Mbali
na midahalo, hatua mbali mbali za kukabiliana na uhalifu huu wa kimtandao kwa
sasa kumekuja na kasi ya kukuza nguvu watu ili kuongeza nguvu ya kukabiliana na
uhalifu huu wa mitandao kwenye taarifa ya "NSA-YA MAREKANI" imeweza kubainisha jinsi taifa hilo linavyo
ongeza mafunzo kwa vijana wapya na kuanzishwa program maalum katika vyuo ambapo
gharama za mafunzo hayo kwa vijana zinakua ni za serikali.
Hili
pia limeonekana kwa nchi ya Afrika ya kusini kupitia mpango wa mafunzo ya mwezi
mmoja ya jinsi ya kukabiliana na uhalifu mtandao ambapo yaliyodhaminiwa na
kupewa jina la kumbukumbu ya Mandela.
Elimu
imekuwa ikisambazwa kwa jamii kwa njia ya mbali mbali ikiwa ni kukuza uelewa wa
hali ya uhali huu mpya wa kimtandao ambao unaaminika kuwa ni tishio hivi sasa
wenye uwezo wakuleta madhara makubwa na hauna watu wakutosha kuweza kukabiliana
nao.
Hili
Limedhihirika kwenye hatua zinazo chukuliwa na "HOLLYWOOD" kutoa
elimu kwa jamii kupitia tamthilia na filamu mbali mbali, pia baadhi ya waimbaji kuingiza maswala ya ulinzi mtandao kwenye
nyimbo zao.
WITO
Imefika
wakati sasa kwa Tanzania nayo kuangaza macho kwenye swala hili la uhalifu
mtandao kwa kuhakiki raia wake wanapata elimu ya kutambua makosa mtandao na
namna ya kujenga hatua za awali kukabiliana nayo katika ngazi ya mtu binafsi.
Hili linaweza kufikiwa iwapo tasnia ya habari na sanaa itashirikishwa kwenye
hili.
Kuandaa
nguvu watu kwa kuweka mafunzo nchini ili kuwezesha vijana wengi nchi kujifunza
ujuzi huu pasi na kusafiri kwenda mbali kutafuta elimu ya maswala ya ulinzi
mtandao.
Mahitajio
ya wataalam wa maswala ya ulinzi mtandao yanazungumziwa kukua kwa kasi na hili
lilionekana kwenye taari niliyoiandikia "CYBERSECURITY
DEMAND" kwa kuliangalia hili uweo wa wataalam hauna budi kujengwa
kuanzia ngazi ya kitaifa ili kujengea utayari wa kukabiliana na uhali mtandao
pasi kuhitaji msaada kutoka kwa wataalam w a nje pale tatizo linapo kuwa nchini
– Tujipange na tujenge tabia ya kuzuia tatizo pasi kusubiri litokee na kuwa
kubwa.
Kuwa
na sharia zinazoenda na wakati katika maswala haya ya uhalifu mtandao, Nchi
nyingi hivi sasa zimeanza tena kupitia upya sharia zake za uhalifu mtandao na
kuziboresha kutokana na mabadiliko makubwa katika ukuaji wa teknolojia. Mfano
3D printa ambazo zimeonekana kuleta athari kubwa sana kwenye maswala ya usalama
mtandao yamepelekea mataifa kadhaa kupitia upya sharia zake.
Hili
pia limeonekana kwa nchi kadhaa ambapo hazikua na sharia rasmi kuingiza maswala
haya ya uhalifu mtandao ikiwa ni pamoja na "TANZANIA" ingawa
kwenye hili Tanzania bado ina safari kwa kupitia na kuborehsa kila inapo paswa
sharia hizi za mitandao kwani hazifanani kabisa na sharia za kawaida kutokana
na mabadiliko ya teknolojia kila kukicha ambayo yanaadhiri moja kwa moja
maswala ya uhalifu mtandao.
Kujenga
utamaduni wa kufatilia maangalizo mbali mbali ya kiusalama mtandao,
Inasikitisha sana kuona sit u Tanzania bali nchi nyingi kuwa karibu sana
kufatilia maswala tofauti tofauti mbayo huwenda si yamsingi kabisa na kutokua
na ufatiliaji wa maswala ya muhimu ambayo yanaweza kuathiri moja kwa moja
Maisha yetu ya kimtandao.
Ni
ukweli watumiaji wa mitandao nchini wamekua kwa kasi nani vizuri kila mmoja
wetu kujenga tabia ya kupitia pale taarifa za maswala ya uhalifu mtandao
yanapokua yakijadiliwa ili kupata uelewa wa kukabiliana nayo katika ngazi ya
mtu binafi.
Hii
pia iwawezeshe waandishi wa habari kujitahidi kufatilia na kuhabarisha jamii
juu ya maswala haya ya ulinzi mtandao.
No comments:
Post a Comment