Polisi Wa kuzuia uhalifu Mtandao. |
Wakala
unaofuatilia matumizi ya mitandao duniani (IAB) umebaini watumiaji wa intaneti
nchini Kolombia wamekua ni asilimia 70 ya wakazi milioni 47 wa nchi hiyo huku
ikibainishwa ya kuwa nchi hiyo ukuaji wa uhalifu mtandao umeendelea kukua kwa
zaidi.
Mwaka
2011 Kolombia ilikua Nchi ya kwanza kuanzisha sera ya usalama mitandao katika
ukanda wan chi za latini amerika kupitia baraza la taifa la nchini humo
linaloshughulikia maswala ya sera za uchumi na kijamii (COMPES).
Kupitia
Sera hiyo, Paliundwa kikundi kinachoshughulikia maswala ya mitandao kilicho
unganishwa moja kwa moja na wizara ya ulinzi pamoja na polisi wa nchini humo
kupitia kitengo kinachojiusisha na maswala ya ulinzi mtandao.
Pamoja
Na jitada zote hizo bado nchi hiyo imeendelea kukumbwa na mamia ya uhalifu
mtandao unaofanywa dhidi ya raia wake na serikali ya nchi hiyo na ndipo palipo
anzishwa misheni inayotoa misaada ya kiufundi ya usalama mitandao jijini Bogota
nchini humo.
Kolombia waliunganisha nguvu na wataalam kutoka
nchi nyingine kuanzia tarehe 31 ya mwezi
machi hadi tarehe 4 ya mwezi aprili mwaka huu (2014) ili kupitia na
kuchambua hali ya usalama mitandao ya
nchi yake na kutoa mapendekezo stahiki.
Bwana
Belisario Contreras kutokea (CICTE)
alieleza ushauri na mapendekez yaliyo tolewa yataingizwa katika vitendo ili
kukabiliana na asakata la uhalifu mtandao nchini humo.
Aidha,
Erwin Doutzauer strampfer kutokea chuo kikuu cha Oxford alipokua akichangia
hali ya uhalifu mtandao amenukuliwa akisema kutokana na uhaba mkubwa wa wataalam
wa maswala ya ulinzi mtandao shabaya ni kuendelea kukuza nguvu watu na
kusisitiza changamoto kubwa iliyoko sasa ni kuingiza mafunzo ya usalama
mitandao kuanzia ngazi ya chini mashuleni ili kuwezesha vijana wadogo kujua
jinsi ya kujilinda mitandaoni ambapo ameeleza kumekua na kesi za watoto kujiua
kutokana na kile alicho kisema kama “Cyberbulling”.
Ufafanuzi wa hili kwa lugha ya kingereza
unasomeka "HAPA" na taarifa ya awali ya kingereza iliyo ainisha juhudi za nchi hiyo dhidi ya
mapambano ya uhalifu mtandao pia inapatikana "HAPA" .
No comments:
Post a Comment