Kwanza kabisa, Faili
lolote ambalo linasomeka na kiambatanishi .exe mfano: umoja.exe nifaili ambalo
limedhamiriwa kuingizwa kuwa ni moja ya program za komputa hivyo kabla ya
kubonyeza aina hii ya mafaili lazima uwe na ujuzi wa unacho kibonyeza ndicho
mahitaji yako au la.
Aidha, kwa upande wa
aina hii ya uhalifu umekua ukitumia vifaa kama USB, au CD na DVD ambazo
muhusika anayetakiwa kudhuriwa anaweza kuvikuta aina hizi za vifaa kwenye ofisi
yake na maranyingi vinakua vimekaa katika sura ya kushawishi muhusika
avichukue.
Maara baada ya kufanya
hivyo kinachofata ni muhusika kuwa na kutaka kujua nini kiko ndani, na ndipo
muhusika atataka kufungua na hapo kunakua na faili/mafaili yenye majina mfano,
Mishahara.exe (ambapo muhusika atajua ni faili litakalo onyesha mishahara ya
wafanya kazi) na huwenda pia ika wa majina mengine mbali mbali.
Muhusika anapo bonyeza
ili kutaka kuona hiyo mishahara, mhalifu anakua tayari kashaingia katika
komputa yake na kuweza kuanza kuleta madhara punde tu anapo anaza kutumia
mtandao. “mara unapo kua mtandaoni tayari unaongeza wigo la mhalifu kuweza
kukudhuru na unapotoka mtandaoni mhalifu anakua hana tena nafasi ya kukudhuru.”
– Yusuph Kileo.
Hili ni jambo muhimu
sana kulifahamu yakua unapokua mtandaoni tayari unakua si salama sana na
utokapo mtandaoni unakua salama kimtamtandao kutokana na madhara ya usalama
mtandao yanaweza kuonekana na kujitokeza pale tu unapo kua umejiingiza
mtandaoni.
Hivyo, unapo kuta kitu
chochote kama CD, USB, DVD na vingine vyenye mfano wa hivyo ambavyo hujui
vimefikaje au hukuwa umeagiza viletwe kwako eidha mlangoni mwa ofisi kwenye
lift ya ofisi au hata mezani ofisini kwako yako unachopaswa kufanya ni
kuviwasilisha maramoja kwa kitengo cha usalama mtandao “Computer security
department” kwa hatua zao.
No comments:
Post a Comment