Polisi
wa visiwa vya kifalme vya Solomon vilivyopo pasifiki ya kusini wameunganisha
nguvu katika mapambano dhidi ya uhalifu mtandao na kuelezwa ya kwamba nguvu
kubwa itasogezwa mashuleni ili kukuza uelewa wa maswala ya uhalifu mtandao (Awareness)
na kusisitizwa hiyo ndio itakua shabaha yao ya awali. Haya yamebainishwa na
Bradford Theonomi katika taarifa yake ya kingereza inayosomeka "HAPA" .
Kupitia
program ya mpango uliopewa jina la “Cyber
safety pasifika” uliopangwa kuwasaidia watoto, vijana
na wakubwa kutumia teknolojia katika hali ya usalama iliyojiri kuanzia mnamo
tarehe 19 -25 May mwaka huu (2014) ulilenga kuhakiki matumizi salama ya
mitandao visiwani humo unapewa kipaumbele na ukanda mzima wa pasifiki ya kusini
kwa ujumla wake.
Makubaliano
hayo yalifikiwa wakati wa mkutano ulio fanyika na kuwahusisha wakuu wa polisi wa
visiwa hivyo. Kauli mbiu iliyo someka kama “ Historia yetu, Utamaduni wetu na
mitandao yetu” Ilidahmiriwa kuhamasisha matumizi salama ya mitandao na simu
katika ukanda huo wa pasifiki ya kusini.
Bi. Juanita Matanga |
Bi.
Juanita Matanga, Mkuu wa polisi wa visiwa hivyo aliainisha utayari wa kujipanga
kukabiliana na uhalifu mtandao huku akitolea maelezo ukuaji wa kasi wa matumizi
ya mitandao na simu katika visiwa hivyo na duniani kwa ujumla. Aidha Alieleza
ukuwaji wa matumizi ya mitandao bahati mbaya wengi hawajui athari zake. Hilo
ndilo lililo wasukuma kuanzisha kampeni hiyo ya kukuza uelewa wa maswala ya
uhalifu mtandao (Cybercrime Awareness Campaign) visiwani humo.
Matanga
alisisitiza kampeni hiyo itakua endelevu na pia kutakua na kupitia sharia zilizopo
ili kuweza kuziboresha kuhimili makosa ya uhalifu mtandao. Alianisha pia katika
visiwa hivyo bado ukuaji wa kasi wa makosa ya kimtandao haujaanza kuonekana na
polisi visiwani humo wako katika kuhakiki wanakuza uelewa kwa raia wake ili
kuweza kukabiliana na hali hiyo – Kuzuia tatizo ni bora zaidi kuliko kusubiri
tatizo litokee ili kuanza kukabiliana nalo.
Mkuu
huyo wa polisi alianisha pia yakua nchi nyingine za ukanda huo wa pasifiki tayari wamesha kua na taratibu wa kuhamasisha matumizi bora ya mitandao kukabiliana na uhalifu mtandao (Cybercrime awareness programs) na umefika wakati visiwa hivyo navyo
kuingiza taratibu hiyo katika vitendo na kusisitiza tena kua swala hilo litakua endelevu.
No comments:
Post a Comment