Kwa mujibu wa tovuti ya "BBC SWAHILI" Serikali ya Kenya
imesema watu watakaopatikana na hatia ya kutuma ujumbe wa kingono kwa kutumia
simu za kiganjani na intaneti watafungwa Jela.
Adhabu hiyo itawahusu
wale wanaotuma ujumbe wenye picha za watu walio uchi na zenye mada ya ngono
nchini humo.
Maafisa wakuu wa
serikali wanasema kuwa yeyote atakayepatikana na hatia atafungwa jela kifungo
cha miezi mitatu kwenda chini.
Afisa mkuu kutoka tume
ya mawasiliano ya Kenya , Christopher Wambua, ameviambia vyombo vya habari
nchini humo ,kwamba watu wenye tabia hiyo ya kutuma ujumbe wa kingono ,pamoja
na picha zenye watu walio uchi ,watatozwa hadi shilingi elfu hamsini za Kenya
au dola miatano na themanini na nane za kimarekani sawa na shilingi laki tisa
arobaini elfu na mia nane za kitanzania kama faini au kufungwa jela.
Onyo hilo litawahusu
hasa wale walio na uzoefu wa kutumiana ujumbe kama huo kupitia kwa simu ya
kiganjani au kwenye intaneti.
Kwa mujibu wa taarifa
za serikali, kiwango ambacho watu hutumiana ujumbe wenye mada ya ngono pamoja
na picha za watu walio uchi, zao wenyewe au za mtu mwingine kwa simu zao za
kisasa ilipanda hadi asilimia sitini.
Hatua
zilizo chukuliwa na wengine:
Kwa muda sasa nchi kadhaa
zimechukua hatua ya kuhakiki wananchi wake hawapati nafasi ya kuperuzi mitandao
isiyo endana na maadili ya nchi husika ikiwa ni pamoja na nchi kama China na
Saudi Arabia. Wakati huo huo nchi mbali mbali zimeendelea kuhakiki picha
zisizofaa mitandaoni hazipatikani kwa watoto hasa walio chini ya miaka 18.
Maswala haya yamekua yakijadiliwa kwa kina
katika vikao mbali mbali vya usalama mtandao ikiwa ni pamoja na kikao cha “CYBERSECURITY EVENT” na pia riport ya Dr. Toure wa ITU aliyo itoa “GENEVA PRESS CLUB” ilipata kuainisha changamoto mbali mbali katika
swala hili. ITU Haikuishia katika maneno bali
imeweza kutilia mkazo zoezi la "COP" ili kuwalinda watoto
mtandaoni ambalo kw sasa lipo katika hatua ya kuridhisha.
No comments:
Post a Comment