WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Sunday 6 April 2014

KUNAHITAJIKA UWEPO WA UMAKINI KATIKA KUTOA TAARIFA BINAFSI MITANDAONI

Katika Muendelezo wa Kuelimisha Jamii jinsi ya kubaki salama mitandaoni leo najikita katika maswala ya USIRI “PRIVACY” ambapo taarifa nyingi za mtu binafsi si vyema kuwekwa mitandaoni napia maelezo mafupi ya namna wahalifu mtandao wanatumia taarifa hizo za siri mitandaoni kuleta madhara.


Njia za awali ambazo wahalifu mtandao wanatumia kabla ya kusababisha madhara ni kukusanya taarifa za mhusika ambaye wanategemea kumdhuru kwa njia inayojulikana kitaalam kama “RECONNAISSANCE” ambapo mara nyingi taarifa za awali zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii kwani inaaminika wengi hawana umakini katika kutoa taarifa zao kupitia mitandao ya kijamii.


Jamii inashauriwa kujenga umakini wa taarifa binafsi wanazo ziweka mitandaoni ili kuweza kubaki salama. “Takwimu inaonyesha asilimia kubwa ya watumiaji wamekuwa wakiweka taarifa ambazo zinaweza kutoa urahisi wakugundua mambo mengi kutoka kwa muhusika” – Yusuph Kileo.

Mfano, Kuna wale ambao hadi leo wanatumia maneno ya siri “PASSWORDS” kwa kutumia mwaka wao wa kuzaliwwa wakati kuo huo mwaka huo wa kuzaliwa umewekwa kwenye mitandao ya kijamii hapo inaonyesha ni jinsi gani muhusika huyu anatengeneza urahisi kwa mhalifu kuweza kumuingilia kumdhuru.


Aidha, Umuhimu mkubwa unahitajika katika utoaji wa siri za mtu binafsi kwani panapokua na ugumu katika kukusanya taarifa za awali za mtu binafsi kunajengeka ugumu wa ukusanyaji wa taarifa za muhusika ambapo kunapelekea ugumu kwa mhalifu kuleta madhara kirahisi kwa mhusika.

Pia Kumekua na wimbi la wahalifu wanao omba moja kwa moja kupitia baruapepe au mitandao ya kijamii taarifa za watu na takwimu zinaonyesha kuna wale ambao bado wanatoa taarifa hizo bila kujua athari zake.
“Nashauri Unapo pokea jumbe inayo kuhitaji utoe taarifa zako binafsi aidha kwa maelezo kuwa kuna matengenezo katika akaunti yako au kukuwezesha kifedha na kuanzisha uhusiano kuwa makini kwani ni moja ya hatua za ukusanyaji wa taarifa za mtu ili kujenga njia ya kuanzisha madhara” – Yusuph Kileo.

Picha: inaonyesha mambo ya msingi kuzingatia utumiapo mitandao ya kijamii ili kuweza kujenga ugumu kwa wahalifu mtandao kuleta madhara.


No comments:

Post a Comment