Bwana. Joseph Tiampati |
Mashambulio
ya mtandao nchini Kenya yamekuwa ni zaidi ya nusu kwa mwaka uliopita, na nchi
kupoteza takriban shilingi bilioni 2 (dola milioni 22.8) kwa mwaka, hii ni kwa mujibu
wa ripoti ya usalama mtandao ya Kenya ya mwaka huu wa 2014.
Ikiwa
ni kipindi muhimu ambapo ripoti za
usalama mitandao katika ngazi mbali mbali zinaendelea kuwasilishwa, Kenya nayo imewasilisha ripoti yake ya mwaka 2014 huku ikiwa imeonyesha hofu kuzidi ya ukuaji ma uhalifu katika
usalama mitandao nchini mwake.
Ripori
hiyo inayoweza kupatikana "HAPA" imekuja wakati muafaka kwani Kenya ipo kwenye
mchakato wa kuboresha sera zake zihusuyo usalama mtandao na kuimarisha uwezo wake wa kupambana na uhali mtandao nchini humo. Ki undani katika hili
linasomeka "HAPA"
Akizindua
ripoti hiyo, Katibu Mkuu Habari na Mawasiliano na Teknolojia Joseph Tiampati
alisema wahalifu, ikiwa ni pamoja na magaidi, wameingia katika mitandao kufanya
shughuli za uhalifu, na aliyataka mashirika kudumisha mifumo mizuri ya usalama
kulinda dhidi ya mashambulizi.
Bwana. Kris Senanu |
Aidha,
Bwana Kris Senanu akizungumza katika uzinduzi huo ameeleza yakua Mitandao hii
leo imekua ni nyenzo muhimu katika ukuaji wa uchumi na pia kijamii pamoja na
kuzitaka kampuni za mawasiliano kuhakiki usalama wa mifumo yao iko vizuri ili
kuweza kukidhi mahitaji ya wateja wao.
Ripoti
hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Habari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
teknolojia ya habari na mawasiliano, ilieleza kulikuwa na mashambulio milioni
5.4 ya mtandao yaliyogunduliwa mwaka 2013, ukilinganisha na milioni 2 mwaka
2012, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti.
Ripoti
ilionyesha kwamba vitisho vikubwa katika usalama wa mtandao mwaka 2013 vilikuwa
ni udanganyifu wa wafanyakazi, vitisho vya mawasiliano ya simu, huduma za benki
katika mtandao, udanganyifu wa kifedha kupitia simu za mkononi na upelelezi kupitia
mtandao.
Idara
ya Uchunguzi wa Udanganyifu katika Benki iliripoti shilingi bilioni 1.49 (dola
milioni 7) ziliibwa kutoka katika akaunti za wateja mwaka 2013 pekee kupitia
mfumo wa udanganyifu uliofanywa na wafanyakazi, kwa mujibu wa ripoti.
No comments:
Post a Comment