Maswala
ya udukuzi yameendelea kushika kasi katika maeneo mbali mbali ulimwenguni
ambapo mataifa mbali mbali yameamua kuunganisha nguvu ya pamoja kupambana na
uhalifu mtandao. Katika "UCHAMBUZI" nilio uandikia nilibainisha umuhimu wa
kupata chombo kimoja chenye jukumu la kupambana na uhalifu mtandao ambacho
kitatoa nguvu kubwa ili kuweza kukabiliana na hali mbaya ya uhalifu mtandao
hivi sasa.
Kundi
jipya lenye makao yake barani ulaya linalounganisha pamoja nchi wanachama wa
bara ulaya pamoja na Canada, Colombia, Australia na marekani limedhamiria
kuunganisha mataifa mengine na kuhakiki maswala mbali mbali yahusuyo usalama
mtandao yanafanyiwa kazi ipasavyo.
Kwa
wafatiliaji wa habari za maswala ya usalama mitandao watakua wamepata kuona taarifa mbali mbali za hivi karibuni
zenye kuonyesha ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao ambapo umetabiriwa kushika
kasi zaidi kadri muda unavyo zidi kwenda ambapo uhalifu mwingi wa sasa
unategemewa kuhamia katika mitandao.
Katika
andiko la naibu mkurugenzi wa chombo cha uingereza kinacho shughulikia maswala
ya uhalifu mtandao pamoja na kiongozi wa
kundi jipya la muunganiko wa nchi la kukabiliana na uhalifu mtandao kama inavyo
someka "HAPA" wame elezea ukuaji wa changamoto mbali mbali kwa vyombo vya
usalama katika mataifa mengi na kusisitiza kuna umuhimu mkubwa wa kuunganisha
nguvu za pamoja ili kuweza kufanikiwa katika vita dhidi ya uhalifu mtandao.
J-CAT
imedhamiria kuzileta pamoja nchi wanachama pamoja na mataifa mengine yatakayo
onyesha utayari ili kuweza kukabiliana kwa pamoja dhidi ya uhalifu mtandao
ambapo matumaini makubwa yatakua ni kukusanya taarifa za kiuhalifu kutoka
katika makampuni ya serikali na binafsi ili kubaini aina za uhalifu na kujua
maeneo athirika zaidi ili kuweza kuunganisha nguvu. Nchi zaidi zitaenelea
kushirikishwa baada ya majaribio ya mpango huu wa kuunganisha nguvu kuweza
kufikia pazuri.
Aidha,
Chombo cha upelelezi cha Marekani (FBI) kupitia taarifa inayosomeka "HAPA" imebainisha kulipa kipaumbele cha juu swala la mapambano dhidi ya uhalifu
mtandao kutokana na kilicho zungumzwa na mkurugenzi wake ya kuwa nchi hiyo
tayari imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na wahalifu wanao onekana na kwa
sasa wahalifu mtandao kua ndio changamoto yake kubwa na hivyo wameazimia kuanza
mapambano na uhalifu huo.
Kwa
upande mwingine katika mkutano mkuu wa maswala ya usalama mtandao wa mwisho wa
mwaka ambapo nimeteuliwa kuwa katika panel ya washauri mada zinazotegemewa
kujadiliwa na wataalam kutoka maeneo yote duniani ni pamoja na kutafuta njia
rafiki ya kufikiwa kwa malengo ya kuunganisha hasa bara la afrika kuweza kuwa
na njia ya pamoja ya kupambana na uhalifu mtandao huku maswala ya kisheria za kimtandao yanavyo sumbua mataifa mbali
mbali nini utatuzi wake.
Panategemewa kupatikana taarifa kamili ya mkutano huo
mapema ili watanzania ( wenye ufahamu wa maswala ya usalama mtandao) nao waweze
kushiriki.
No comments:
Post a Comment