Katika
sehemu ya kwanza ya habari hii inayosomeka "HAPA" na pia ilipata kusikika kwenye
kipindi cha redio cha Teknohama kama kinavyosikika "HAPA" nilizungumzia changamoto
za uhalifu mtandao hii leo na kugusia aina mbili za awali za uhalifu mtandao
unaotegemea kuongeza kasi hapo kesho.
Aidha katika sehemu hii ya pili nitajikita
katika mifano zaidi ya Uhalifu mtandao hapo kesho , kugusia mapambano yanayoendelea
katika kukabiliana na uhalifu mtandao kwa mifano nikianzia na huu unaosomeka "HAPA" na mwisho nitazungumzia wito wangu kwenye hili ili kuweza kupata taifa, Afrika
na Hatimae Dunia salama kimtandao . . .
Kuingilia kila kinachotumika
majumbani, Hili nalo limeanza kuleta wasi
wasi mkubwa ya kuwa wahalifu watafikia mahali waweze kuzima au kuwasha taa za
majumba ya watu bila wao kuwepo eneo la tukio Si tu kufanya hivyo hii itausisha
na kubadilisha vitu mbali mbali ndani ya majumba ya watu pasi na wao kuwepo
eneo latukio.
Hili limezungumzwa baada ya kukuwa kw kasi kwa kinacho julikana
kama “Smart Houses” ambapo tayari zimesha anza kutumiwa katika maeneo mbali
mbali. Nyumba hizi kila kilichomo ndani kina ongozwa na rimoti maalalum ambayo
inakua inahusisha mtandao, hivyo wahalifu wanapokuwa wameingilia mtandao wa
muhusika wanaweza kusababisha athari niliyo ieleza hapo juu.
Kuingiliwa kwa mifumo ya magari, Inagawa uhalifu huu si mgeni tayari ulisha anza kuleta athari katika baadhi ya maeneo kama taarifa inayosomeka "HAPA" ilivyo changanua kwa kina aina hii ya uhalifu. Pametabiriwa uhalifu huu kushika kasi zaidi hapo kesho.
Hili limeleta wasi wasi mkubwa sana kwa wataalam wa maswala ya ulinzi
mtandao ukizingatia magari mengi yamekua yakiwekewa mifumo ya komputa kuwezesha
mambo mbali mbali katika magari hayo. Mapema mwaka huu kulitokea tukio
maarafufu lililogundulika pale “Formula One racing team” waliposema wanaamini
mfumo wa kuliongoza gari waliyokuwa wanatumia lilikua na virusi.
Tukio hilo
lilipelekea kampuni ya “Ford” kuangalia upya magari yake kujua kama kuna
mengine yaliyokuwa ya meathirika na virusi na sasa hivi “Ant-virus” za magari
ziko mbioni kutengenezwa na inasemekana zitatumika kwa magari yote yenye
kutumia mifumo ya kidigitali.
Wizi wa utambulisho wa watu,
kwa sasa bado utambuzi kwa njia ya mtu alicho nacho (namaanisha, Macho, vidole
na vinginevyo) kutoa ruhusa kwa muhusika kupata huduma au kuingia katika
majengo haija shika sana kasi ingawa ndio njia imekua ikiaminika kuwa salama na
imeendelea kuonekana kutumika katika baadhi ya sehemu.
Kinachotokea ukusanyaji
wa taarifa hizi za watu “Biometric details” unapokamilika uhifadhi wa taarifa
hizi huwa unafanyika pasipo salama kutokana na kutokuwa na wizi wa taarifa
hizi. Hivi karibuni wasi wasi umeonyeshwa yakua taarifa hizi zitakuwa zikiibiwa
ilikuwapa ruhusa wahalifu kuzitumia kufanya uhalifu. Hili tayari lime anza
kuingizwa kwenye tamthilia mbali mbali ikiwa ni hatua za kuelimisha jaami dhidi
ya uhalifu mtandao.
Mifano
hiyo mitano ni baadhi tu ingawa tayari mijadala mbali mbali inategemewa kuanza
kujadili hali ya kesho katika maswala ya uhalifu mtandao. Na namna ya kuanza
kutengeneza mipango madhubuti ya kukabiliana nao. Hii ni pamoja kila nchi
husika kukuza uelewa kwa raia wake kuhusiana na changamoto za uhalifu mtandao
na kueleza kama ilivyo kwa uhalifu mwingine kuzuia kunaanzia nyumbani. Taarifa
maarufu iliyotolewa na " THE NEW YORK TIMES" imeliainisha hili.
No comments:
Post a Comment