Mataifa
mbalimbali duniani ifikapo tarehe 28 ya kila mwezi wa kwanza wanaadhimisha siku
ya kimataifa ya faragha ya taarifa ambapo kunakua na matukio mbali mbali ya kuhamasisha
njia rafiki za kuweka salama taarifa za watu hasa wawapo mtandaoni. Taarifa
zaidi za siku hii "BONYEZA HAPA"
Siku
hii imekua ikitumika vizuri kwa ushirikiano mkubwa ma mashirika binafsi,
serikali na vyombo vya habari kukumbusha watumiaji mitandao kuzingatia matumizi
salama ya mitandao ili kubakisha taarifa za watumiaji mtandao salama.
Inafahamika,
ukuaji wa wa kasi wa Teknolojia umeambatana matumizi yasiokusudiwa wa
teknolojia ambapo umekua ukihatarisha sana ufaragha wa watumiaji wa teknolojia
hizo. Kwa kuzingatia hili siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa imekua
ikihimizwa kutumika vizuri kukumbusha watumiaji mtandao yale yanayoweza
kuhakikisha taarifa zao zinabaki salama watumiapo mitandao.
Kwa
uchache mambo kadhaa ya kuzingatia ili kuweza kulinda faragha yako ya taarifa ikiwa
ni ukumbusho ni kama yafuatayo:-
Kupitia mahojiano maalumu katika kuadhimisha
siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa yaliyofanyika kati yangu na kituo cha
radio cha East Africa pamepata kuanishwa kwa uchache mambo muhimu ya kuzingatia
ili kuweza kujiweka salama utumiapo mtandao na kuhakiki taarifa zako zinabaki
salama ambapo ni umakini wa kuperuzi tovuti pamoja na utumiaji wa Hotspots (Wifi au Wireless) zinazotolewa bure katika maeneo ya mkusanyiko.
Ufafanuzi
wa kujua jinsi gani utajua kama tovuti unayoitembelea ni salama au la – Kuna tool
maarufu ijulikanayo kama “WOT – Web Of Trust” ambayo inatoa msaada wa kutoa
tathmini ya tovuti. Inapo ona tovuti haiku salama inakutahadharisha unapojaribu
kuitembelea, ni vizuri ikatumiwa ili iweze kukupa msaada wa kujua kama
unachotembelea ni salama au la.
Aidha,
Ufafanuzi juu ya Man in the middle attack – Unapotumia Wifi za bure si zote
zinakua ziko salama na ndio maana mara nyingi wana tahadharisha “Use it at your
own risk” ikimaanisha ukiitumia basi ujue lolote linaweza kukutokea. Ili kujua
kama Wireless unayoitumia iko salama hakikisha ina alama ya kikufuli au maelezo
kua ni salama kinyume na hapo mtu yoyote anaweza kuona kila unacho safirisha.kujifunza
zaidi juu ya Man in the middle attack "BONYEZA HAPA"
Ikumbukwe
kilichozungumzwa hapo juu ni kwa uchache tu katika mengi na pia ni vigumu kuwa
salama kwa asilimia miamoja ingawa kilicho jadiliwa ni njia mbali mbali
zinazoweza kuweka ugumu wa taarifa zako kufikiwa kirahisi na wahalifu mtandao.
Msisisito
ni kua kila mmoja anajukumu kubwa la kuhakiki anajiweka salama binafsi na
kumueka salama mwenzake. Hii ni pamoja na kuhakiki usambazi viambatanishi
mtandaoni vinavyoweza kuwa hatarishi kwa wengine. Mfano: Kumekua na uhalifu
mtandao unaojulikana kama “Fishing” ambapo kwa bahati mbaya baadhi ya watu kwa
kutokujua wamekua wakiwasambazia wengine na hatimae kuongeza wigo la usambaaji
wa uhalifu uo na hatimae wengi taarifa zao kuwa mashakani.
Aidha,
bado kumekua na muamko unaokua kwa kasi ndogo wa watu binafsi kujenga tabia ya
kufatilia taarifa zinazoweza kutoa msaada wa kila mmoja kuweza kubakisha salama
taarifa zake atumiapo mtandao.
Nitoe
wito kwa kila mmoja kuwa na tabia ya kujifunza na kutaka kujua zaidi juu ya
matumizi salama ya mitandao yatakayo wezesha taarifa za kila mmoja kubaki
salama.
No comments:
Post a Comment