WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday, 31 October 2014

MWEZI WA USALAMA MITANDAO UMEFIKIA TAMATI - YALIYOJIRI NA MAZINGATIO YAKE.

Mwezi huu wa Oktoba mataifa mbali mbali yamekua yakiadhimisha kwa kukuza ufuhahamu kwa watu wake juu yamatumizi salama ya mitandao. Ni wazi ya kuwa mitandao inapotumika vibaya inaweza kuleta athari kubwa sana kwa jamii, na tayari matukio mengi kutoka maeneo mbali mbali tayari tumeendelea kuya shududia.

KATIKA MWEZI HUU: kwa uchache kabisa nitaangazia matukio baadhi nikianzia na kutokea nchini "MAREKANI" Raisi wa Marekani Alipitisha agizo muhimu kwa taifa hilo kuhusiana na matumizi ya kadi ili kufanyia miamala ya kibiashara ikiwa ni katika kukabiliana na matukio ya hivi karibuni nchini mwake.tukio ambalo limeibua mijadala mbali mbali huku mataifa mengine yakiaswa kulifanyia kazi na kuboresha baada ya uchambuzi wa tukio hilo kufanywa na wataalam mbali mbali wa maswala ya usalama mitandao.

"KENYA" kupitia mkutano wake mkuu wa mwaka unao wakutanisha wataalam na wafanya maamuzi katika maswala ya TEHAMA walipata kuangalia kwa karibu maswala mbali mbali ya kiusalama mitandao kwa kina na kuyatafutia ufumbuzi.

"TANZANIA" pia kupitia Warsha iliyofanyika na kushirikisha mataifa mbali mbali iliyofanyikia Tume ya Taifa Sayansi COSTECH mjadala wa kina ulio jikita kwenye maswala ya usalama mitandao ulioibua mazuri mengi ikiwa ni pamoja na kuendeleza ushirikiano baina ya washiriki pamoja na kubadilishana ujuzi na taarifa za msingi katika maswala ya usalama mitandao.

"CERT - EU" inayosimamia mwaswala ya usalama mitandao katika nchi wanachama za bara ulaya  walianza rasmi kujumuisha taarifa zinazopatikana hapa kwenye tovuti yao huku mijadala mbali mbali ya kiusalama mitandao kupitia foramu mbali mbali yakijadili taarifa zinazopatikana hapa.

"BBC - SWAHILI" na Vyombo vingine vya Habari Nchini vilionekana kuhamasisha matumizi salama ya mitandao, hatua ambayo naipongeza sana – Hii ni kwa sababu , vyombo vya habari vimekua na nafasi kubwa sana katika kuhakikisha wananchi wanapata ufahamu mzuri wa matumizi salama ya mitandao ili kuweza kujiweka salama wao na taifa lao kwa ujumla.

Kwa wale ambao kwa namna moja au nyingine hawakubahatika kufatilia kampeni hii ya mwaka huu ya mwezi wa kukuza ufahamu juu ya matumizi salama ya mitandao wanaweza kupitia taarifa nilizo ziandika nikiambatanisha na viambatanishi muhim kufafanua umuhimu wa kuadhimisha mwezi huu kama inavyoweza kusomeka katika link zifuatazo.

OKTOBA NI MWEZI WA KUKUZA UELEWA WA MATUMIZI SALAMA YA MITANDAO

WITO: Kusha kwa mwezi huu maalum wa kukuza uelewa wa matumizi salama mitandao haumaanishi juhudi za kukuza uelewa kwa taifa juu ya matumizi salama mitandao ziishie hapa bali iwe ni fursa tosha kabisa kwa kila mmoja wetu kuchukua yale yaliyopatikana kwenye kampeni za mwezi huu kuyafanyia kazi.

Tujenge tabia ya kujifunza zaidi na kuhakiki tunautambuzi yakinifu yakua kila mmoja anajukum la dhati la kuhakikisha anajiweka salama awapo mtandaoni na anakua na matumizi salama ya mtandao ili kuwa na mafanikio chanya yatokanayo na ukuwaji wa matumizi ya teknolojia nchini.


2 comments:

 1. Kaka Kwa Tanzania Mwezi huu huwa unaadhimishwa au Kutambulika? Au Tatizo bado si kubwa hapa kwetu?
  Nimeipenda sana hii kaka.
  Kazi njema.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kwanza nashkuru sana Kwa Maoni - Aidha, Kwa Tanznaia Bado Hatuja anza kuadhimisha Rasmi Huu mwezi ingawa Naimani Mwakani huwenda Pakawa na Utofauti.
   Nimelihimiza hili kwa mara ya Kwanza nchini kutokana na Kuwepo kwangu Nchini kwa mara ya Kwanza Ndani ya Mwezi wa Kumi Toka Nifahamu vizuri Maazimisho haya ya Kukuza ufahamu wa matumizi salama ya Mitandao.
   Na Tayari nilijaribu kulizungumzia na kuomba wadau wakubwa kulifanyia kazi na nimategemeo yangu mwakani patakua na madiliko kwenye hili.

   Ahsante.

   Delete