Ukipitia
takwimu za mwaka huu na mwaka jana inaonyesha Nchi za Ulaya na Marekani
zimeendelea kuathirika zaidi na uhalifu mtandao, Huku Nchi za mashariki ya kati
kuonekana kunyemelewa na wahalifu mtandao. Wakati huo huo takwimu zilitabiria
Nchi za Afrika kuwa katika hali mbaya
baadae kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya mitandao ambao hauendani
sanjari na maandalizi madhubuti ya usalama wa mitandao.
Mengi
yalizungumzwa kuhusiana na tishio jipya katika nchi za kiarabu huku kampuni
inayojihusisha na ulinzi mtandao ya Kaspersky wakiandika "NCHI YA SAUDI ARABIA" imedhamiriwa zaidi na wahalifu mtandao kauli ambayo iliambatana na "UTAFITI" ukibainisha kampuni za mashariki ya kati zimeendelea kulengwa na wahalifu
mtandao.
Hatua
hiyo ilisababisha nchi hizo za mashariki ya kati kuwekeza zaidi na kuimarisha
jitihada zake za mapambano dhidi ya uhalifu mtandao. "JEDDAH" iliyoko Saudi
Arabia ilianzisha kituo kipya kilicho imarishwa maalum kwa ajili ya mapambano
dhidi ya uhalifu mtandao na Hivi karibuni "JORDAN" nao wakazindua kituo chao
maalum kwa ajili ya kupambana na uhalifu mtandao.
Vile
vile nchi nyingine za Mashariki ya kati (ME) zimeendelea kuwekeza na kufungua
vituo maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao katika ukanda huo ambapo
imeenda sambamba na uboeshwaji wa sharia mitandao.
NINI
TUNAJIFUNZA KAMA TAIFA?
Tayari
imezoeleka nchi za ulaya na Marekani zimekua vinara kwenye kuwekeza katika
mapambano dhidi ya uhalifu mtandao kutokana na athari kubwa ambayo tayari
imesha ziona.Na hivi sasa inaonekana Nchi za Mashariki ya kati nazo zikiwekeza
katika upande huo.
Nchi
za Afrika pia zimeendelea kujipanga na kkuwekeza kwenye sekta hii ambayo
inaonekana kuwa tishiokubwa mapema baadae. Jitihada zilizopo zinapaswa kuendana
sambamba na kuweka vizuri sharia mtandao huku itafutwa njia rafiki
itakayofungua mipaka kwenye mapambano dhidi ya uhalifu huu mtandao ambao hauna
Mipaka.
Maboresho
ya mara kwa mara yanahitajika kwenye vituo maalum vya mapambano dhidi ya
uhalifu mtandao pamoja na kuwa na mapitio ya sheria mtandao mara kwa mara
kutokana na mabadiliko na ukuaji wa teknolojia inayochangia kasi ya uhalifu
mtandao kuongezeka. Haya na mengine nimepata kuya ainisha kwa kina kwenye andiko linaloweza kusomeka
"HAPA"
No comments:
Post a Comment