WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Wednesday, 31 December 2014

TU UFUNGE MWAKA KWA KUJIHADHARI NA UHALIFU MTANDAO

Mwaka 2014 Umekua Wenye changamoto nyingi sana kwenye upade wa mitandao ambapo wahalifu mtandao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuitikisa anga ya usalama mitandao duniani kote ambapo walifikia kutamba kuwa wameshinda mapambano na wanausalama mitandao.

Kubwa zaidi ni uelewa mdogo wa watumiaji mtandao juu ya kujiweka salama kimtandao iliyo ambatana na wana usalama mitandao kuwa wachache sana katika ngazi ya kidunia huku baadhi ya mataifa kutotoa kipaumbele katika maswala ya usalama mitandao.

Aidha, Mengi katika jitihada yameweza kufikiwa ikiwa ni pamoja na Kikao cha funga mwaka cha tathmini ya hali ilivyokuwa kwa mwaka 2014 ambapo iliweza kutabiri hali ya uhalifu mwaka 2015 na kuweka mikakati ya dhati ya kukabiliana na hali hiyo kwa mwaka 2015 inayotegemewa kuwa na matokeo chanya. Kwenye hili unaweza kulisoma kwenye  “TAARIFA FUPI INAYOSOMEKA HAPA"

Wamarekani nao kupitia “US department of Justice” wameamua kuazisha kitengo maalum kitakachotoa msaada kwa mataifa yote duniani katika upande wa maswala ya usalama mitandao ikisisitiza itaangazia zaidi katika kuzuia matatizo kabla hayajatokea.

Tanzania nayo haikubaki nyumba kwenye hili, Tumeshuhudia warsha, semina, kongamano na mikutano mingine yenye malengo thabiti ya kukuza na kuongezea uwezo wa uelewa wa matumizi salama ya mitandao paoja kukuza uwezo wa kukabiliana na hali ya uhalifu mtandao nchini.



Sheria za usalama mitandao zimeweza kupaziwa sauti na kutoa matumaini makubwa kwa mwaka ujao, Huku vyombo vya habari kuw na jitihada ya dhati katika kampeni ya kutoa elimu na kuhabarisha jamii kuhusiana na janga la uhalifu mtandao linaloweza kuleta athari zaidi kwa taifa.

Nikumbushe tu, Uhalifu Mtandao umeendelea kuja kwa kasi ya juu na njia ambazo watanzania wengi wameweza kuwa waathirika. Kubwa nililoliona ambalo kueleke mwisho wa mwaka limeweza kukamata kasi ni pamoja na uhalifu aina ya “Phishing kama unavyo onekana kwenye picha nilizo tumiwa na baadhi ya raia wema ambapo wengi wameendelea kuathiriwa na uhalifu huu wa kimtandao.


Umakini zaidi unahitajika na tumalize mwaka kwa kuwa salama kimtandao.

No comments:

Post a Comment