WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday, 12 June 2014

ZAIDI YA DOLA BIL. 400 ZAPOTEA KUTOKANA NA UHALIFU MTANDAO

Pamoja na kua na ugumu wa kupata takwimu halisi za pesa zinazopotea kutokana na uhalifu mtandao, bado takwimu zimesisitizwa kutolewa kupitia ripoti ndogo ndogo zinazo andaliwa kwa ushirika wa makampuni ya usalama mitandao na hatimae ripoti ya pamoja (Kubwa).

Ripoti ndogo za awali tayari zimesha anza kutoka ,  hadi hivi sasa mbili kutoka MacAfee na pricewaterhousecoopers (PWC) zi mesha wekwa mitandaoni ilikutoa ruhusa kupitiwa na jamii mbali mbali huku ripoti nyingine zikiendelea kutengenezwa.

Katika ripoti ya MacAfee ambapo ilishirikiana na Center of strategic and international studies (CSIS) imeeleza zaidi ya dola bilioni 400 za kimarekani  zimepotea kutokana na uhalifu mtandao katika ngazi ya kidunia.

Katika ripoti hiyo pia pame ainishwa kile ambapo kimekua kikizungumzwa kila siku yakua uhalifu mwingi wa mitandao umekua hauripotiwi huku hamasa ikiendelea kutolewa kwa jamii za nchi mbali mbali kujenga tabia ya kuripoti matukio ya uhalifu mtandao kila yanapotokea.

Jamii inaporipoti uhalifu mtandao unaotokea inatoa fursa kwa walinzi mtandao kutambua maeneo hatarishi na kuweza kudhibiti ipasavyo ingawa, vita dhidi ya uhalifu mtandao imeendelea kuonekana ngumu kutokana na uhaba wa nguvu kazi watu.

Kwa mara hii Afrika imeshika nafasi ya mwisho kuathirika na uhalifu mtandao huku marekani ya kaskazini ikishika nafasi ya kwanza kwa mujibu wa takwimu za mwaka huu.
Utabiri uliofanywa kutokana na uhalisia wa uhalifu mtandao unavyoendelea kusambaa umesema mataifa tajiri pamoja na makampuni makubwa yanahofiwa zaidi kua hatarini kiusalama mtandao katika kipindi kijacho.

Ripoti mbali mbali zilizo wasilishwa zimeendelea kutoa mapendekezo yake (Mfano – Katika ripoti inayosomeka mwisho wa taarifa hii) ambapo mapendekezo mengi yameendelea kushabihiana ikiwa kubwa ni kukuza nguvu kazi watu katika maswala ya ulinzi mtandao.

Kupitia ripoti ya macafee wao wame sisitiza kuimarishwa kwa teknolojia (Kua na vifaa vya teknolojia vinavyoendana na wakati), kuimarisha  ulinzi mitandao na kukuza upatikanaji wa nguvu kazi watu wanaosomea fani hii ya usalama mtandao.

Aidha, Ripoti nyingine zimeendelea kusisitiza makubaliano ya pamoja ya mataifa yote kuunganisha nguvu na kutumia njia ya pamoja kukabiliana na uhalifu mtandao.

Kwaupande wa  nchi za Afrika, kwenye hili jitihada zinaendelea huku nchi mbali mbali zikiendelea kukuza uwezo wa ndani kukabiliana na uhalifu mtandao ikiwa ni pamoja na kuboresha sharia zake na kuimarisha uwezo wa watu wao kuweza kupambana na uhalifu matandao.

Tayari nchi kama Afrika ya kusini, Tanzania, Zambia, Ghana, Kenya, Rwanda na nyinginezo zimeendelea kulifanyia kazi hili katika ngazi ya kitaifa nani mategemeo kupitia njia sahihi nguvu ya pamoja itapatikana.

Ili kupata undani wa jitihada zinazoendelea katika nchi za Afrika pitia taarifa inayosomeka "HAPA" mwishoni kuna kiambapatisho kitakacho kupa fursa kuweza kufatilia jitihada za nchi nyingine kwa karibu. Huku Uingereza kutegemewa kushika nafasi ya juu dhidi ya vita ya uhalifu mtandao Taarifa inayosomeka "HAPA" na "HAPA" inafafanua hili.

Bado safari ni ndefu na wahalifu mtandao wameendelea kuja na mbinu mpya kila kukicha huku ikitabiriwa miaka michache baadae takriban makosa mengi yatakuwa yakitekelezwa kupitia mitandao (Mfano: Wizi wa pesa na magari , Kuuwa n.k) hili nimesha liandikia kirefu kwenye taarifa inayosomeka "HAPA"

Kwa kifupi yafuatayo yametiliwa mkazo kupitia taarifa zote zilizotolewa hadi hivi sasa.

Kukuza uelewa kwa jamii juu ya makosa mtandao (Cybercrime awareness campaign programs) – Matumizi ya vyombo vya habari na sekta nyingine zenye nguvu ya kuifikia jamii ni vizuri zikatumika.

Kukuza nguvu watu na kurekebisha mitaala ya mashule na vyuoni kuweza kuendana na mabadiliko ya teknolojia yanayo sababisha ukuaji wa uhalifu mtandao hivi sasa.

Kuboresha mifumo ya ulinzi mtandao na kuongeza matumizi ya vitu vilivyo ndani ya wakati na vilivyo pitiwa (kuchunguzwa kabla ya matumizi).

Kuunganisha nguvu katika ngazi ya mabara na hatimae kimataifa/ kidunia (muunganiko wan chi za ulaya tayari imeonyesha mfano kwenye hili)

Taarifa inayofanana na hii katika lugha ya kingereza inasomeka "HAPA" Ripoti ya  PWC inaweza kusomeka "HAPA" na Mcafee inasomeka hapo chini.

No comments:

Post a Comment