WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday, 20 June 2014

TCRA YATOA ONYO KWA WANAOTUMIA MITANDAO KUCHAFUA WENGINE

Dr. Raynold Mtungahema
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA, imewaonya wale wote wanaotumia mitando kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo watakabiliwa na mkono wa sheria.

Onyo hilo limetolewa jana mjini Arusha na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, Dkt, Raynold Mtungahema, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maswali ya wanahabari kuhusu kuenea kwa picha chafu zinazowadharirisha watu mbalimbali kwenye mitandao.

Nilipata kufafanua yakua mtandao au kifaa chochote cha digitali kinapotumiwa visivyo kinaweza kupelekea mtumiaji kujikuta akifanya uhalifu mtandao. Mifano katika hili nilipata kueleza, pale mtumiaji anapotumia mtandao kutukana, kutishia na kudhalilisha wengine mitandaoni anakua amefanya kinachoitwa "Cyberbullying" ambacho ufafanuzi wa hili unaweza kusomeka "HAPA"

Kwa nchi za magharibi wamekuwa na kampeni mbali mbali zinazo hamasisha kutokomeza aina hii ya uhalifu mtandao ambapo takwimu za ITU za mwaka 2013 zilionyesha takriban nusu ya wenye umri kati ya miaka 13 - 17 wamekua wana athirikazaidi na "Cyberbullying".

Kwa Tanzania hapakua na tofauti, Mitandao imekua ikitumika kusambaza taarifa za uongo, chuki na kudhalilisha wengine na hata baadhi kutishia wengine kupitia mitandao (Simu pamoja na Komputa) kitu ambacho ni hatari sana kwa usalama wa taifa lolote. Hili lilipelekea TCRA kuja na kampeni ya "Futa delete kabisa" inayo hamasisha kutosambaza jumbe za chuki, matusi au uongo ili kulinda amani ya Tanzania.


Aidha, hapo jana Katika muendelezo kuhakiki yakua kunakua na matumizi salama ya mitandao Dr. Mtungahema amesema, matumizi ya mitandao ambayo sio sahihi ni kosa la jinai na hivyo wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja na akawataka  wanaochafuliwa kupitia mitandao wafungue majalada polisi na mamlaka hiyo itasaidia kuwafuatilia wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria .

Alisema mitandao yote imesajiliwa hata kama aliyehusika kuchafua anaishi uvunguni atakamatwa kwa kuwa mitandao haipo kwa ajili ya matumizi yasiyo sahihi  ambayo hayaruhusiwi.

Mtungahema,  amesema  atakaebainika anatumia mtandao kumchafua mtu mwingine huyo amefanya kosa la jinai hivyo afikishwe mbele ya vyombo vya sheria kwa kuwa tayari zipo sheria zinazotoa adhabu kwa mtuhumiwa atakaepatikana na hatia.

Aliongeza kuwa TCRA, imeshapokea malalamiko mengi na tayari wahusika wameshatiwa mbaroni  na ufuatiliaji utaendelea ili mradi tu mamlaka hiyo itaarifiwe.

Nchi wanachama wa jumuia  afrika mashariki zimeaanza kikao cha siku nne  mjini Arusaha kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa chang moto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mawasiliano.

Mwenyekiti wa jumuia hiyo ya sekta za mawasiliano, EACO, Dakta   Fracis Wangusi, amesema sekta ya mawasiliano inakabilwa na changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa haraka.

Wangusi ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya,amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na kuhama kutoka mtandao wa analojia kwenda digital na  matumizi ya visumbusi kwa ajili ya luninga.

Aliongeza kuwa , sekta ya simu inakabiliwa na changamoto ya kuwepo gharama kubwa za matumizi ya simu, usambazaji barua na vifurushi kunakofanywa namashirika ya posta unaotokana na ukuaji wa mji ambao haujapangiliwa ,matumizi ya  vikwazo vya kuchelewesha huduma ya haraka ya internet .


Alisisitiza kuwa ili kupatikana kwa mafanikio hayo ni kuondoa vikwazo na kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano ICT.

No comments:

Post a Comment