WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Saturday, 7 June 2014

KUPERUZI KUPITIA WI-FI NI HATARI ZAIDI KIUSALAMA MTANDAO

“Pale mtumia mtandao anapotumia Wi-Fi ilikupata intaneti anajiweka katika hali tativu  kiusalama mtandao zaidi ya Yule anae tumia mtandao unaotumia nyaya za intaneti – Kwa lugha ya kingereza, wireless LAN is more vulnerable to cyber-attacks compare to wired LAN” – Yusuph Kileo.

Haya niliyabainisha wakati nazungumzia changamoto mbali mbali tunazokumbana nazo za kiusalama mtandao kupitia matumizi yasiyo salama ya Wi-Fi yanayo endelea kushika kasi kaika maeneo mbali mbali hivi sasa.

Ninapozungumzia matumizi yasio salama, Namaanisha watumiaji wengi wa Wi-Fi wamekua wakipendelea sana kutumia huduma za Wi-Fi zilizoachwa huru (Hazi hitaji Maneno ya siri kuweza kutoa ruhusa kwa mtumiaji kuzitumia) wanapokua katika viwanja vya ndege, mahoteli na sehemu nyinginezo.

UFAFANUZI:

“Wireless LAN” au wengine hupenda kuita “Wi-Fi” zimekua na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuruhusu mtu yeyote kuzitumia, kuweza kusababisha taarifa zinazo safirishwa kuonekana na mtu mwingine na mara nyingi kutumika kusababisha uingiliwaji wa mifumo ya mitandao unaowea kufanywa na wahalifu mtandao.

Niliasa na kusisitiza elimu kutolewa zaidi maeneo mbali mbali juu ya matumizi salama ya mitandao isiyo hitaji nyaya maarufu kama “Wi-Fi” hii ikiwa ni pamoja na kujizuia  kutumia Wi-Fi zisizo hitaji maneno ya siri  kwani mtu yeyote anaweza kirahisi kuona kila kinachosafishwa na mtumiaji.


Katika maelezo yangu niliweza pia kuonyesha kipande cha video (Kama kinavyo onekana hapo chini) iliyokua na makusudio ya kukuza uelwa kwa watumia mitandao juu ya athari za matumizi yasiyo salama ya “Wi-Fi”.


Aidha, Msisitizo zaidi nilitoa kwa wale wa miliki wa vifaa vinavyo weza kuruhusu mtu kuingia mtandao (Wi-Fi routers) kuwekea maneno ya siri ili kuongeza usalama wa taarifa zinazosafirishwa huku kile kijulikanacho kama “Encryption” kuingizwa katika vitendo hasa pale taarifa muhimu zinapo safirishwa.

MAZINGATIO:

1.     Yafuatayo ni mazingatio machache ambayo mtumiaji mtandao anapaswa kuyajua.
2.     Kunachangamoto kubwa sana za kimtandao kwa mtumiaji wa Wi-Fi.
3.     Hadi sasa hapaja patikana njia sahihi na nzuri ya kumfanya mtumiaji wa Wi-Fi kuweza kuwa salama kimtandao.
4.     Mtumiaji mtandao anapaswa kujenga tabia njema pale anapotumia mtandao
5.     Kuna njia baadhi ya njia tayari zimewekwa za kitaalamu ili kumuweka mtu salama mtandaoni – Mtumiaji hana budi kuziingiza katika vitendo.

JINSI YA KUJIWEKA SALAMA:

Ilikua salama Hizi ndio njia unazo paswa kuzijua
ü Wi-Fi salama huwa inaonyesha alama ya Kiufunguo au unapo taka kujiunga inakutaka kuingiza neno la siri “password”
ü Ili kugundua taarifa unazo ziingiza kwenye mitandao zinasafiri salama kua makini kuangali URL na hakikisha ina neon “HTTPS” njia hii inakuhakikishia unachosafirisha kinakua tayari kimefanyiwa “Encryption”
ü Matumizi ya “Anti-virus” zilizo ndani ya wakati “Updated” ni muhimu sana
ü Jiepushe kutoa taarifa zako kwenye mitandao kwa watu usio wajua
ü Jenga tamaduni za kufatilia kwa karibu taarifa ziusuzo maswala ya usalama mtandao ili kujua hali ilivyo.

MUHIMU:

Mtumiaji anapo tumia tovuti zisizo na URL inayo anza na neno “HTTPS” na zina mtataka
kuingiza taarifa zake mtandaoni (Mfano: Jina lako na Maneno ya siri au taarifa za kibenki)
unapaswa kutambua taarifa hizo ni rahisi sana kuonekana na mtu mwingine.
Kila siku wahalifu mtandao wanakuja na mbinu mpya ili kufanikisha uhalifu huu unaokua
kwa kasi sit u katika ngazi za kin chi au mabara bali duniani kote nan i muhimu sana kila
mmoja wetu kujenga tabia ya kufatilia kwa karibu sana taarifa za usalama mtandao kila
zinapotolewa.

MWISHO:
Swali la msingi nililopata kuulizwa mara kwa mara ni kua ninazungumzia nini juu ya hali
mbaya ya iusalam aambapo “HTTPS” nazo zilikumbwa na Tatizo hali iyopelekea kila
mmoja kutokua salama kimtandao? – Hili limefanyiwa kazi na hali kwa sasa imerejea pazuri
ingawa bado jitihada za dhati kuzuia tatizo kutojirudia zinaendelea kufanyika.
Ili kusoma kwa kina Taarifa iliyotolewa kuhusiana kuathirika kwa “HTTPS” unaweza
kuipitia "HAPA"

Na hapo chini unaweza kupata kusoma nilichokua nikikiwasilisha kwa lunga ya kingereza.

No comments:

Post a Comment