Jumamosi tangazo hilo linalosomeka hapa "TANGAZO" limeweza kubainisha internet explorer toleo la sita (6) hadi la kumi na moja (11) yote yameweza kugundulika yanatoa mwanya kwa wahalifu mtandao kupenya kwa watumiaji na kuchukua taarifa zozote zitakazo patikana kwenye computer zao.
Aidha, Kampuni inayo jihusisha na na maswala ya ulinzi mtandao ya "FireEye" imeonyesha takwimu yakua asilimia 56 ya vi vinjari, hadi ilipofikia mwaka 2013 vilikua hatarini kuingiliwa na wahalifu. na kubainisha kwamba wahalifu wamekua na uwezo wa kutengeneza vivinjari visivyo sahihi vinavyo weza ruhusu wahalifu hao kuingilia computer za watu mara tu watumiaji wa vi vinjari hivyo wanapo vitumia.
Microsofti imeshindwa kupata suluhu ya tatizo hilo ambapo CERT ya marekani imetoa tahadhari inalosomeka hapa "CERT ALERT" yakuwa watumiaji vivinjari vya "internet explorer" wanapaswa kubadili vivinjari kwa sasa na badala yake watumie vingine kama vile (Mozilla fox, Google chrome n.k) hadi hapo tatizo litakapo rekebishwa na kutangazwa vingenevyo.
Aidha,Christian Tripputi Ametumia muda huu kuonya watumiaji wa Window XP yakuwa kwa sasa wako hatarini kwani hakuna tena huduma zitakazo endelea kutolewa kwa Window hiyo na wahalifu mtandao wamesha anza kuleta madhara kwa wote wanaoendelea na matumizi ya windo hiyo na kusisistiza hapata kuwa na msaada kwa waathirika. Taarifa ya awali niliyo andika dhidi ya matumizi ya Window XP inasomeka hapa "TAHADHARI KWA WATUMIAJI WINDOW XP"
Taarifa ya kingereza inasomeka kama ifuatavyo.
Taarifa ya kingereza inasomeka kama ifuatavyo.
UPDATES: Hatimae Microsoft wametatua tatizo lililoathiri watumiaji wengi Suluhisho la tatizo limepelekwa pia kwa watumiaji wa Window XP ingawa ilitangaza mapema kua haitotoa tena msaada wa kiusalama kwa watumiaji wa Window XP. Hatua hiyo imefikiwa kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo endapo suluhisho lisingetolewa kwa watumiaji wote.
ReplyDelete