Wadukuzi
wa kichina katika utaftaji wa taarifa zihusianazo na mitambo inayo ongozea
makombora yanayotumiwa na wa Israel nchini palestina wamefanikiwa kuingilia
mifumo ya wakandarasi watatu wa ki Israel. Wadukuzi hao wa kichina
wamefanikiwa pia kupata kujua taarifa za mipango mingine yawa Israel pamoja na
taarifa nyingine muhimu za makombora yawa Israel.
Taarifa
hii imekua ikipokelewa kwa namna tofauti na makundi mbali mbali yaliyo onyesha
hisia zao kupitia mitandao huku baadhi wakihoji kama inaweza kuleta salama
katika hali ya mapigano yanayo endelea hivi sasa huko Gaza.
Kwa
mujibu wa taarifa inayosomeka "HAPA", imeelza wadukuzi hoa wana uhusiano wa
karibu na Jeshi la Uchina. Mwezi wa tano mwaka Huu 2014, Marekani ilitangaza
kuwatafuta wadukuzi wa tano wa kichina wakiwashtumu kuingilia mitandao ya
mifumo ya kimarekani. Taarifa hizo hazikuweka wazi ni taarifa kiasi gani
wadukuzi hao walifanikiwa kuzichukua huku ikisemekana taarifa 700 ndizo
zilizochukuliwa na baadae kuaminika huwenda ikawa ni zaidi ya idadi iliyo
tangazwa awali.
Kwa
mujibu wa mtafiti wa Chuo kikuu cha Kalifonia cha marekani bwana. John Lindsay
alipozungumza na "BUSINESS INSIDER" alielezea huwenda udukuzi huo unaambatana
na jitihada za wachina kujifunza zaidi maswala ya mifumo ya kuongozea mitambo
ya kivita.
Wakati
gumzo la Udikuzi huu ukiendelea kujadiliwa, baadhi wamekuwa wakisema ya kuwa wadukuzi
wakichina huwenda walivutiwa na mifumo hiyo yawa Israel ya kuongozea mitambo ya
kivita baada ya kushinda kwakwe mapigano ya mwaka 2012 dhidi ya wapiganaji wa
kipalestina.
Aidha,
Kampuni moja ya ulinzi ya Israel iliyohusishwa na sakata hili imesema hapakua na tahadhari
yoyote iliyotolewa kwa washirika wao wa kimarekani juu ya hali hiyo ya
kiusalama huku akielezea taratibu zimewekwa vizuri ili kuzuia hali yoyote
inayoweza kuhatarisha usalama wa mifumo yao.
Wakati
huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa CyberESI ,Joseph Drissel alieleza kuwa Nyingi
katika taarifa zilizoibiwa zilizuiliwa na Idara ya Marekani. "teknolojia nyingi za
Arrow 3 hazikutengenezwa na Israel, bali zilitengenezwa na Boeing na
makandarasi wengine wa ulinzi wa Marekani," alimweleza Krebs.
"Tulichokifanya
ni kuhamisha teknolojia tuliyokua nayo
kwa wamarekani, nao baadae ndipo walipokutwa na tatizo la kudukuliwa kwa
taarifa zao. Katika mchakato huo, pengine katika taarifa zilizo chukuliwa
zinaweza kua ambazo hutumika katika mifumo yetu pia. " Alimalizia Bwana
Joseph Drissel.
Marekani
ime endelea kuishutumu serikali ya Uchina kwa udukuzi wa aina hii ambao pia unahusisha mifumo ya
kuongozea ndege za kivita, Mbali na maafisa watano wakichina kushtakiwa mwezi
Mei. Pia mwezi Juni, Marekani iliwashtaki wadukuzi wengine wa kichina kama
kwenye taarifa inayosomeka "HAPA" inavyo jieleza kwa kirefu.
Kwa
upande wake, China imeendelea kukanusha madai haya ya wamarekani na waizrael,
huku ikisisitiza ni mbinu za nchi ya marekani kuzitengeneza njia ya kuziba
uhalifu wao wa kudukua taarifa za nchi ya china wanzo endelea nao hivi sasa.
Matishio mbali mbali ya kuathiri mifumo ya mimtadao ya wa Israel
yameendelea kuonekana kwa kasi hivi sasa. Hivi karibuni Kundi la Anonymous lilitangaza kuongeza mashambulizi mtandao zaidi kwa taifa la israil kufuatia
taifa hilo kuendelea kuishambulia Nchi ya palestina huko Gaza. Kenye taarifa
iliyoweza fafanuliwa vizuri "HAPA" ilieleza kundi hilo limewataka pia makundi
mengine kuunga mkono jitihada hizo ili kufanikisha mashambulizi yake kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment