WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Wednesday, 9 April 2014

USALAMA MTANDAO NA NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUTOA ELIMU.

Hali ya usalama mtandao ni dhahiri bado jitihada za dhati zinahitajika ili kuweza kuleta mabadiliko na kupata Tanzania salama kimtandao, Afrika na dunia kiujumla. Ili kuleta mabadiliko chanya jukumu la kutoa elimu halipaswi kubaki kwa mtu mmoja au kundii Fulani la watu bali ni lazima kuwe na kuunganisha nguvu ya pamoja kutoka katika kila mtu mmoja mmoja.


Miongoni mwa jitihada zinaonekana kwa vyombo vya habari na makundi mbali mbali nchini Tanzania kuanza kuona umuhimu wa maswala ya ulinzi mtandao ili kupata taifa salama kimtandao, Jitihada Zaidi bado zinaitajika ili jamii iendelee kujua Zaidi nini hasa umuhimu wa kujenga tabia ya kutumia mitandao kiusalama ili kuweza kuliweka taifa kuwa salama kimtandao.

Mfano wa mazungumzo kutoka katika kipindi cha radio "Daladala" kilicho pata mualiko kushiriki semina ya maswala ya ulinzi mtandao na kuweza kuwakilisha yale waliyo yapata kutoka kwangu baada ya vyombo vya habari kunihoji maswala mbali mbali juu ya ulinzi mtandao maara tu baada ya kumalizika semina hiyo.


Aidha bado naendelea kutowa wito kwa vyombo vya habari kuendeleza jitihada katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii ili kujua athari na nini kifanyike ili kupata taifa salama kimtandao. kwani ni dhahiri kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa kuweza kuhamasisha jamii kujua umuhimu wa uasalama mtandao.


Kwa upande mwingine, Tasnia za Sanaa pia zina nafasi kubwa sana katika kuleta mabadiliko katika jamii kwani nchi kubwa zimekua zikitumia sana tasnia za uigizaji kupitia tamthilia na muvi mbali kupata fursa ya kuingiza vipengele vyenye kugusa moja kwa moja swala la kutoa elimu katika jamii kuhusiana na maswala ya ulinzi mtandao.
Tanzania Haina budi kuiga jitihada hizi bila kungoja tatizo kuwa kubwa katika jamii yetu Tanzania. Kwa kuzingatia haya na kuweza kupata muunganiko wa nguvu kupigana na uhalifu mtandao na Imani mwisho wa siku taifa litaweza kupunguza uhalifu kimtandao.