Huduma
ya kufanya miamala ya kibiashara kupitia mtandao inafanya maisha ya leo kua
rahisi zaidi kulinganisha na maisha ya awali. Hii ni kutokana na uwezekano wa kufanya miamala hiyo popote pale
ilimradi tu uwe unamtandao.
Hili lakua na mtandao kwa Tanzania limeendelea kuwa
rahisi hasa baada ya mitandao ya simu kutoa huduma za wavuti inayo sababisha
takriban watanzania walio wengi hasa waishio mijini kuweza kupata huduma za
mitandao.
Kila
teknolojia inachangamoto zake. Na hii ya kufanya miamala kwa msaada wa mtandao
pia imekuja na changamoto kadhaa ambazo bado kuna tatizo kubwa la uelewa wa
jinsi gani ya kua salama pale miamala ya kibiashara inapofanywa.
Muamala wa
kibiashara unapofanyika vibaya unaweza kumgharimu sana mtumiaji kwa kupoteza fedha na hata kupoteza
utambulisho wake ( Hii ni pale taarifa zako kupatikana na wahalifu na kutumika
vibaya baadae).
Swala
la uhalifu mtandao unao athiri miamala ya kibiashara inayofanywa kwa msaada wa
mitandao hapo awali ulikua maarufu sana katika nchi za afrika magharibi hasa
Nchi kama Nigeria na Ghana – Unaweza
kusoma taarifa ya nchi hizo na hali ilivyo hadi sasa kupitia taarifa
inayosomeka "HAPA"
Aidha
Kwa afrika mashariki ikiwemo Tanzania, Hali Imebadilika na Hivi sasa uhalifu
huu umeendelea kushika kasi sana ambapo wahalifu mtandao wamekua wakielekeza
zaidi nguvu zao kuibia watu wafanyao miamala ya kibiashara kwa msaada wa
Mitandao. Hivi karibuni nilipata kuandikia taarifa ya uhalifu mpya unaokua kwa
kasi kama inavyosomeka "HAPA" nikifafanua hali halisi nchini hivi sasa kwenye
hili.
Hivi
karibuni Benki ya CRDB imewaonya wateja wake kuwa makini na baadhi ya mitandao
inayoibuka na kulaghai kwa kuwataka wananchi,kutoa taarifa zao muhimu za
kibenki,jambo ambalo linahatarisha usalama wa fedha zao zinazohifadhiwa na
benki hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Dr Charles Kimei alipolizungumzia hili jijini Dar es salaam
alifafanua kuwa kumeibuka mchezo kwa baadhi ya mitandao ya kijamii,ikijaribu
kuwalaghai wateja kwa kuwaomba taarifa za akaunti zao ili kufanya uhalifu.
Alisisitiza
wananchi wanatakiwa kuwa makini na kundi hilo,wasikubali kudanganyika kwa kutoa
taarifa zinazohusiana na nyaraka nyeti za benki zao na kusisitiza kuwa ni
marufuku kutoa taarifa hizo kwa wafanyakazi wa benki.
Mkurugenzi
huyo amesema pamoja na kwamba benki hiyo inawapigia simu wateja wao wakitaka
kukamilisha usaili wao kuhusiana na kuingia katika mfumo wa uboreshaji wa
huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi unaoitwa Simbaking watambue kuwa hawataulizwa kutoa taarifa
zozote za akaunti.
Kuhusu
mbinu zinazotumiwa na wahalifu,Mkurugenzi wa Idara Hatarishi James Mabula
amesema huwapigia simu wakijifanya kuwa wakurugenzi ama wafanyakazi wa benki
hiyo na kisha kuwaghilibu kwa kutaka kupatiwa namba za siri za akaunti husika.
Kwa
upande mwingine, Mitandao ya simu bado haijabaki salama – huduma za miamala inayofanywa kwa msaada wa simu pia
imeendelea kuathirika ambapo kila mara pameendelea kuripotiwa uhalifu katika
maeneo hayo.
Nilipata
kuandika mwishoni mwa mwaka jana Taarifa ya kingereza inayosomeka hapo chini
kuonyesha hali halisi na makabiliano yanayoendelea kudhibiti uhalifu huu
mtandao nchini Tanzania huku nikiambatanisha na mapendekezo ambapo juhudi za
dhati kuyaendea zinaendela ili kupata taifa salama kimtandao.
No comments:
Post a Comment