhalifu
mtandao na kuhakiki jitihada za dhati zinachukuliwa mapema bila ya kungoja hali
kuwa mbaya kiasi cha kuwa na ugumu kupata suluhu ya jinsi ya kukabili uhalifu mtandao
nchini.
Sehemu ya kwanza ya tamthilia hiyo inaweza kutazamwa kwenye video hapo chini
Hi Brother Kileo, Hii ni maneno poa sana nimekua nikifatilia unacho write na na vutiwa sana na unavyo weka maneno.
ReplyDeleteMimi ni Silvia wa KE.