Watumiaji
wa simu za mkononi wameendelea kukua kadri siku zinavyo endelea na kumekua na
maswali mengi jinsi gani mtu anaweza kubaki salama atumiapo simu za mkononi.
Hapa
nitaangazia uhalifu mtandao unao ambatana na simu za mikononi na njia za matumizi salama ya simu za mkononi.
Nianze
kuangazia uhalifu unaoweza kusababishwa na simu za mkononi.
Swapping:
Huu ni uhalifu mtandao unao kua kwa kasi hivi sasa maeneo mbali mbali unaotoa
fursa kwa mhalifu mtandao kuwa na matumizi ya simu ya mtu bila ya mwenye simu
kujua. Mara nyingi wahalifu mtandao wana lenga kuiba pesa au kuwasiliana na
watu wa karibu wa mtumiaji halisi wa simu ya mkononi kwa sababu tofauti
tofauti.
Hii
inatokea pale mhalifu mtandao anapo kua amepata namba yako ya simu na kusoma ratiba yako hasa muda gani unakua hauna
matumizi makubwa na simu – Baada ya kujua hivyo kupitia programu zilizopo sasa
zina mpa fursa kukutoa hewani na kuanza kuitumia namba yako ya simu ambapo anaweza kufanya mengi baada ya kua na
umiliki huo ikiwa ni pamoja na kutoa au kuhamisha pesa zako na pia kuitumia
vibaya simu yako.
Shoulder surfing:
Hii ni njia inayotumika na wahalifu mtandao kuweza kujua namba za siri
anazotumia mmiliki wa simu kwa kuangalia pale mtumiaji wa simu anapofanya miama
ya kifedha kupitia simu au kufungua simu yake.
Mhalifu
baada ya kupata taarifa hizo anaweza kukwapua simu hiyo na kuitumia vibaya
kwani tayari Alisha jua namba za siri unazotumia na pia kuweza kufanya miamala
na simu hiyo. Inashauriwa kuwa makini sana uwekapo namba za siri kwenye simu
yako kwa kuhakikisha hakuna anayeweza kutazama ufanyacho kupitia simu yako.
Mobile Keyloggers:
kwa sasa kumekua na mtindo wa namba tofauti tofauti kut umia wenzao link ambazo
maranyingi zimeambatanishwa na program inayo toa ruhusa ya kuweza kujua kila
kinachoandikwa na mtumiaji wa simu mara tu baada ya kufungua link hizo.
Kwakufanya
hivyo mtumiaji anaweza kuwa kila anacho andika mhalifu mtandao anakua
anafatilia au kujua – uhaifu huu umekua ukiathiri zaidi simu za kisasa maaru
kama Smart phones.
Inashauriwa
unapotumiwa message yenye kiambatanishi cha link kuwa makini hasa inapotoka kwa
usiye mfahamu hii ni pamoja na ujumbe unaotumiwa kwenye programu ya WhatsApp.
mSpy:
Hii niaina moja wapo ya program ambayo
inampa fursa mhalifu mtandao kuweza kufatilia kila kifanyachwa na mtumiaji wa
simu za mikononi. Inaweza kutoa fursa kwa mtumiaji wa simu ya mkononi kwa simu
yake kugeuzwa kuwa kipaza sauti na hatimae aliye mbali kuweza kufatilia
mazungumzo yoyote yanayofanya na mtumiaji wa simu hizo.
Aina
hii ya uhalifu umekua na uwezo mkubwa wa kuathiri simu za kisasa maarufu kama
smart phones haza zile zinazotumia program za Androids. Ikumbukwe situ simu
kubadilishwa kuwa kipaza sauti bali hata kuweza kufanya mambo mengi na mtu
aliye mbali na simu yako.
Inashauriwa
kuhakiki unakua na simu yako mara zote na kutowapa usio wafahamu kwani program
iayoweza kusababisha aina hii ya uhalifu inaweza tu kuanza kufanya uharibifu
maara baada ya mhalifu kuweza kuiweka mikononi simu yako.
Manythings:
Hii ni program ambayo ni mpya kwa sasa inayotoa fursa kuzifanya simu za kisasa
maarufu kama smart phones kutumika kama kamera za kiusalama “Security camera” Hii
inaweza ikapelekea simu hizo kuwa na matumizi salama au mabaya inategemewa na mtumiaji.
Matumizi
sahihi, Imekua inatoa fursa kwa simu za kisasa zilizo pitwa matoleo yake
kuendelea kuwa na matumizi kwani program hii inayotolewa bure inatumiwa pale mtumiaji anapokua na simu
mbili ya zamani asiyo itumia na ya sasa anayo
itumia.
Simu
hizo mbili zinawekwa program ambayo itamuwezesha mtumiaji kuweza kurekodi na
kufatilia kwa karibu matukio yote anayo taka kuyafatilia kama ilivyo CCTV hivi
sasa.
Matumizi
mabaya, Imesadikiwa kuwa wahalifu wanaweza kuingia na simu katika maeneo ambayo
wanayafanyia uchunguzi na kuziacha simu hizo kwa kigezo cha kuzisahau huku wakirejea
kwenye simu zao kuhakiki wanafatilia matukio yote yanayoendelea katika eneo
husika bila ya kugundulika kirahisi – Hili tayari limeweza kujiri mara tu baada
ya simu hizi za kisasa kuwezeshwa kurekodi matukio na mhusika kutumia simu yake
mpya kufatilia akiwa mbali kabisa na eneo.
Sasa
Niangazie njia salama za matumizi ya simu za mikononi maarufu kama “best practice”
Namba za siri:
Simu za mikononi zimetoa fursa ya kuweka maneno ya siri wakati wa kufungua simu
hizo na kwa watumiaji huduma mbali mbali mfano za utumaji wa pesa kupitia simu
zao. Namba hizo za siri ili kubaki salama nimuhimu ukawa muangalifu kwa
kutoweka mwaka wa kuzaliwa, namba zinazo fatana au namba yako ya simu.
Kwakufanya
hivyo utatoa ruhusa kwa mtumiaji asiye husika kuwa na uwezo mkubwa wa kubashiri
kirahisi na kuweza kusababisha ma dhara kwa simu yako ikiwa ni pamoja na
matumizi mabaya na hata kufanya vitendo vya wizi wa pesa kupitia simu yako.
Ujumbe mfupi wa maandishi:
Kumekua na wimbi la wahalifu mtandao kupitia jumbe fupi za maandishi wanaomba
taarifa binafsi za watu wakijitabulisha kama watu kutoka mabenki au sehemu
nyingine. Unashauriwa kuwa makini sana na usitoe kabisa taarifa zako binafsi
kwa Yule usie mjua kupitia ujumbe mfupi wa maandishi.
Pia
ina shauriwa kuto sambaza ujumbe wa maandishi usio kua na uhakika nao na
unaoweza kusababisha taharuki kwa wasomaji wa ujumbe huo. Kwenye hili pia
inashauriwa upatapo ujumbe mfupi wa maandishi kwa mtu asiye jitambulisha na
wewe kumfaham kutompatia majibu.
Weka simu yako karibu nawe muda
wote: Ifahamike aina nyingi za uhalifu mtandao unaofanywa
kupitia simu za mikononi unasababishwa na mtumiaji simu kuweka simu yake mbali
na yeye au kuwaazima simu kwa asiye wafahamu.
Kwenye
hili nitoe kisa kifupi sana, Kuna Mhalifu mtando alienda kwenye kibanda cha
kutolea pesa na wakati yuko katika jitihada za kutoa pesa alijifanya anampigia
anayehitaji kumtumia pesa na mawasiliano kutokua mazuri.
Baadae
alimuomba mhudumu wa kibanda cha miamala ya kifedha kumpatia simu yake ya
mkononi ili aweze kutumia huduma ya ujumbe mfupi wa maandishi. Baada ya
kupatiwa simu alicho kifanya ni ku rekebisha orodha za namba ya simu na baadae mtumiaji mwingine aliyekua amewekewa namba zake
pale kuanza kutuma jumbe akimtaka mwenye kibanda kuanza kuhamisha pesa
akionekana kama bosi wake tukio ambalo lilipelekea kiasi kikubwa cha pesa
kupotea na uhalifu huu kuripotiwa katika vyombo vya dola.
Funzo
hapo, Umakini wa kuwa karibu na simu yako muda wote na kuto waazima usie wajua
simu yako unaweza kukuepushia matatizo mengi sana ikiwa ni pamoja na matumizi
mabaya ya simu yako na hata kupoteza pesa ulizo zi hifadhi katika simu yako.
Kuwa makini sana na huduma ya “Bluetooth”
pamoja na “Wireless”: Simu nyingi za kisasa zimekua zikitoa
huduma hizi ili kurahisisha mawasiliano ya kusafirisha taarifa kutoka kwa mtu
mmoja kwenda kwa mwingine kwa haraka bila gharama yoyote.
Bahati
mbaya unapo kua umeweka huduma hizi wazi muda wote zinaweza kupelekea mhalifu
mtandao kuweza kudukua simu yako kirahisi na mara nyingine kukuwekea program
hatarishi kwenye simu yako ya mkononi bila ya wewe kujua.
Hii
ina mabatana na wale wanao penda kutumia huduma za Wi-Fi zinazotolewa katika
viwanja vya ndege au mikusanyiko ya watu. Huduma hii inapo chukuliwa kwenye
simu ikumbukwe inatoa fursa kwa mhalifu mtandao kupitia “Man in the middle
attack” kuweza kupata taarifa zako na kuzitumia atakavyo.
Inashauriwa
kuwasha huduma hizi za Bluetooth na Wireless pale tu unapokua na ulazima
kuzitumia na kujiepusha kabisa kutumia huduma za Wi-Fi za bure pasi na ulazima
hasa usafirishapo taarifa zako binafsi na za siri.
Kua makini na program za simu:
Imekua kawaida kwa watumiaji wa simu za kisasa kupakua program mbali mbali za
simu katika simu zao na wakati mwingine hata zile wasizo kuwa na matumizi nazo.
Ikumbukwe
si program zote ni salama na wakati mwingine program unayo ipakua na kuiweka
kwenye simu yako inaweza kua chanzo cha simu yako kudukuliwa na wahalifu
mtandao.
Inashauriwa
kuwa makini sana na kila programu unayo ipakua
katika simu zako maarufu kama Mobile Apps na uwe natabia ya kuikagua kwa karibu
pale unapokua na ulazima wa kuwa na program hiyo kwa kuangalia walio whi
kuipakua wameitolea maoni gani.
Tatizo letu kubwa ni kwamba tumekua tunatumia tu simu bila ya kujua mambo mengi sana
ReplyDeleteHii imetufungua macho sana mkubwa.
Big up.
Nashkuru kwa maoni Kassim.
DeleteNamna ya kujua kuwa simu yako ya smartphone imeingiliwa, mlio kama wa mtetemo (vibration) hutokea mwanzoni kabisa wakati unapiga simu au wakati unapokea.
ReplyDeleteunalizungumziaje hili mtaalam? kuna ukweli wowote?
nimeipenda mada yako ya leo Mtaalam.
kaka na mimi niliwahi kumuazima mtu simu akidai anataka kumtumia mama yake ujumbe amepatwa na matatizo kumbe alikua anakazana kuhamisha pesa.
ReplyDeleteMachale yalinicheza kumnyag'anya simu ghafla nikakuta alikua katika menu za tigo pesa nikaanza kumpigia kelele za mwizi ni hatareee.
Asante kwa elimu unayotoa mkuu,naombautupe elimu kuhusu sheria za Tanzania na namna ya kumshtaki mtu ambaye anakutumia msg za matusi na unamjua.
ReplyDeletePili naomba utueleze kuhusu usiri unaotakiwa katika mtandao.Tunaambiwa kuwa message zetu zinasomwa na wanaomiliki mitandao kama Voda,Tigo,na Airtel.Ni vipi tutakuwa salama na hawa watu wasisome message zetu?
Asante kwa maarifa unayotoa, na kushauri uendelee na tutauunga mkono. Nashauri pia mihutaasari ya masomo kuhusu TEHAMA KATIKA VYUO VIKUU NA TAASISI ZINGINE ITAZAMWE UPYA HAPA NCHINI, ILI ANAYEFUNDISHWA APATE MAARIFA MAKUBWA BADALA YA KUWA NA SIFA YA CHETI KIKUBWA! Kumbuka kwamba cheti cha elimu si elimu bali ni ishara ya elimu iliyojificha kwa kila binadamu! Kwa sababu utaalamu uhalifu wa wizi katika mitandao ya mawasiliano umeanzia Nchi za nje ambazo zinategemea sana viwanda katika uchumi. Inaonyesha wazi kwamba Nchi hizo zimetuzidi katika ujuzi na maarifa makubwa na lazima TUWEKEZE KWA NGUVU KATIKA UTOAJI BORA WA ELIMU KUJARIBU KUWAFIKIA WENZETU.
ReplyDeleteNawashukuru wote kwa maoni yenu mazuzuri - nimeyapitia kwa karibu na najitahidi kuyaingiza katika vitendo kufikia malengo.
ReplyDeleteNawatakia Siku njema.