Wizara ya Mawasilano, Sayansi na Teknolojia ipo katika mkakati wa kuandaa muswada wa sheria za matumizi salama ya mtandao ili kukabiliana na changamoto za uhalifu kupitia mtandao.
Kupitishwa kwa miswada hiyo kuwa sheria kutapunguza hali ya kukithiri kwa matukio ya uhalifu wa kutumia mtandao, uvujaji wa taarifa za siri pamoja na upotevu wa haki miliki kutokana na kukosekana kwa sheria ya kudhibiti vitendo hivyo.
Miongoni mwa Miswada ya sheria itakayoandaliwa na Wizara hiyo ni pamoja na muswada wa sheria ya kulinda taarifa binafsi, Muswada wa sheria ya Biashara ya Miamala ya kielectronic na Muswada wa sheria ya kuzuia uhalifu kwa njia ya komputa.
Sheria hizo zimelenga kudhibiti uhalifu kwa kutumi mtandao, udukuzi, utunzaji wa taarifa za siri na kuwalinda watoto dhidi ya matumizi yasiyofaa ya kwenye mitandao.
Kwasasa sheria zinazotumika kudhibiti masuala ya uhalifu katika mitandao ni sheria ya Ki electronic na Posta, Sheria ya makosa ya jinai na sheria za ushahidi Tanzania - STAR TV HABARI
"Uhalifu Mtandao Umeonekana Kushika Kasi Nchini Kwa Sasa" - Yusuph Kileo.
/
Aidha Mataifa Mbali mbali tayari yameweza kuongeza kasi katika vita dhidi ya uhalifu mtandao huku sheri zikiendelea kuboreshwa ili kukabiliana na mabadiliko katika teknologia ya mtandao hivi sasa. Tanzania Nayo Imeweza kupiga hatua kiasi katika kukuza mapambano dhidi ya uhali mtandao ingawa jitihada za ziada na za dhati bado zinahitajika.
Video Hapo chini Imetoa mafunzo kwa jamii dhidi ya uhalifu unao shika kasi Nchini wa kutumia Mtandao kuiba fedha katika mabenki.
good thing!!
ReplyDelete