Mahakama
katika nchi mbalimblai zimekua na taratibu zakukusanya vielelezo vya kidigitali
vitakavyo weza toa uthibitisho katika makosa mbali mbali ya kimtandao.
Mtandano wa kijamii
wa Facebook ulitakiwa kuwasilisha taarifa za wateja wake ambao walihusishwa na
uhalifu mtandao wa kujipatia pesa kinyume na sharia kupitia mtandao wa kijamii
wa facebook.
Mtandao
huo wa kijamii wa Facebook umekata rufaa dhidi ya amri hiyo ya mahakama ambapo ilitakiwa
kuwasilisha taarifa za watu takriban 400
waliouhusika na visa vya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Mtandao
huo wa kijamii ulisema kuwa ombi hilo la mahakama lilihusisha idadi kubwa ya
majina ya watu kuwahi kuombwa na shirika la kiserikali kutoka kwa mtandao huo
Picha
na ujumbe wa faragha pamoja na taarifa nyinginezo kuhusu watu hao
ziliwasilishwa kwenye mahakama mwaka jana, lakini mahakama ilitoa tangazo hili
wiki hii.
Uamuzi
wa mahakama ulitaja Facebook kama mhifadhi wa data za kidijitali.
Jaji
wa kesi hiyo alisema maana ya kuwa mhifadhi ni kwamba Facebook inapaswa kutii
agizo la mahakama la kutaka kufanysa msako.
Kesi
halisi ilichunguza visa vya watu kadhaa kudai malipo kutoka kwa mfuko wa taifa
kwa watu wenye ulemavu Marekani.
Lakini
akaunti zao za Facebook zilionyesha wakiwa hawana ulemavu wowote.
Mtandao
huo ulilazimishwa kuwasilisha taarifa kuhusu akaunti za watu 381 ambazo
mahakama ilisema zilikuwa na ushahidi kuonyesha watu hao walifanya uhalifu.
Baada
ya ombi lao la rufaa kupinga agizo hilo kukataliwa, Facebook ilitii amri ya
mahakama na kuwasilisha taarifa hizo ingawa ilisisitiza kuwa agizo hilo
lilikiuka katiba ya Marekani ambayo inazuia msako wowote usio na msingi.
Kesi
hiyo imekuwa ikisikilizwa faraghani lakini tangu Facebook kukata rufaa jaji wa
kesi hiyo aliamua kuendesha kesi hiyo hadharani.
Taarifa zaidi kwenye hili kwa kingereza zineweza kusomeka "HAPA"
Taarifa zaidi kwenye hili kwa kingereza zineweza kusomeka "HAPA"
No comments:
Post a Comment