Wana mitandao kote duniani hivi sasa bado wako katika hali ya taharuki
kufuatia wataalam wa ulinzi mtandao kuweka hadharani tishio jipya la mapungufu
yaliyo bainika yanayo ruhusu wahalifu mtandao kuweza kuiba maneno ya siri
“passwords” na hata taarifa za kadi za ma benki.
“SSL” ambayo nimeifafanua zaidi kwenye chapisho langu linalosomeka WEB SECURITY ni moja ya program/ kiunganishi cha programu inayo aminika kuweza kuficha taarifa mitandaoni ili kutoonekana
kirahisi, ila baada ya kugundulika hivi karibuni ya kuwa aina hiyo ya
program iliyo aminika kuwa salama imeingiwa na mapungufu lukuki na hadi sasa
imeweza kutoa athari kubwa kwa watumiaji wengi wa mitandao ya intanet.
Aidha, tayari makampuni mengi
yamesha anza kutoa tahaddhari dhidi ya hali hii ya kutisha kiusalama mtandao na
kusisitiza watumiaji kuweza kubadilisha maneno yao ya siri “Password” ili
kuweza kujiweka katika hali ya amani kwani huwenda wanayo tumia sasa tayari
yalisha chukuliwa na wahalifu mtandao.
Hadi
sasa makampuni kama “Google”, “yahoo” na “amazon” kumepatikana namna ya
kurekebisha hali hiyo na kumekua na makala yanaendelea kuandikwa kuweza
kusambaza elimu kwa uma jinsi ya kuji linda na hali hiyo. Zaidi unaweza pitia
taarifa hii ya Heartbleed bug kwa lugha ya kingereza inayo fafanua na nini chakufanya.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete