WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday 22 May 2014

KESHO YA UHALIFU MTANDAO SEHEMU YA KWANZA - 1

Swala la uhalifu mtandao limezidi kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha pakizingatiwa ukuwaji wa mbinu mpya za wahalifu mtandao zinazo wawezesha kufikia malengo ya kuleta athari kimtandao hivi leo. Wakati huo huo vita ya uhalifu mtanda imeendelea kwa kasi katika maeneo mbali mbali duniani.

Mijadala, maazimio mbali mbali pamoja na kupitishwa maamuzi yakua mwaka huu wa 2014 kua mwaka wa vitendo kukabiliana na uhalifu vimeenda sambamba na ukuwaji wa kasi wa uhalifu mtandao hivi sasa.Tumeweza shuhudia matukio mbali mbali mara tu baada ya kauli ya pamoja tuliyoiweka ya kupitisha mwaka 2014 kuwa wa vitendo kupambana na uhalifu mtandao kwenye kikao maalumu tulichokaa mapema mwaka huu.

Mifano wa matukio hayo ni pamoja na tishio la simu za android kugubikwa na matukio ya kiusalama mtandao, Heartbleed iliyo athiri makampuni mengi, internet explorer iliyo rahisisha wahalifu kuingilia Kopyuta za watu, na hili la hivi karibuni la eBay kuingiliwa na wahalifu. Hii ni mifano michache ingawa ipo mingi mingine iliyojiri kwa kipindi hiki kifupi baada ya maazimio ya pamoja.

LEO KWENYE UHALIFU MTANDAO.

Inaaminika makosa mengi yaleo yanayofanyika na wahalifu hapo kesho yatageuka kuwa makosa mtandao. Napenda kuanza na mifano michache ikiwa ni pamoja na wizi katika mabenki hapo awali wahalifu walikua wakiingia moja kwa moja katika mabenki na kuiba pesa lakini hivi leo uhalifu huo umegeuka kuwa ma kimtandao na pesa nyingi zimekuwa zikipotea kupitia wizi wa ATM na kuibiwa mitandaoni. Itakumbukwa FBI walitoa takwimu na kusema wizi katika mabenki ambapo muhalifu anaingia moja kwa moja benki umepungua kwa asilimia 60.



Hivi sasa tayari kumekuwa na uhalifu unaokua kwa kasi hasa katika nchi za ulaya na marekani ambapo wezi wa magari hivi sasa wameamia kwenye wizi mtandao kwa kuweza kufungua milango ya magari pasi na kuwa eneo la tukio na bila kuwa mmiliki wa gari husika. Ripoti iliyotolewa na “TODAY NEWS" ambapo polisi wa marekani wameonyeshwa kushangazwa na aina hii mpya ya uhalifu mtandao.

Itakumbukwa katika mkutano uliyo aminika ni kihalifu mtandao wenye jina la “Black Hat hacking conference” ulitoa nyenzo kwa wahalifu mtandao zitakao wawezesha kufanikisha aina hii ya uhalifu  wa wizi wa magari kwa kufungua milango ya magari pasi na kuwa eneo la tukio. Uhalifu huu umewafanya wahalifu kuto pasua viyoo wala kutumia nguvu yoyote wakati wa kufaya uhalifu huo kitu ambapo Polisi wamekua wakionyesha wasi wasi mkubwa kwani Uchunguzi unakua ni wa shida sana.

Hiyo ni mifano tu ingawa ni wazi bado kuna mifano mingine ya uhalifu ambapo awali ilihusisha nguvu ila leo bahati mbaya imegeukia kwenye uhalifu mtandao. Hali imezidi kuongeza wasi wasi kwa wataalam wa maswala ya ulinzi mtandao huku tukiamini bado kuna mahitaji makubwa sana ya wataalam zaidi katika fani hii.

KESHO YA UHALIFU MTANDAO

Ni wakati sasa kwa kila mmoja kujua uhalifu mtandao situ ule unaofanywa kwenye komputa pale tunaposikia kuna wahalifu wameingilia tovuti au komputa za watu. Kufuatia umwagikaji wa vifaa vyerevu “Smart devices” uhalifu mtandao utazidi kuwa tishio kubwa sana hapo kesho. Na Hapa tunaangazia mifano kadhaa ya makosa ya kimtandao hapo kesho.

Kuteka njara, Kuna swali limekua likiulizwa na wahalifu yakua kwanini mhalifu ahatarishe maisha yake kwenda kuteka nyara ndege il-hali anauwezo wa kufanya hivyo bila kuwa katika ndege husika? Hili limeonyesha wasi wasi yakua wahalifu watakuwa na uwezo wa kuingilia mifumo ya ndege inayo iongoza na kuipeleka pale wanapo taka wao.

Kupandikizwa vitu hatarishi kwenye mili ya wanadamu, Hivi karibuni Chuo Kikuu cha Liverpool kimetoa kile kinachoitwa "NEW RESEARCH"  ambapo magonjwa yatakuwa na uwezo wa sambazwa kupitia “Wi-Fi” kwenda kwenye mili ya binadamu. Swala Hili lilipewa jina la “Human Malware” kama ilivyo kwenye “Computer Malware” ambapo ni Virus zinazo sambazwa kwenye komputa.

( Nitaendelea kuliandikia hili kadri siku zinavyo sogea ili kukuonyesha mifano zaidi na kusogea kwenye nini la kufanya na kadhalika) - To be continued.

No comments:

Post a Comment