Miaka 11 iliyopita Marekani ikitambua ukuaji wa matumizi mabaya ya
mitandao walianzisha kampeni maalum iliyoamuliwa kufanyika kila mwezi oktoba.
Kampeni hiyo maalum ilihamasisha mashule , kampuni binafsi na serikali kutumia mwezi oktoba kuhamashisha uelewa wa matumizi salama ya
mitandao.
Kadri
muda ulivyojongea Mataifa mengine yaliamua kutumia mwezi huo kuwa mwezi wa
kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao ambapo sasa mataifa mengi tayari
yamesha kua yakiazimisha kampeni hizi. Mwaka huu wa 2014 Kama Inavyo ainishwa "HAPA" imeweza kuchanganua kwa ufupi maudhui na kauli mbiu ya mwaka huu, ratiba,
namna ya kushiriki na mambo mengine muhimu.
Ifahamike vizuri jitihada za kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao duniani kote ni endelevu na mwezi oktoba umechukuliwa kuwa maalum ili kuonyesha umuhimu wa kampeni hizi kwa kuzingatia ukuaji wa matumizi ya mitandao unaoambatana kabisa na matumizi mapaya kwa baadhi ya watu.
"JUMBE" teule kwa upande wangu ni kuongeza matumizi mazuri na sahihi ya maneno ya siri
ili kujiweka salama utumiapo mitandao.
Kwa
Upande mwingine Tanzania imeendelea kuwa mwenyeji wa midahalo na warsha mbali mbali zihusianazo na maswala ya
usalama mitandao ambapo ni fursa nzuri kwa watanzania kuweza kushiriki ili
kukuza uelewa wa maswala haya ya ulinzi mitandao ambapo dunia ya leo
yemeonekana kua na sura ya pekee.
Mwanzoni
mwa mwaka huu Nikiwa Ughaibuni, Kwenye "MKUTANO"mkuu wa mwaka katika maswala
usalama mitandao na teknolojia ya habari kwa ujumla miongoni mwa mazungumzo
mengi nje ya vikao yalionyesha mataifa mbali mbali kua na jitihada binafsi za
kuhakiki mikutano na warsha mbali mabli zinachukua nafasi ya pekee ili kuhamasisha
matumizi salama ya teknolojia habari na
mawasiliano.
Kwa
Tanzania, "MKUTANO" Unaotegemea kukamilika Hapo Kesho wa Maswala Ya Usalama
Mitandao Jijini Arusha umekua ni moja ya fursa nzuri kwa watanzania kuhakiki
wanatambua hali halisi kuhusiana na uhalifu mtandao na jitihada endelevu
zinazoendelea kwenye taifa kwenye mapambano dhidi ya uhalifu mtandao.
Aidha,
mwezi wa Oktoba mwaka huu Tanzania
Inategemewa kuwa mwenyeji wa mkutano/ Warsha ya kimataifa ya maswala ya usalama
katika mitandao ambapo wataalam kutoka mataifa mbali mbali watategemewa
kujadili maswala mbali mbali. Kushiriki warsha hii muhimu,Mtanzania anapaswa
kusoma na kujaza Fomu maalumu iliyo ambatanishwa hapo chini na kuirudisha
COSTECH Tanzania.
Mwezi
Novemba mkutano Mwingine mkubwa wa kufunga mwaka unaotegemewa kuhusisha
wataalam mbali mbali wa maswala ya uslama mitandao watakutana kuongezeana uwezo
na kujadili maswala makuu manne ya jinsi ya kutambua uhalifu mtandao, Kuuzuia,
Kuchukulia hatua unapotokea na jinsi ya kurudisha uslama mitandao katika hali
yake ya awali baada ya kutokea.
"MKUTANO" huu ambapo Mwenyeji wake ni Nchi ya Afrika Kusini ni fursa nyingine kwa
watanzania kuhuduria ili kujua mengi katika maswala haya ya uhalifu mitandao
ikizingatiwa mimi nikiwa kama Mtanzania kuteuliwa kuwa katika Paneli ya
Washauri katika Mkutano huo.
N.B: The article is in SWAHILI But, The attached Links are In ENGLISH.
ReplyDelete