WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Tuesday, 8 July 2014

TANZANIA NA UHALIFU MTANDAO - MJADALA

Mijadala ihusuyo maswala ya usalama mtandao imeendelea katka ngazi mbali mbali. July 6 ya Mwaka huu wa 2014 Yusuph Kileo alipata kushiriki na wataalam wengine wa ndani kujadili maswala mbali mbali yahusuyo usalama mtandao nchini. Mjadala ulihusisha mkusanyiko wa taarifa mbali mbali za kiusalama mitandao kutoka katika mataifa mengine pamoja na mwelekeo wa kukabiliana na uhalifu mtandao katika mataifa mbali mbali Duniani.

Kipindi kilihusisha wageni walio alikwa Katika studio pamoja na mjumuisho wa simu kutoka kwa wasikilizaji ili kupata mawazo mchanganyiko yahusuyo maswala ya usalama mtandao. Kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio kilikua na lengo la kutoa elimu kwa umma, hali halisi ya uhalifu wa kimtandao duniani ilivyo na hapa nchini Tanzania. (Sikiliza kipindi kizima kwenye link hapo chini)
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na hali halisi ya uhalifu mtandao ambapo takwimu na baadhi ya makosa mapya ya kimtandao yalipata kujadiliwa.  Mifano, uhalifu mtandao unaoweza kutoa fursa ya kuua mtu kwa msaada wa mtandao bila ya kuwa karibu na mlengwa pamoja na makosa mengine yalipata kuangaliwa kwa karibu.
Aidha, paligusiwa namna ambavyo sheria za mtandao na uhalifu wa kimtandao zilivyo hivi sasa nchini Tanzania na faida zake endapo zitaanza kutumika rasmi. Maswala makubwa matano ambayo yanategemewa kupewa nguvu katika mataifa mbali mbali ili kupunguza uhalifu mtandao pia yalijadiliwa.

Maswala hayo ni pamoja na elimu ya ulewa kwa wananchi ( awareness), Kupatikana kwa sharia madhubuti zitakazoweza kuto uwezo wa kuwadhibiti wahalifu katika mataifa mbali mbali, Kujengea uwezo wa wataalam wa ndani katika maswala ya usalama mitandao, Kuwa na framework ya pamoja kama bara ( Bara Ulaya tayari limesha fanyia kazi hili) pamoja na uwazi wa takwimu za uhalifu mtandao katika ngazi za kitaifa ili kuwezesha wataalam kugundua maeneo hatarishi zaidi na hatimae kuunganisha nguvu kudhibiti maeneo hayo hatarishi.

Pakizingatiwa, kundi kubwa la watu ni la vijana kati ya Umri wa miaka 15 hadi 30 na vijana hao ndio wanao onekana kuathiri zaidi mitandao (Uhalifu matandao) pamoja na aina nyingine za uhalifu. pameendelea kuwa na mbinu mbali mbali zenye malengo ya kuwawajibisha vijana ili kupunguza uhalifu ikiwa ni pamoja na uhalifu mtandao.
Jitihada hizo ni pamoja na za wakala wa umoja wa mataifa inayojihusisha na maswala ya teknohama (ITU) kupitia Young innovators ambapo Yusuph kileo aliteuliwa kuwa miongoni mwa mabalozi wapya anaetegemewa kuungana na wengine wote wakiwa na malengo ya kuwashughulisha vijana kifikra kutoka maeneo yote duniani.
Vijana wanashirikishwa katika kubuni maswala mbali mbali yahusuyo Teknohama ambapo zawadi za fedha taslim pamoja na kuwezeshwa kufanikisha kilicho buniwa kuingia katika uhalisia ni miongoni mwa faida zinazo patikana.

Wito umetolewa kwa vijana wa kitanzania kuchangamkia fursa hii hasa ukizingatia Mtanzania (Yusuph kileo) ni miongoni mwa mabalozi katika hili. Kwakushiriki kwenye hili patawezesha vijana wa kitanzania kuweza kutambulika zaidi uwezo wao na kupeperusha bendera yataifa kimataifa pamoja na kujumuika na vijana wengine kutoka maeneoo mbali mbali (Network building).
Ilikupata Kuona na kujua zaidi juu ya shindano linaloendelea chini ya mpango huu wa Young innovators iliyo chini ya wakala wa umoja wa mataifa inayo jihusisha na maswala ya teknohama (ITU) tembelea "HAPA"
Walio shiriki katika mjadala uliohusisha maswala ya usalama mitandao ni pamoja na Yusuph Kileo,Josephine Safiel,Kevin Chungu,Mahadhi Juma na Mtangazaji Maduhu wa Morning Star Radio.

No comments:

Post a Comment