WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday 12 December 2014

MCAFEE YASEMA VITA NA UJASUSI MTANDAO UTAONGEZEKA ZAIDI MWAKA 2015

Kumekua na wimbi kubwa la uhalifu mtandao unaofanywa na mhalifu kwa lengo la kujipatia fedha, taarifa na mambo mengine katika maeneo mbali mbali duniani. Katika mfululizo wa vipindi mbali mbali vinavyo weza kusikika "HAPA" nimeweza kueleza hali halisi huku kesho ya uhalifu mtandao kama ilivyo tabiriwa kupata kuangaziwa macho kwa karibu.

Kwa sasa kumeendelea kukua kwa uhalifu unao ihusisha nchi moja dhidi ya nyingine au kampuni moja dhidi ya nyingine yenye malengo ya kupata taarifa za ndani na wakati mwingine kwa nia ya kuangusha tu mifumo ya nchi/ kampuni nyingine kwa sababu mbali mbali.

Kupitia ripoti ya McAfee iliyo chambuliwa "HAPA" imetabiri aina hii ya uhalifu kati ya nchi na nchi au kampuni na kampuni kuongeza kasi zaidi mwaka wa 2015. Hili limeambatana na kitu kipya kilicho tambulishwa kama “Cybercrime –as – service” ambapo uhalifu mtandao utakua unatumiwa kama huduma. Haya yanategemea kuiweka dunia katika hali mbaya zaidi kimtandao.

Hadi sasa Tayari mataifa makubwa yame endelea na vita mitandao ambapo kumekua na taarifa mbali mbali ambazo zimeonyesha vita hivyo mitandao zinavyo athiri mataifa hayo makubwa.

Mifano michache ni pamoja na kuibiwa kwa taarifa za mitambo ya kivita ambapo imekua ikipelekea mitambo hiyo kudhibitiwa mifumo yake na kusababisha kuleta athari. Nilipata kuliangazia hili katika taarifa inayosomeka "HAPA"  Aidha, taarifa za siri zenye athari kiuchumi zimekua zikilengwa katika vita hivi mtandao. Wakati mwwingine kuingilia tu mifumo na kuisimamisha kufanya kazi.


Vita hivi vimekua vikiletea mataifa mbali mbali hasara kubwa ambapo makampuni katika nchi husika yameonekana pia kuathirika na vita hivi. Hili lilipelekea mataifa mengi kuwekeza zaidi si tu katika kuwa na mufumo thabiti itakayo wapelekea kuwa salama bali hata kuwekeza katika nguvu watu na kusaidia mataifa mengine yanayoweza kutumika kuangamiza mataifa hayo makubwa.

Marekeani ilionekana kuwa ya kwanza kuanzisha mafunzo na kitengo maalum kwa wanajeshi waliokuwa na kazi pekee ya maswala ya usalama ambapo walipatiwa ujuzi wa kuzuia na upambana kimtandao. Huku Urusi nan chi nyingine kubwa kuanzisha majeshi hayo.

Kufuatia kukua kwa majeshi mtandao katika nchi zilizo endelea pamepelekea kuonekana kutakua na uwezekano mkubwa sana mwaka huu ujao wa 2015 namna mbali mbali za kufanikisha vita hivi mtandao sambamba na ongezeko kubwa la mbinu ya kutumia mataifa dhaifu kimtandao kuwa kama njia ya kuathiri mataifa mengine katika vita mtandao.

Ushauri umetolewa kwa mataifa kuongeza nguvu na kuwekeza zaidi katika maswala ya usalama kwani athari nyingine inayoweza kutegemewa ni pamoja na kuingiza migongano kati ya mataifa rafiki katika mikwaruzo ya kisiasa kutokana na kuonekana kushiriki vita hivi mtandao bila ya kutambulika inawezekana kabisa mataifa hayo yametumiwa na mataifa mengine kutokana na udahifu waliyo kuwa nayo.


Zaidi ugaidi mtandao unao ambatana na mataifa madogo ambayo awali hayakua yanajihusisha na vita hivi mtandao yametabiriwa kukua kwa kasi kutokana na sababu niliyo ielezea hapo juu. Kwa kumalizia naambatanisha "MJADALA" niliofanya ikiwa ni katika kutolea taarifa ripoti ya mikutano ya kiusalama mitandao ya hivi karibuni ambapo nilichukua jukumu kubwa la kuwasilisha mada kwa wataala wengine katika mijadala mbali mbali iliyokua ikiendelea barani Afrika.

1 comment: