Ransomware
Gang, imebashiriwa kuleta athari kubwa sana kwa watumiaji wa simu za androids. Kauli
hii iliainishwa na mkurugenzi mkuu wa Trend
Micro bwana JD Sherry baada ya kunukuliwa akisema mwaka huu wa 2014 watumiaji
simu wanategemea kuathirika zaidi kiusalama mtandao huku akionyesha wasi wasi
kuwa wateja/watumiaji wa simu hizo hawako tayari (bado hawajajipanga)
kukabiliana na changamoto hii ya kiusalama.
Kile
kilicho onekana sana kwa watumiaji wa komputa ambapo wahalifu wanazifunga
komputa kwa watumiaji makusudi ili kuwataka wahitaji msaada wa kufunguliwa na Ransomware
uhalifu huu umegeukia simu za viganjani
hivi sasa kutokana na ukuwaji mkubwa wa watumiaji wa simu za viganjani.
Nini Kinacho tokea?
Mara
tu “Reveton mobile” inapo athiri simu
itaonnyesha kwenye simu tahadhari isiyo sahihi ambayo chanzo chake kinaonekana
kutokea mahala ulipo / katika nchi unayo patikana zaidi inaonekana inatoka
katika chombo cha ulinzi na usalama mahali ulipo – hii imekua na usumbufu
mkubwa kwa watumiaji simu.
Palipo
hojiwa ni jinsi gani wahalifu wanaweza kujua mahali ulipo? – Bwana Bogdan Botezatu kutoka katika kampuni ya “Bitdefender”
inayo jihusisha na ulinzi mtandao maarufu kwa utengenezaji wa “Antivirus”
ijulikanayo kama “Bitdefender antivirus” alifafanua na kusema wahalifu hao wanatumia
“Geolocation” ambayo inamuwezesha mhalifu kujua muhusika yuko wapi.
Kisha simu hiyo inafungwa/ kujifunga na mtumiaji
kupata shida kufuingua hapo ndipo msaada zaidi utahitajika. Ili mtumiaji aweze kupata simu yake/ kuifungua
anahitajiwa kulipia kiasi cha dola mia tatu (300) kwa wahalifu mtandao kupitia
njia zisizo weza kugundulika kirahisi pale uchunguzi unavyotakiwa kufanya.
Mifano wa njia hizo umetolewa ni Paysafecard au uKash.
Nini
chakufanya?
Bado kuna jitihada za dhati kwenye hili ili kupata
ufumbuzi ila pia yafuatayo ni vizuri watumiaji simu wakazingatia.
1.
Umakini wa kujitahidi sana kuwa na matumizi
salama ya simu zetu za viganjani hasa kwa wale wanaotumia intaneti kuweza
kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki pamoja na kupata taarifa mbali mbali.
2.
Kujitahidi kutumia Antivirus katika simu na
hakikisha antivurus unayo itumia iko ndani ya wakati (Haijapitwa na muda) nan i
salama kwa matumizi.
3.
Jitahidi kuto
bonyeza links kwenye simu ambazo zinaonekana haziko salama hasa kwenye mitandao
hatarishi.
4.
Jitahidi
kujiunga na “wireless network” ambayo ina alama ya ufunguo kwani iko salama
vinginevyo unaweza kujikuta kila unacho safirisha na kupokea kinaonekana na
wengine. Aidha wigo la wahalifu kukuingilia linaongezeka. – Tazama Mfano wa
wireless salma hapo chini kwenye picha.
5.
Marazote unapo
pata tatizo la kiusalama mtandao sit u katika simu bali hata komputa jitahidi
sana kutoa taarifa katika kitengo kinacho husika na maswala ya ulinzi mtandao (
Kama Uko Ofisini) Na inashauriwa maswala ya kiofisi - hasa yanayo hitaji
umakini mkubwa si vyema sana kuyafanyia
kazi kupitia simu yakiganyani pale unapokua mtandaoni.
Taarifa hii pia nilipata kuiandikia kwa lugha ya
kingereza kama inavyo someka hapo chini.
No comments:
Post a Comment