Swala
la kukuza uelewa wa matumizi mtandao salama maarufu kama “Cybersecurity Awareness programs” imekua iki
himizwa sana kwani uhalifu mtandao unaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa sana
pale watumiaji watakapo pata ufahamu wa kina wa matumizi salama wa mitandao.
Swala
hili limekua liki imizwa sana na mataifa mbali mbali ili kuhakiki matumizi salama
ya mitandao yanakuwepo na hatimae kupunguza wimbi kubwa la uhalifu mtandao unao
endelea kukua hivi sasa. Katika kuonyesha umuhimu wa swala hili Mwezi Wa Kumi
umekua ukitumika kama mwezi maalum wa kukuza uelewa wa matumizi salama katika
mataifa mengi. Kujua zaidi katika Hili Fatilia Taarifa inayoweza kusomeka "HAPA"
Kwa
kutambua umuhimu Huo Chuo cha Teknolojia cha Dar-es-salaam (DIT) kiliandaa
semina maalum ambapo wanafunzi wa vyuo mbali mbali waliweza kualikwa kuhudhuria
semina hiyo ambayo ilikua na lengo la kukuza uelewa wa matumizi salama ya
mitandao.
Washiriki
ambao walikua ni kundi kubwa la vijana, ambao pia wanachukua idadi kubwa ya
watumiaji mitandao nchini waliweza kupata elimu hiyo ambapo nili iwasilisha kwa
kufafanua mambo mbali mbali kuanzia uelewa wa nini hasa maana ya usalama
mitandao, uhusiano wa matawi mbali mbali yahusuyo usalama mitandao na athari za
uhalifu mtandao hadi sasa katika ngazi ya Dunia.
Aidha,
niliangazia Hali ilivyo katika bara La Afrika na Juhudi mbali mbali
zinazoendelea ili kuweka Bara salama. Huku niki eleza namna mbali mbali
wanavyoweza kujilinda na kuwalinda wengine na uhalifu mtandao.
Maangalizo
mbali mbali ambayo yanaweza kupelekea kuweza kuwatenganisha watu wema wanaofanya uhalifu
mtandao bila kukusudia na wahalifu halisi wa mitandao niliweza kufafanua.
Katika
Semina Hiyo Palipatikana maswali kadhaa kutoka kwa washiriki hao. Pia
Niliendelea kutoa wito wa wataalam wengi kujisukuma katika fani hii ambayo kwa
sasa mbado ina wataalam wa chache sana na mahitaji ni makubwa kutokana na
ukuwaji wa teknolojia unao ambatana kabisa na matumizi makubwa ya TEHAMA katika
maisha yetu ya kila siku.
Kwa
Picha Na taarifa iliyo andikwa na mwandishi aliye hudhuria smina hiyo unaweza
kusoma kwa "KUBONYEZA HAPA"“
No comments:
Post a Comment