Nikiwa na Maduhu mara baada ya mahojiano |
Mwishoni mwa mwaka jana 2013, nilipata mualiko wakuzungumzia kirefu maswala ya usalama mtandao ambapo pia nilipata kuweka mahojiano hayo kupitia moja ya maandiko niliyo andika kupita blog hii kama yanavyoweza kusomeka na kusikika kwenye mada yangu niliyo elezea na kufafanua kwa kina NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUTOA ELIMU USALAMA MTANDAO ambapo mlango wa muendelezo wa mjadala uliendelea na elimu kuzidi kutolewa. Aidha taarifa inayo husu nafasi ya vyombo vya habari vinavyoweza kutoa mchango mkubwa katika vita dhidi ya maswala mtandao ilinasomeka katika andiko linalopatikana VIJIMAMBO: USALAMA MTANDAO - VYOMBO VYA HABARI
Napongeza
vyombo vya habari nchini kuona umuhimu wa kuelimisha jamii kuhusiana na usalama
mitandao kwani kwa kufanya hivyo jamii inaweza kufungua macho na kuona nini
umuhimu wa kujiweka salama watumiapo mtandao.
Kwa
sasa hali ya usalama mtandao kwa mujibu wa twakwimu imekua ikiongezeka huku
aina mpya za kuweza kusababisha uhalifu zikiendelea kugundulika nabado jitihada
za dhati zinaendelea ili kuweza kukabiliana na hali ya uhalifu mtandao.
Kwa
upande wa mataifa mbali mbali jitihada znaonekana za dhati, hasa nikitolea mifano
vikao vya hivi karibuni katika ngazi ya kidunia nilivyopata kushiriki na kupata
kuunganisha nguvu na hatimae makubaliano ya msingi kufikiwa ya kuhakiki mwaka
2014 kuwa mwaka wa vitendo kuhakiki panaingizwa katika vitendo yale yanayo
jadiliwa.
Natoa
wito kwa watanzania kujenga tabia ya kujiweka salama kimtandao kwani athari
inayoweza kumpata mtu mmoja inaweza pia kupelekea watu wengine wengi kuathirika
kimtandao. Wahalifu mtandao huwa wanacho kitafuta ni upenyo kupita kwa mmoja tu
ili kujijengea mlango wa kuingia katika eneo wanalo panga kulidhuru.
Hivyo
swala la kuwa salama kimtandao halijalishi uko katika ngazi gani, ni swala la
kila raia kujua anapaswa kua salama ili kuweza kuwalinda na wengine.
Majadiliano mbali mbali yanaendelea ndani nanje ya nchi huku hatua stahiki za
kukabiliana na hali ya uhalifu mtandao ikiendelea kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment