WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Wednesday 21 May 2014

SERIKALI NCHINI UCHINA IMEPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA WINDOW 8.

Nchini uchina kumezuka gumzo baada ya serikali kupiga marufuku matumizi ya Window 8 katika computa zote za serikali nchini humo. Taarifa iliyo chapishwa na “CHINA DAILY” ilibainisha uamuzi huo wa serikali uliowekwa kwenye tovuti ya serikali ya nchini humu ambapo ilisisitiza zoezi hilo hali husu komputa za watu binafsi isipokuwa zile zinazotumiwa na serikali.

Tangazo hilo la serikali linalosemeka “HAPA” limebainisha uamuzi huo wa serikali umekuja baada ya kufungiwa huduma za kiusalama kwa Window XP huku likiweka wazi ya kuwa wamefikia hapo kutokana na sababu za kiusalama mtandao. Komputa hizo za serikali zitakua ziki tumia Operating system nyingine yoyote isipokua Window 8 ilisistizwa.

Kwa sasa nchini uchina inasemekana Komputa nyingi za serikali zilikua zinatumia Window Xp ambayo imekua si salama tena kimtandao ambapo inaweza ruhusu mhalifu kupenya na kuleta madhara kwa mtumiaji hivyo kuongeza wimbi la uhalifu mtandao kwa sasa, hususan watumiaji wa Window hiyo iliyositishiwa huduma kwa sasa.

Kwa upande wa Microsoft, Imeonyehsa mshangao kuwa window 8 imeonywa kutumika nchini humo ilhali wanaamini iko salama na wanaipatia huduma zozote za kiusalama kila inapo hitajika, Msemaji wa Microsoft alinukuliwa akisema hivyo na kusisitiza ya kuwa Microsoft imekua ikitumia nguvu ya ziada kuhakiki bidhaa zake na huduma zake zinafikia kiwango cha matumizi kwa mujibu wa mahitaji ya serikali.



Uchina imeonyesha dhamira yake ya kuongeza nguvu katika kutengeneza Operating system zake zenyewe, huku Bwana Qi Xiangdong, raisi wa Qihoo 360, akieleza ni muda muafaka kwa makampuni ya nchi hiyo sasa kukuza utengenezaji wa operating system zake.


Kwa upande wa balozi wa uchina nchini marekani amesita kutoa kauli ya haraka ikizingatiwa kuwepo na hali isiyo njema inayo husiana na maswala ya kiusalama mtandao kwa nchi hizo mbili ( Marekani na Uchina) kama ilivyosomeka kwenye taarifa hii “ HAPA

No comments:

Post a Comment