WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Tuesday, 3 June 2014

RASIMU YA USALAMA WA MTANDAO YAKAMILIKA NCHINI TANZANIA

Uhalifu mtandao umeendelea kukua kwa kasi katika maeneo mbali mbali duniani. Hii imepelekea Microfoft kuanzisha kitengo maalumu kitakacho ongeza uwezo wa kukabiliana na usalama mtandao kama inavyosomeka kwenye taarifa ya kingereza inayosomeka "HAPA".

Wakati huo huo takwimu zilizo tolewa na Idara ya upelelezi kupitia kitengo cha kukabiliana na uhalifu mtandao ya nchini Sirilanka zimeonyesha ukuaji wa makosa hayo katika nchi hiyo yameendelea kukukua kwa kasi. Takwimu hizo zinapatikana katika tovuti yao inayosomeka "HAPA".

Pamoja na nguvu kubwa ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao bado changamoto kubwa hasa katika nchi za afrika imekua ni upungufu wa sharia zinazoweza kuwafanya wahalifu kuchukuliwa hatua stahiki pale inapothibitika uhalifu mtandao kufanyika.

Nchi mbali mbali zimeendelea kuboresha sharia zao na kuzifanya kua kali zaidi ili kuweza kuhimili vishindo vya wahalifu mtandao ambapo wanaonekana kushika kasi ya kipekee. Moja ya nchi hizo ni hapa kwetu TANZANIA.

Prof. Makame Mbarawa
Wizara ya mawasiliano, sayansi na teknolojia imekamilisha rasimu ya miswadada mitatu ya sharia za usalama wa mtandao ili kudhibiti uhalifu katika mitandao nchini Tanzania.

Akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo, Waziri profesa makame Mbarawa alitaja miswada hiyo kuwa ni sharia ya usalama wa mtandao, sharia ya kulinda taarifa binafsi, sharia miamala ya kielektoniki na sharia ya kudhibiti uhalifu mtandao na komputa.
Alisema rasimu hizo zimewasilishwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili ziweze kuandaliwa kwa mujibu wa taratibu za uandishi wa sharia.

Pia alisemawizara hiyo imetengeneza kanuni mpya zinazosimamia mawasiliano kupitia mitandao ya simu ambayo ilianza kazi mwezi oktoba mwaka mwaka jana kwa makampuni ya nje kutakiwa kulipa senti 25 za marekani kwa kila dakika moja ya mazungumzo ya simu zinazongia nchini kutoka nje.

Profesa Makame ali ongeza na kusema katika kanuni hiyo mpya imeweka mgawanyo wa mapato hayo ya senti 25 ambapo serikali kupitia hazina inapata senti saba, watoa huduma wanapata senti kumi na tatu na senti tano ni kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ikiwa ni pamoja na kumlipa mwekezaji wa mtambo huo.


Aidha, kwa upande wa sharia mtandao, zinatofautiana sana na sharia nyingine kwani mapitio yake yanapaswa kufanyika mara kwa mara kutokana na sababu za msingi za makosa mtandao kubadilika badilika kutokana na ukuaji wa haraka wa teknoljia hivi sasa.

4 comments:

 1. Ni hatua nzuri kwa serikali yetu kulipa umuhimu suala la udhibiti wa uhalifu mtandao unaozidi kukua siku hadi siku.

  ReplyDelete
 2. Tanzania imekua inajitahidisana kwendana na wakati , tatizo ni mara chache sana kuzipata taarifa kama hizi. Mara nyingu tunazosikia zaidi ni za udaku tu
  Mungu ibariki Tanzania

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nashkuru kwa maoni yako - Jitihada za taarifa za maswala ya Usalama Mtandao na tehama kwa ujumla kwa sasa Tanzania kupitia Vyombo vya habari naamini vimekua na jitihada za kina kuweza kukuza uelewa.
   Sasa pia ni jukumu lako na langu na la mwingine kufatilia ili kuweza kuwa salama kimtandao.

   Delete