Bwana. Keriako Tobiko |
Mkurugenzi
wa Mashtaka ya umma ya nchini Kenya Bwana. Keriako Tobiko ametangaza kuanzishwa
kwa kitengo maalumu kitakacho pambana na
uhalifu mtandao katika ofisi yake. Amedai hatua hii imefikiwa kutokana
na kuongezeka kwa idadi ya uhalifu unaofanywa na wahalifu wenye uelewa wa
teknolojia.
"Kwa
mtazamo wa kuongezeka kwa uhalifu wa mtandao, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka
wa Umma (ODPP) imeanzisha kitengo maalumu kusimamia mashtaka ya wahalifu wa
mtandao," Tobiko alisema, kwa mujibu wa The Standard la Kenya.
Takwimu
zinaonyesha Kenya inapoteza kiasi cha shilingi bilioni 2 (Dola milioni 23.3)
kwa mwaka kupitia uhalifu wa mtandao." Aliongeza Bwana Tobiko.
Hata
hivyo, alisema, jitihada za kuwakamata na kuwashitaki watuhumiwa zimekua ngumu
kutokana na ukosefu wa sheria zinazofaa, zikiwaacha huru wahalifu kufanya
uhalifu wa mtandao ambao unatishia usalama wa taifa, miundombinu ya teknolojia
ya habari na mawasiliano pamoja na haki ya usiri wa raia.
"Kwa
kutambua kwamba kwa sasa kuna sheria zisizotosheleza za kushtaki uhalifu wa
mtandao, ODPP imeandaa warsha ya kupitia upya sheria zilizopo na kuandaa rasimu
ya mswada wa kina kuhusu uhalifu wa mtandao kulingana na taratibu husika za
kimataifa zinazofaa," Tobiko alisema, akiongeza kwamba matumaini ya kuwa
na mswada wa kina wa uhalifu wa mtandao yatakamilika mwaka huu.
Itakumbukwa
taarifa iliyo andikwa na tovuti ya
sabahi inayosomeka "HAPA" iliainisha nchi ya Kenya imekua ikikabiliwa na idadi
kubwa ya uhalifu kwa kutumia zana za teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo
uhalifu kuanzia ngazi ya wizi kuwaibia watumiaji wa simu hadi viwango vya juu
vya udanganyifu unaozigharimu taasisi za fedha mamilioni ya dola imeendelea
kushamiri.
Baadae
shirika la Umoja wa Mataifa la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) lilieelezea
wasiwasi wake kuhusu mifumo ya usalama wa mitandao na hatimae ITU ilisaini
makubaliano na Tume ya Mawasiliano ya Kenya (CCK) ya kuboresha ujuzi wa watu
wanaofanyakazi na Timu ya Kushughulikia Matukio ya Kompyuta.
Kwa
Upande wa Tanzania changamoto iliyokua ikirudisha nyuma juhudi za kupambana na
uhalifu mtandao imepatiwa suluhu baada ya kuwepo kwa kitengo maalum cha
kupambana na uhalifu mtandao ambacho kimejiri kwa muda sasa huku kikitegemewa
kuwa na ufanisi zaidi kutokana na
kukamilika kwa rasimu itakayowezesha waalifu kushughulikiwa kisheria. Taarifa
kuhusiana na hili inasomeka "HAPA"
Aidha
tukiangalia afrika kasi ya mapambano imeongezeka huku Afrika ya kusini
ikifanikiwa kubomoa kikundi cha wahalifu mtandao waliokua wakiathiri sana nchi
nyingi – Taarifa hiyo ya afrika kusini inasomeka "HAPA" Rwanda nao hajabaki
nyuma kasi ya kuendana na ulimwengu wa “DOT” com pamoja na kuongeza nguvu
kupambana na uhalifu mtandao imeonyesha kuchukua sura mpya – Taarifa ya hili
inasomeka "HAPA"
Napenda
kumalizia kwa kutolea mfano wa Ghana kupitia taarifa inayosomeka "HAPA"na
kuendelea kutoa wito kwa wananchi kutambua ya kua swala la uhalifu mtandao
linakua sawa kabisa na teknolojia inavyokua na changamoto za mapambano ni kubwa
kama inavyosomeka "HAPA" huku tukiwa nanguvu watu wachache sana kuhimili
changamoto hizo hivyo mafunzo zaidi yanaendelea kutolea maeneo mbali mbali na
hili litaenda sambamba na kila mmoja kujenga tabia ya kujifunza maswala ya
husuyo namna ya kujiweka salama kimtandao walau
kwa uchache .
No comments:
Post a Comment