Nianze
kuliandikia hili kwa kuonyesha furaha yangu kuwa huwenda sasa kumekua na uelewa
juu ya maswala ya usalama mitandao. Nalisema hili kutokana na uhalisia kwamba
Jana nilipata maswali kutoka kwa watu wengi sana huku nikipata jumbe nyingi
zilizofanana zikielezea juu ya tukio la benk ya NBC kuingiliwa na wadukuzi.
Wengi
walinitaka pia nielezee huku nikiulizwa mbona hakuna nilichozungumza.
Nilifarijika sana kwani muda uliopita wengi hawakua wakihoji juu ya maswala ya
udukuzi pamoja na usalama mitandao na huwenda hii ilitokana na kutokua na
uelewa wa maswala husika.
NINI HASA KILITOKEA?
Kwanza
kabisa Kulikua na Itlafu ya Umeme ambayo ilisababisha baadhi ya Mashine kuzima.
Pili,
Kulitokea Tahadhari ya Moto iliyosababisha wafanyakazi kuchuukua tahadhari ya
kutoka nje.
Na Tatu,
Mifumo ya Mobile banking (Inayotoa huduma za miamala kupitia simu za kiganjani)
kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo iliyo sababisha kutoa kiwango kisicho sawa
kwa waliokua wakiangalia salio.
Matukio
haya matatu yaliunganishwa na kutengeneza taarifa moja iliyo sambazwa kua kuna
mdukuzi aliingilia banki ya NBC na kusababisha mifumo kutofanya kazi na hatimae
kuhamisha kiasi kikubwa cha pesa. Kitu
ambapo kilipelekea wafanya kazi kutoka nje ili uchunguzi zaidi uweze kufanywa.
Na
anaepata taarifa anapo angalia salio anaona kunatatizo katika kiasi chake na
kuamini jumbe ile. Panapotoka ufafanuzi wa taarifa hii wengi bado wanahoji bado
kuna shaka niendelee kutoa ufafanuzi nini hasa kinaweza kikawa kimesababisha?
NINI KINAWEZA KUWA TATIZO?
Wengi
wanaweza kuhusisha matukio mawili ya mifumo kuzimika na mifumo ya Mobile money
kutofanya kazi (Kuzidiwa nguvu) na kutoa taarifa zisizo sahihi na kinacho
julikana kama "DDOS ATTACKS" ambapo pia ni uhalifu mtandao unaoweza kusababisha
tukio la mifumo kuzima na kuzidiwa kufanya kazi.
Lakini
pia ikumbukwe mifumo kuzima na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi huwenda
ni maswala tu ya kiufundi na isi husiane kabisa na uhalifu nilio uzungumzia.
Panapo
zimika kwa mitambo ya umeme wakati mwingine husababisha komputa kuzima ghafla
kama mifumo ya kuhifadhia moto kutokua vizuri.
Watu
wengi wanapotuma maombbi kwenye mfumo wanaweza kuisababishia kushindwa kufanya
kazi yake ipasavyo kutokana na kuzidiwa nguvu – Hii inafanana na aina ya
uhalifu nilio uzungumzia ingawa huwenda ikawa ni wengi wametaka kwa nia njema
kujua kiasi cha pesa zao baada ya kusikia kuna tatizo.
Niendelee
kuwasihi wa Tanzania, wanapo ona tatizo ni vizuri kulifatilia na kulichunguza
kwa makini kabla ya kulitolea taarifa na pia kuwapongeza kwa dhati kwa kuweza
kuchanganua mambo hadi kuweza kufikiria juu ya uhalifu mtandao ambapo ni hatua nzuri ya uelewa wa maswala ya usalama mitandao
nchini.
Aidha,
Nimefahamishwa kua tayari taarifa kuhusiana na tukio hilo lilio ambatana na
taarifa zilizo sambazwa limetolewa ufafanuzi na uongozi wa benki hiyo kwa
wateja wake. Na Pia Nitafurahi sana kuona pakiwa na wa Tanzania wakiendelea
kutaka kujuua zaidi kuhusiana na maswala ya usalama mitandao.
Nifungue Mjadala - Mawazo , maoni, na Maswali Pia Kuhusiana na Nilicho andikia ili kuongeza ufahamu pale inapo stahiki.
ReplyDeleteboss nakukubali sanaaaa
DeleteNashkuru Sana Piter! - Ni Kuweka tu mambo sawa!!
Deletekaka pamoja na kutolea ufafanuzi vizuri hili tukio la NBC naomba tukubaliane tu kua mabenki yameendelea kuibiwa sana tu ingawa ndio hawasemi na wamekua wakiugulia chini chini.
DeleteMi nadhani imefikiau tuweze kuona taifa kama taifa lina adress hili swala kipekee na pakaonekana kunakila haja ya kulipatia uzito swala hili na shauri tu kaka naimani na wewe umekua ukiliona hili.
Tunashkuru sana kwa ushirikiano na Jitihada zako katika suala la Uhalifu Mtandao. Ni suala ambalo limekua tishio sana Ulimwenguni kote.
ReplyDeleteAhsante kwa maoni Hamza - Ni Jukum maana Mwisho wa siku Taifa salama Na bara Salama Kimtandao ndio Target ya Muhim.
DeleteKAKA KUMEKUA NA CHANGAMOTO SANA HASA KATIKA MABENKI KUNA JITIHADA ZOZOTE ZIPO KUKABILIANA NA MATATIZO TUNAPIGWA SANA PESA ZETU KAKA.
ReplyDeleteAhsante sana Kwa Maoni John, Lakini Pia Nikujulishe tu kwmba Si Mabenki pekee na maeneo mengine mengi kwani kwa sasa Uhalifu mtandao ndio umekua na nafasi kubwa sana.
DeleteAidha, Kwa Upande wa jitihada zipo za dhati na kumekua na namna mbali mbali za kuweka mambo sawa jitihada ambazo zinaendelea maeneo mengi.
Tanzania - kumekua na Mipango pia huku mengi yakiendelea kuwekwa sawa.
N.B: Jukumu la Usalama Mitandao ni vizuri ikajulikana si la aina flani tu ya watui bali ni lakila mmoja wetu kuhakiki anachukua tahadhari stahiki ili kubaki salama kimtandao.
I also experienced changes in my account balance from Friday last week, unusual transaction happened in my account at NBC, may be this is due to one of the above reasons KILEO, I left it to NBC management, but we need to put more emphasis on cyber security especially to our young growing countries in Technologies like Tanzania. Security against hackers and Systems attacks matters in Financial Organizations esp banks. Thanks
ReplyDeleteI have learned about this situation Yesterday - Last Friday I'm not sure, It might another reasons as well.
DeleteAnd we should remember Online theft / Fraud is Still there And that's why - Training, Awareness , Cyber laws and other measure to combat cybercrimes not only in Tanzania but also other parts have to be in place to make sure we meet the target ( Safer Africa and world at large ) when it comes to cyber.
Hapo mtandao wa benki haujakaa vizuri. Kuliko mtu apate ujumbe wa salio ambao sii sahihi ni bora asipate huo ujumbe mpaka pale mtandao utakapokaa vizuri
ReplyDeleteNashkuru Emmanuel, Na Kikubwa ni kwamba Matatizo ya Kiufundi katika mitandao ni Jambo la kawaida na ndio maana kuna watu wanashughulika nayo pale tatizo linapo jitokeza.
DeleteNaimani Wakati mwingine measures zaidi zitachukuliwa kuepukana na tatizo lililo jitokeza sasa.
Samahani. Mm ni mteja wa Nbc na nina tatizo la online internet banking toka July 2014. August 7, 2014 Nimewasiliana na wahusika wakanieleza taratibu za kufanya ambazo hazikuweza kutatua tatizo. Mpk sasa hivi sina hio huduma. Ss na wasiliana nao lkn wako kimya je nifanyeje ili niweze kupata hio huduma ikiwa sipati ushirikiano na NBc. Na mm niko nje ya Tanzania.
DeleteSina Hakika Tatizo hapo ni nini - Labda Ni costumer care tu!
DeleteWalipaswa kukupa maelekezo - Aidha nadhani Kwenye site yao kutakua na maelezo.
Naimani Utapata Ufumbuzi Soon.
Pole na Tatizo hilo.
Kwa kweli hii ni huduma yao si ya kuridhisha. Ukweli ni kitu cha msingi. Mm naona km kuna tatizo kwann wasieleze. Wanaishia kukata mawasiliano bila ufumbuzi wa tatizo la mteja. Kwanini watanzania hatusemi ukweli. Ss kuna faida gani kuweka hela bank ya nyumba ni halafu huna access yoyote zaidi ya a ATM isiyokueleza una kiasi gani na all transactions ulizofanya. NBC mnatushangaza.
DeleteUfumbuzi wa kupatakana soon siijui unamaanisha lini maana sasa huu ni mwezi wa tano nina hili tatizo na Nimewasiliana nao kwa simu na emails bila mafanikio. Tena ukiongea nao kwa simu majibu ni kama dakika au siku tu watakuwa wamekutatulia tatizo lkn hakuna kitu. Sasa hivi ni mwezi wa kumi mwisho kujibu email zangu nikiwaandikia hawa jibu . Nashangaa sana ni mteja gani anaestahili kuhudumiwa na yupi hatusemi kuhudumiwa.
DeleteBasi NBC it uweke wazi tujue
Kwanza Kabisa naomba niseme siko NBC - ila pia naweza kuwa msaada maana na wa NBC maoni haya wangeweza kuyafanyia kazi kama ungeweza kueleza details ulizokuwa ukitumia, Tatizo na nani ulikuwa ukiwasiliana nae - na mimi niangalie namna ya kukuunganisha na mwingine atakae weza kukupa msaada wa haraka.
DeleteKwa Mara nyingine Pole sana kwa tatizo unalo lipata.
Vizuri umesema hauko NBC ila nina imani km ulivyoamua kuchangia mjadala humu ndani basi waweza kutufikishia ujumbe au kilio changu mteja wa NBC. Ukweli ni kwamba nimefanya taratibu zote za kufuatilia hili tatizo kwa kupiga simu NBC mako makuu nikaunganishwa na wahusika na ndipo nikapewa email za kutuma information zangu. Na zilipokelewa na ndipo waliponitumia details zote za kujiunga tena. Lkn ilishindikana. Nikawaarifu wakasema walikosea namba ya simu. Nikawapa lkn kutokea hapo imekuwa dili dale nyingi bila msaada. Mm ningependa u nipatie namba ya muhusika mkuu wa online internet banking na information zaidi nimtafute. Nimpe vielelezo vyote vya kuonyesha hali halisi ili nipate hio huduma.
Deletenbc bado mnaibiwa japo mtaki kuwambia wateja ukweli.badilisheni system zenu
ReplyDeleteUlichozungumza kinaendana sambamba na wito wa wataalam wa usalama mitandao amabapo tumehimiza sana si sehemu moja bali maeneo yote ya kifedha kuhakiki ya kua wanatoa taarifa zao sahihi wanapo kumbwa na matatizo ili wana usalama mitandao waweze chukua hatua stahiki - Kuna Task force maalum zinazo kabiliana na maeneo Hatarishi kimtandao katika nchi za Afrika na ndio maana tuna sisitiza hilo.
DeleteAidha, Ni kweli takwimu za Kidunia zinaonyesha Financial istitution ndio zimekua kinara katika kuathiriwa kimtandao.
Nashkuru kwa maoni yako.
Ukiangali kwa tanzania kuna usalama kweli wa fedha zetu au ndio mabenki yanalizwa na kuingia hasara kimya kimya? Kuna jitihada zozote zipo maana mimi sijaona mambo haya yanazungumzwa sana zaidi nione wewe ukiyazungumzia na baadhi ya watu wengine wachache sana.
ReplyDeleteKwanza Kabisa Nashkuru sana sabrina Kwa Maoni Yako - Yamenifurahisha sana.
DeleteNimekua nikieleza mara kwa mara Mabenki kote duniani yamekuwa yakiathirika sana kutokana na wahalifu mtandao moja ya wanavyo vitaka ni pesa (Kiba/Kujipatia pesa kirahisi) na Mabenki ni hadi wataalam wagundue na kuzungumzia ila hakuna Benki Duniani inapenda kushare kirahisi taarifa za kihalifu wanazo fanyiwa - Kwa maana Hiyo Mara nyingi Jitihada zipo za kuangaika kupata Majibu ya matatizo na wataalam koto tukutanapo kubwa tunaliangali swala la kuhakiki Fedha zetu zinabaki salama ( Hii ndio imepekelea si tu majarida bali na maafunzo kadhaa ndani na nje ya Tanzania Kuendelea kwa sasa)
Kwa kusema Hivi Naweza kujibu swali kuwa NDIO - Kunajitihada za dhati zinaendelea Mifano Michache ni kwamba: -
1. Kume kuwa na awareness Program kadha zinazorushwa kupitia Luninga na Tuna mpango Wa Kufanya Nyingine Kubwa mwezi Huu ambapo itashirikisha Watu wengi.
2. Kumekuwa na Maswala ya Kuongezea uwezo wataalam wa ndani ( Capacity building) na Hivi karibuni COSTECH kwa kushirikiana na COMSAT walifanya warsha moja Nzuri tu.
3. Kuna Sheria Tatu Mtandao tunazitegemea Bunge Lijalo zijadiliwe ambapo naimani itakua na majibu mazuri kwa wa Tanznaia.
4. Tumeanza mipango ya Kushirikisha Wengine ili kupata kubadilisha taarifa na ujuzi na Mataifa Mengine na Hili Nategemea litakua endelevu.
5. Kumekua na Mambo kadhaa ambayo yanafanywa sasa Kama Ku register Simu n.k yenye malengo ya Kuweka Mambo sawa Ki usalama Mitandao.
Hii Ni mifano Michache ingawa bado kuna Juhudi Nyingine tunaendelea nazo na Naomba Nisistize swala La Usalama Mitandao si kwa aina fulani ya watu ni jukumu la KILA MMOJA wetu.
Kama Kuna swali lingine au kama utataka nitolee ufafanuzi baadhi ya Mambo Nitafanya Hivyo.
Ahsante.