Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), kwa kuzingatia kifungu 5 (b) na (e) cha Sheria ya Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania ya 2003 inatoa tahadhari kwa watumiaji wa huduma za
mawasiliano, wananchi na umma kwa ujumla kujihadhari na utapeli unaofanywa kwa
kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti kama ifuatavyo:-
1. Usimpe mtu yeyote
usiyemfahamu vizuri simu yako au kadi yako ya simu ili atumie.
2. Usitoe maelezo
yoyote kuhusu namba yako ya simu au taarifa za binafsi kwa mtu yeyote
anayekupigia simu kutaka taarifa hizo.
3. Usijibu ujumbe wa
simu unaohusiana na fedha zako hata kama namba iliyotuma unaifahamu.
4. Usitekeleze maagizo
yoyote yanayohusu fedha kwa ujumbe wa maandishi hata kama yanatoka kwenye namba
ya mtu unayemfahamu. Mpigie aliyekutumia ujumbe uzungumze naye.
5. Usitekeleze maagizo
yoyote kutokana na ujumbe wa simu za mkononi unaokutaka kutuma fedha kutoka
namba ambayo mtumiaji wake unamfahamu na ambao unakueleza kwamba simu yake ina
hitilafu hivyo hawezi kuongea, usitekeleze maagizo hayo.
6. Ukipata ujumbe
kwamba umepokea fedha kwa njia ya simu, mpigie aliyekutumia na usitoe pesa hizo
hadi uthibitishe kwamba zimetumwa kwa nia njema.
7. Weka njia za
kuthibitisha taarifa kabla ya kufanya miamala ya kifedha kutumia simu ya
mkononi.
8. Ukipigiwa simu na
mtu yeyote kuhusu masuala ya fedha, hata kama unadhani unamfahamu mtu huyo;
mpigie tena kwa namba yake unayoijua ili kuhakikisha kwamba ni yeye.
9. Iwapo unafanya
biashara ya huduma za simu hakikisha kwamba simu unayoitumia kwa miamala ya
kifedha ni tofauti na unayotumia kwa shughuli nyingine na hakikisha simu hiyo
haitumiwi na mtu mwingine
10. Tumia namba ya siri
ambayo sio rahisi mtu mwingine kukisia.
11. Usitoe namba zako
za siri unazotumia kwa huduma
12. Thibitisha na
hakiki namba ya mtu unayemtumia pesa au salio kabla ya kutuma
13. Ukipoteza simu au
laini yako ya simu toa taarifa kwa mtoa huduma wako na Polisi mara moja.
14. Ukifanyiwa uhalifu
ambapo simu au mtandao umetumika kufanyia uhalifu huo hilo nikosa la jinai. Toa
taarifa Polisi ili wahalifu wasakwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
15. Usipopata
ushirikiano wa kutosha kwa mtoa huduma wako katika kutatua taizo lako wasilisha
malalamiko yako Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Unaweza kuwasilisha malalamiko
kwa kutuandikia ( S.L.P 474 Dar Es Salaam); kufika ofisini makao makuu namba 20
Sam Nujoma Dar es Salaam au kwenye ofisi za Kanda na Zanzibar; kupiga simu (
namba 0784 558270 au 0784 558271) na kwa barua pepe (malalamiko@tcra.go.tz au
complaints@tcra.go.tz)
Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
No comments:
Post a Comment