WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday 12 June 2014

TANZANIA YAASWA KUJIFUNZA KUFUATIA KUKATAZWA MATUMIZI YA WINDOW 8 CHINA

Katika wiki chache zilizopita kulikuwa na msuguano kati ya serikali ya Marekani na China , Serikali ya Marekani inailaumu china kwa kufanya udukuzi kwenye kampuni zake na biashara nyingine huku china nayo ikiilaumu marekani taarifa juu ya hili inaweza kusomeka "HAPA" .

Uchina baada ya hali hiyo ikaamua kukataza matumizi ya windows 8 kwenye kompyuta zote za serikali na taasisi zote zinazopewa fedha na serikali ya nchi hiyo na hili linaweza kusomeka kwa kirefu na viambatanishi vingine "HAPA"

Serikali ya China na wataalamu wake kadhaa wanasema matumizi ya windows 8 ni hatari kwa usalama wao na ustawi wao , kwahiyo wamekataza na kuendelea kutengeneza program yao ya COS China Operating System kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na taasisi zake .

Kwan nchi za ulaya suala kama hili liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita , lakini umoja wa ulaya ulienda mahakamani na mahakama ikaamua Microsoft itoe source code kwa umoja wa ulaya ili waweze kubadilisha na kuweka mambo yao kwa maslahi ya umoja wa ulaya .

Kitu kikubwa ambacho serikali ya uchina inalalamikia kuhusu Windows 8 ni hii source code, serikali ya china inataka source code ya bidhaa hii ili iweze kuifanyia mabadiliko iendane na maslahi yake haswa kwenye mambo ya ulinzi na usalama .


Hapa nchini kwetu tumeona taasisi mbalimbali na wizara mbalimbali za serikali tena nyeti zikitumia bidhaa mbalimbali za windows bila kufanya mabadiliko yoyote kwa ajili ya usalama wao , tumeona watu haswa viongozi wakinunua kompyuta na vifaa vingine vya mawasilino na kuvitumia kuhifadhi taarifa nyeti bila vifaa hivi kuchunguzwa au kubadilishwa chochote .

Suala la serikali ya China lituamshe na tuanze harakati za kuangalia maslahi makubwa ya taifa wakati wa manunuzi na matumizi ya vifaa na program mbalimbali toka nchi za nje , program hizi na vifaa vyake vinaweza kutumika kwa urahisi kuhamisha taarifa na chochote kile au kufanya uhalifu bila mnunuzi au mtumiaji kujua .

Wakati serikali inafikiria kupeleka muswada wa sheria ya usalama wa mtandao bungeni , ni vizuri suala kama hili lijulikana na wataalamu watakaojadili sera au chochote kinachohusiana na usalama wa Taifa .


Huwezi kulinda taifa kama taarifa zako zinaweza kuchukuliwa au kuangaliwa na mtu akiwa popote duniani .

No comments:

Post a Comment