WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday 23 January 2015

BAKI SALAMA KIMTANDAO UTUMIAPO SIMU ZA MKONONI

Watumiaji wa simu za mkononi wameendelea kukua  kadri siku zinavyo endelea na kumekua na maswali mengi jinsi gani mtu anaweza kubaki salama atumiapo simu za mkononi.
Hapa nitaangazia uhalifu mtandao unao ambatana na simu za mikononi na njia za matumizi salama ya simu za mkononi.

Nianze kuangazia uhalifu unaoweza kusababishwa na simu za mkononi.

Swapping: Huu ni uhalifu mtandao unao kua kwa kasi hivi sasa maeneo mbali mbali unaotoa fursa kwa mhalifu mtandao kuwa na matumizi ya simu ya mtu bila ya mwenye simu kujua. Mara nyingi wahalifu mtandao wana lenga kuiba pesa au kuwasiliana na watu wa karibu wa mtumiaji halisi wa simu ya mkononi kwa sababu tofauti tofauti.

Hii inatokea pale mhalifu mtandao anapo kua amepata namba yako ya simu na kusoma  ratiba yako hasa muda gani unakua hauna matumizi makubwa na simu – Baada ya kujua hivyo kupitia programu zilizopo sasa zina mpa fursa kukutoa hewani na kuanza kuitumia namba yako ya simu  ambapo anaweza kufanya mengi baada ya kua na umiliki huo ikiwa ni pamoja na kutoa au kuhamisha pesa zako na pia kuitumia vibaya simu yako.

Shoulder surfing: Hii ni njia inayotumika na wahalifu mtandao kuweza kujua namba za siri anazotumia mmiliki wa simu kwa kuangalia pale mtumiaji wa simu anapofanya miama ya kifedha kupitia simu au kufungua simu yake.


Mhalifu baada ya kupata taarifa hizo anaweza kukwapua simu hiyo na kuitumia vibaya kwani tayari Alisha jua namba za siri unazotumia na pia kuweza kufanya miamala na simu hiyo. Inashauriwa kuwa makini sana uwekapo namba za siri kwenye simu yako kwa kuhakikisha hakuna anayeweza kutazama ufanyacho kupitia simu yako.

Mobile Keyloggers: kwa sasa kumekua na mtindo wa namba tofauti tofauti kut umia wenzao link ambazo maranyingi zimeambatanishwa na program inayo toa ruhusa ya kuweza kujua kila kinachoandikwa na mtumiaji wa simu mara tu baada ya kufungua link hizo.

Kwakufanya hivyo mtumiaji anaweza kuwa kila anacho andika mhalifu mtandao anakua anafatilia au kujua – uhaifu huu umekua ukiathiri zaidi simu za kisasa maaru kama Smart phones.

Inashauriwa unapotumiwa message yenye kiambatanishi cha link kuwa makini hasa inapotoka kwa usiye mfahamu hii ni pamoja na ujumbe unaotumiwa kwenye programu ya WhatsApp.

mSpy: Hii niaina moja wapo  ya program ambayo inampa fursa mhalifu mtandao kuweza kufatilia kila kifanyachwa na mtumiaji wa simu za mikononi. Inaweza kutoa fursa kwa mtumiaji wa simu ya mkononi kwa simu yake kugeuzwa kuwa kipaza sauti na hatimae aliye mbali kuweza kufatilia mazungumzo yoyote yanayofanya na mtumiaji wa simu hizo.

Aina hii ya uhalifu umekua na uwezo mkubwa wa kuathiri simu za kisasa maarufu kama smart phones haza zile zinazotumia program za Androids. Ikumbukwe situ simu kubadilishwa kuwa kipaza sauti bali hata kuweza kufanya mambo mengi na mtu aliye mbali na simu yako.

Inashauriwa kuhakiki unakua na simu yako mara zote na kutowapa usio wafahamu kwani program iayoweza kusababisha aina hii ya uhalifu inaweza tu kuanza kufanya uharibifu maara baada ya mhalifu kuweza kuiweka mikononi simu yako.

Manythings: Hii ni program ambayo ni mpya kwa sasa inayotoa fursa kuzifanya simu za kisasa maarufu kama smart phones kutumika kama kamera za kiusalama “Security camera” Hii inaweza ikapelekea simu hizo kuwa na matumizi salama au mabaya inategemewa na mtumiaji.

Matumizi sahihi, Imekua inatoa fursa kwa simu za kisasa zilizo pitwa matoleo yake kuendelea kuwa na matumizi kwani program hii inayotolewa  bure inatumiwa pale mtumiaji anapokua na simu mbili ya zamani asiyo itumia  na ya sasa anayo itumia.
Simu hizo mbili zinawekwa program ambayo itamuwezesha mtumiaji kuweza kurekodi na kufatilia kwa karibu matukio yote anayo taka kuyafatilia kama ilivyo CCTV hivi sasa.

Matumizi mabaya, Imesadikiwa kuwa wahalifu wanaweza kuingia na simu katika maeneo ambayo wanayafanyia uchunguzi na kuziacha simu hizo kwa kigezo cha kuzisahau huku wakirejea kwenye simu zao kuhakiki wanafatilia matukio yote yanayoendelea katika eneo husika bila ya kugundulika kirahisi – Hili tayari limeweza kujiri mara tu baada ya simu hizi za kisasa kuwezeshwa kurekodi matukio na mhusika kutumia simu yake mpya kufatilia akiwa mbali kabisa na eneo.

Sasa Niangazie njia salama za matumizi ya simu za mikononi maarufu kama “best practice”

Namba za siri: Simu za mikononi zimetoa fursa ya kuweka maneno ya siri wakati wa kufungua simu hizo na kwa watumiaji huduma mbali mbali mfano za utumaji wa pesa kupitia simu zao. Namba hizo za siri ili kubaki salama nimuhimu ukawa muangalifu kwa kutoweka mwaka wa kuzaliwa, namba zinazo fatana au namba yako ya simu.

Kwakufanya hivyo utatoa ruhusa kwa mtumiaji asiye husika kuwa na uwezo mkubwa wa kubashiri kirahisi na kuweza kusababisha ma dhara kwa simu yako ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya na hata kufanya vitendo vya wizi wa pesa kupitia simu yako.

Ujumbe mfupi wa maandishi: Kumekua na wimbi la wahalifu mtandao kupitia jumbe fupi za maandishi wanaomba taarifa binafsi za watu wakijitabulisha kama watu kutoka mabenki au sehemu nyingine. Unashauriwa kuwa makini sana na usitoe kabisa taarifa zako binafsi kwa Yule usie mjua kupitia ujumbe mfupi wa maandishi.

Pia ina shauriwa kuto sambaza ujumbe wa maandishi usio kua na uhakika nao na unaoweza kusababisha taharuki kwa wasomaji wa ujumbe huo. Kwenye hili pia inashauriwa upatapo ujumbe mfupi wa maandishi kwa mtu asiye jitambulisha na wewe kumfaham kutompatia majibu.

Weka simu yako karibu nawe muda wote: Ifahamike aina nyingi za uhalifu mtandao unaofanywa kupitia simu za mikononi unasababishwa na mtumiaji simu kuweka simu yake mbali na yeye au kuwaazima simu kwa asiye wafahamu.

Kwenye hili nitoe kisa kifupi sana, Kuna Mhalifu mtando alienda kwenye kibanda cha kutolea pesa na wakati yuko katika jitihada za kutoa pesa alijifanya anampigia anayehitaji kumtumia pesa na mawasiliano kutokua mazuri.

Baadae alimuomba mhudumu wa kibanda cha miamala ya kifedha kumpatia simu yake ya mkononi ili aweze kutumia huduma ya ujumbe mfupi wa maandishi. Baada ya kupatiwa simu alicho kifanya ni ku rekebisha orodha za namba ya simu na baadae mtumiaji mwingine aliyekua amewekewa namba zake pale kuanza kutuma jumbe akimtaka mwenye kibanda kuanza kuhamisha pesa akionekana kama bosi wake tukio ambalo lilipelekea kiasi kikubwa cha pesa kupotea na uhalifu huu kuripotiwa katika vyombo vya dola.

Funzo hapo, Umakini wa kuwa karibu na simu yako muda wote na kuto waazima usie wajua simu yako unaweza kukuepushia matatizo mengi sana ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya simu yako na hata kupoteza pesa ulizo zi hifadhi katika simu yako.

Kuwa makini sana na huduma ya “Bluetooth” pamoja na “Wireless”: Simu nyingi za kisasa zimekua zikitoa huduma hizi ili kurahisisha mawasiliano ya kusafirisha taarifa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa haraka bila gharama yoyote.

Bahati mbaya unapo kua umeweka huduma hizi wazi muda wote zinaweza kupelekea mhalifu mtandao kuweza kudukua simu yako kirahisi na mara nyingine kukuwekea program hatarishi kwenye simu yako ya mkononi bila ya wewe kujua.

Hii ina mabatana na wale wanao penda kutumia huduma za Wi-Fi zinazotolewa katika viwanja vya ndege au mikusanyiko ya watu. Huduma hii inapo chukuliwa kwenye simu ikumbukwe inatoa fursa kwa mhalifu mtandao kupitia “Man in the middle attack” kuweza kupata taarifa zako na kuzitumia atakavyo.

Inashauriwa kuwasha huduma hizi za Bluetooth na Wireless pale tu unapokua na ulazima kuzitumia na kujiepusha kabisa kutumia huduma za Wi-Fi za bure pasi na ulazima hasa usafirishapo taarifa zako binafsi na za siri.

Kua makini na program za simu: Imekua kawaida kwa watumiaji wa simu za kisasa kupakua program mbali mbali za simu katika simu zao na wakati mwingine hata zile wasizo kuwa na matumizi nazo.

Ikumbukwe si program zote ni salama na wakati mwingine program unayo ipakua na kuiweka kwenye simu yako inaweza kua chanzo cha simu yako kudukuliwa na wahalifu mtandao.


Inashauriwa kuwa makini sana na kila programu unayo  ipakua katika simu zako maarufu kama Mobile Apps na uwe natabia ya kuikagua kwa karibu pale unapokua na ulazima wa kuwa na program hiyo kwa kuangalia walio whi kuipakua wameitolea maoni gani. 

7 comments:

  1. Tatizo letu kubwa ni kwamba tumekua tunatumia tu simu bila ya kujua mambo mengi sana
    Hii imetufungua macho sana mkubwa.
    Big up.

    ReplyDelete
  2. Namna ya kujua kuwa simu yako ya smartphone imeingiliwa, mlio kama wa mtetemo (vibration) hutokea mwanzoni kabisa wakati unapiga simu au wakati unapokea.
    unalizungumziaje hili mtaalam? kuna ukweli wowote?
    nimeipenda mada yako ya leo Mtaalam.

    ReplyDelete
  3. kaka na mimi niliwahi kumuazima mtu simu akidai anataka kumtumia mama yake ujumbe amepatwa na matatizo kumbe alikua anakazana kuhamisha pesa.
    Machale yalinicheza kumnyag'anya simu ghafla nikakuta alikua katika menu za tigo pesa nikaanza kumpigia kelele za mwizi ni hatareee.

    ReplyDelete
  4. Asante kwa elimu unayotoa mkuu,naombautupe elimu kuhusu sheria za Tanzania na namna ya kumshtaki mtu ambaye anakutumia msg za matusi na unamjua.
    Pili naomba utueleze kuhusu usiri unaotakiwa katika mtandao.Tunaambiwa kuwa message zetu zinasomwa na wanaomiliki mitandao kama Voda,Tigo,na Airtel.Ni vipi tutakuwa salama na hawa watu wasisome message zetu?

    ReplyDelete
  5. Asante kwa maarifa unayotoa, na kushauri uendelee na tutauunga mkono. Nashauri pia mihutaasari ya masomo kuhusu TEHAMA KATIKA VYUO VIKUU NA TAASISI ZINGINE ITAZAMWE UPYA HAPA NCHINI, ILI ANAYEFUNDISHWA APATE MAARIFA MAKUBWA BADALA YA KUWA NA SIFA YA CHETI KIKUBWA! Kumbuka kwamba cheti cha elimu si elimu bali ni ishara ya elimu iliyojificha kwa kila binadamu! Kwa sababu utaalamu uhalifu wa wizi katika mitandao ya mawasiliano umeanzia Nchi za nje ambazo zinategemea sana viwanda katika uchumi. Inaonyesha wazi kwamba Nchi hizo zimetuzidi katika ujuzi na maarifa makubwa na lazima TUWEKEZE KWA NGUVU KATIKA UTOAJI BORA WA ELIMU KUJARIBU KUWAFIKIA WENZETU.

    ReplyDelete
  6. Nawashukuru wote kwa maoni yenu mazuzuri - nimeyapitia kwa karibu na najitahidi kuyaingiza katika vitendo kufikia malengo.

    Nawatakia Siku njema.

    ReplyDelete