Miongoni
mwa makosa mtandao kuna lijulikanalo kama “Phishing” ambapo kosa hili limekua
likidumu kwa muda sasa katika nchi mbali mbali na kwa upande wa Afrika
ilizoeleka kuanzishiwa kutokea Naigeria pamoja na Ghana.
Nchi
mbali mbali zimechukulia uhalifu huu kua ni hatari kwani unaweza kuwa na madhara
makubwa kwa mtendewa ikiwa ni pamoja na kupelekea kufilisi mtu, kupata taarifa
za watu kinyume na sheria/ makubaliano na hata wakati mwingine kupelekea kuleta
madhara mengine kama kutumika kuhatarisha mifumo mbali mbali.
Kwa
kuzingatia hili nchi mbali mbali zimekua na sheria kali dhidi ya uhalifu huu ,
huku nchi za afrika kupitia umoja wa wataalam wa maswala ya usalama mtandao
kuanzisha kamati yenye watu maalaum kuangazia macho uhalifu huu na kutoa taarifa
huku hatua zikichukuliwa.
Makampuni
ya Ati-vurus nayo yametoa uzito kwenye hili na kuhakiki wanaunda nyezo
madhubuti za utambuzi wa aina hii ya uhalifu na mara kwa mara wakiwasilisha
ripoti zao.
Changamoto
bado zipo kutokana na upungufu wa uelewa kwa wananchi mbali mbali juu ya
uhalifu huu inayo sababisha waathirika kueendelea kuwa wengi kila kukicha.
Uchunguzi
umeonyesha mara nyingi panapokua na jambo linalo fatiliwa na wengi ndipo
wahalifu wanapenyeza hapo na kuanza kusambaza aina hii ya uhalifu. Nimepata
kuliandikia hili kupitia taarifa ya Uhalifu unao ambatana na World cup kama inavyosomeka
"HAPA" kwa kirefu.
Kwa
upande wa Tanzania pamekua pakizungumzwa mara zote matumizi mabaya ya mitandao,
yanapelekea uhalifu mtandao na hatua kali zitachukuliwa kwa wale wote watakao
bainika kujihusisha na uhalifu mtandao.
Ni
vizuri tukakumbushana Tanzania imesha kamilisha rasimu ya sheria za mitandao
ambazo zitatoa fursa kwa wahalifu kushughulikiwa ipasavyo na hivi karibuni TCRA
nayo ilizungumzia mpango wake wa kushughulikia watumiaji vibaya wa mitandao.
Hili likiwa linafuatia kampeni yao ya Futa delete kabisa.
Wakati
hili linajiri pamekua na wimbi la wahalifu wa uhalifu huu wa "Phishing" ambapo wana dukua na kuchukua akauti za mitandao za
watu na kuanza kusambaza taarifa zitakazo wawezesha kupata taarifa za wengine na maranyingine wanatengeneza akaunti feki za mitandao wakitumia majina ya watu maarufu na kuanza kuzitumia vibaya.
Pamekua
pakitumiwa majina ya watu mashuhuri na kutumia watu jumbe wakiwataka wa bonyeze
link ili kujiunga na huduma kama Vikoba, Pia wamekua wakituma ujumbe wakiwataka
watu wafungue tovuti n.k
Katika
kulikamilisha hili pamegundulika baadhi ya akaunti za watu tayari wameondolewa
umiliki na hatimae wahalifu wanazitumia kusambaza uhalifu huu. Pakumbukwe
linapokuja swala la usalama mtandao unapo chukua akaunti ya mtu ni kosa moja na
unapo itumia vibaya ni kosa jingine lakini pia unapo tumia watu jumbe kubonyeza
tovuti yeyote ni kosa jingine.
Hadi
sasa Baadhi wame toa taarifa kuwa akaunti zao zimechukuliwa, mfano kupitia
taarifa inayosomeka "HAPA" na huku baadhi wakitengeneza akaunti feki za majina
ya watu na wengine kutuma jumbe za Kiswahili fasaha zinazo onyesha uhitaji wa
kuendea tovuti mbali mbali.
TAHADHARI:
Kila mmoja anapaswa kua makini na unapo hisi ya kuwa unaweza ukawa muathirika
wa uhalifu huu mtandao basi badilisha neno la siri na siku zote jiepushe kujibu au
kufata maelekezo yatakayo kutaka ufanye kitu Fulani. Kutoa taarifa kwenye hili
kila linapo jitokeza ni muhimu sana ili hatua stahiki zichukuliwe.
Ili
kujua zaidi uhalifu huu na viambatanishi vingine vya uhali unao fanana na huu
unaweza kuusoma "HAPA" na pia nime ainisha namna ya kutambua barua pepe na
Tovuti zisizo sahihi katika kiambatanisho hapo chini.
Nashkuru sana Kwa Taarifa Kileo
ReplyDelete