Ni ukweli matumizi ya mtandao ni swala lisilo epukika katika kufanya mambo mbali mbali ya kila siku ikiwa ni pamoja na kufanya miamala ya biashara, mawasiliano, kuhabarisha na mengineyo.Taarifa ya awali niliyo iandikia kuhusiana na ukuwaji wa matumizi mtandao na athari zinazoendelea kukua inaweza kusomeka hapa “TANZANIA NA HALI YA USALAMA MTANDAO” taarifa iliyo weza kusomwa na kituo cha radio cha “CLOUDS FM” na kuandikwa kirefu kupitia “MWANANCHI”
Tishio jingene jipya la kiusalama mtandao
limebainishwa kwa watumiaji wa televisheni za Philips toleo la la mwaka 2013
maarufu kama “Philips smart TVs” ambapo wahalifu mtandao wanauwezo wa kuingilia
TV hizo na kuanza kurusha matangazo yao binafsi pamoja na kufatilia kila kinacho tazamwa na
mtumiaji.
Tahadhari
hii imetolewa ikiambatana na ushauri ambapo imeelezwa wahalifu mtandao
wanauwezo mkubwa sana wa kuleta athari kwa watumiaji wa televisheni hizo na
msemo “You have been watched” unaomaanisha unatazamwa kuanza kutumika kwenye
mitandao ya kijamii kuelezea hisia za waathirika.
Tayari
Kampuni ya Philips imekiri kuwepo kwa tatizo na kueleza kampuni hiyo ipo katika
jitihada za dhati kulitatua tatizo huku ikiwataka watumiaji wa Aina hii ya TV
kuzima Kinachijulikana kama “Miracast function” amapo hili linaweza kufanyika
kwa kufata maelekezo yafuatayo (Quick help: Press the HOME button –
navigate to Set up – select Network Settings – Select Miracast –
set to OFF). Kukiri kwa tatizo katika lugha ya kingereza inaweza kusomeka “HAPA”
VIDEO INAYO ONYESHA UHALIFU
UNAVYO FANYIKA.
No comments:
Post a Comment