Suala
la hivi karibuni la nchini Israel la kiusalama mitandao linaloweza kusomeka "HAPA",
Polisi wanchi ya Botswana kuonyesha wasi wasi wao juu ya maswala ya usalama
mtandao kama inavyoweza kusomeka "HAPA" pamoja na matukio mengine kadhaa ya
uhalifu mitandao ambayo yamekua yakigonga vichwa vya habari hivi sasa yameibua
swali, je kuna uwezekano mapambano dhidi ya uhalifu kufikiwa malengo kwa
kupunguzwa walau kwa kiasi Fulani?
Jibu
ni kwamba hivi sasa uhalifu mtandao umeendelea kukua huku pakitumika njia za
kisasa na hatarishi zinazo onekana kua tishio katika mifumo ya mitaandao katika
nchi nyingi duniani. Ingawa pia wataalam
wa maswala ya usalama mitandao wameendelea kujipanga na kuangalia kila namna ya
kuweza kukabiliana na uhalifu mtandao katika ngazi ya kidunia.
Kubwa
lililo jiri hivi karibuni kumeendelea kutafutwa mbinu za kuhakiki uhalifu
mitandao unapata kudhibitiwa huku baadhi ya makampuni nanchi mbali mbali
kuchukua hatua stahiki nikitolea mfano "FACEBOOK" na tukio la "UJERUMANI" ikiwa
ni mifano miwili kwa uchache.
Lakini
pia azimio la hivi karibuni lililokua limebeba mambo ma tano (5) limeendelea kufanyiwa kazi katika mataifa mbali
mbali ambapo yatatoa fursa ya kuweza kupunguza na kuzuia uhalifu mtandao katika
maeneo husika. Mambo hayo ni pamoja na kukuza uelewa wa maswala ya usalama
mitandao kwa wananchi ( Cyber security awareness programs), Kuwa na Sheria za
usalama mitandao ( Cyber laws) , Kuweza kukuza uwezo wa wataalam wa ndani
katika mataifa mabali mbali ( Capacity building).
Mengine ni pamoja na Kuwa na uwazi wa takwimu
za kiuhalifu mtandao ( Cybercrime statistics) pamoja na kupatikana kwa
makubaliano ya pamoja ya nchi katika mabara ili kuweza kuunganisha nguvu ya
pamoja kwenye mapambano dhidi ya uhalifu mtandao ( Cybersecurity framework).
Kwenye
andiko hili nitatolea ufafanuzi juu ya mambo hayo matano na jinsi gani yanavyoweza
kusaidia mapambano dhidi ya uhalifu mtandao huku nikitolea mifano kadhaa.
CYBERSECURITY AWARENESS PROGRAMS:
Inaaminika ni vizuri kujikinga na tatizo kuliko kungoja litokee kisha litaftiwe
tiba. Na pia inaaminika tatizo linaweza kuzuiwa kuanzia katika ngazi ya mtu
moja mmoja. Kila Mmoja anapoweza kujiweka salama mtandaoni atasababisha uhalifu
kupungua na kutoa urahisi kwa wana usalama mitandao kuweza kupambana na uhalifu
huo.
Hivyo
jukumu la kila mtu kujijengea muda wa kutaka kujua namna za kuweza kukaa salama
kimtandao ni muhimu sana. Tasnia ya habari michezo na maigizo kupitia
vipeperushi, Sinema , maandiko mengine yanaweza kutumika kuweza kukuza uelewa
kwa wananchi kujua namna ya kua salama na hatimae kujenga uelewa wa kujikinga
na uhalifu mtandao kuanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja.
CYBER LAWS:
Hizi ni sharia mitandao. Ni vigumu sana kwa mahakama kuweza kutoa hukumu
stahiki kwa wale wote wanaoweza kukamatwa kwa maswala ya uhalifu mitandao ikiwa
hapata kuwa na sheriashariai inayo kidhi mahitaji ya maswala ya ulinzi
mitandao.
Hili
limekua likionekana kua kikwazo kikubwa nanchi nyingi zimeendelea kuchukua
hatua za kuboreshwa sharia mtandao zilizo kuwepo ili kwenda na wakati (Mfano: "UINGEREZA")
pamoja nanchi nyingine kuazisha sharia hizo ili kuweza kusaidia kutoa hukumu
kwa wahalifu mtandao (Mfano: "TANZANIA")
CAPACITY BUILDING:
Hili la kukuza uwezo wa ndani kwa wataalam wa maswala ya usalama mitandao ili
kuweza kupata watakao kua na ujuzi sahihi wa uhalifu mtandao na namna ya
kuppambana nao pia imeendelea kua muhimu sana. Nilipata kuhojiwa na chombo
kimoja cha ughaibuni na baadae kuwekwa hili vizuri kama linavyo someka "HAPA"ambapo
msisitizo juu ya kila nchi kuweza kujenga miundo mbinu ya kuweza kukuza vipaji
vya wataalam wake wa ndani wa maswala ya usalama mitandao ni muhimu sana
ukizingatia uhaba mkubwa ulioko wa wataalam wa maswala ya usalama mitandao kote
duniani.
Nchi
nyingi kwa sasa zimeendelea kulichukulia hili uzito na tayari limeendelea
kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na Marekani, Visiwa Vya Solomoni, Uingereza na
Afrika Kusini kutaja nchi kwa uchache. Uzuri kwa Tanzania Pia Hili huwenda
likawa na sura nzuri hivi karibuni ambapo itakua ni fursa kwa watanzania
kulichangamkia ili kuweza kuendana na hali
ya ukuwaji wa teknolojia hivi sasa.
CYBERCRIMES STATISTICS:
Hili lakuwa na takwimu za uhalifu mitandao zinazowekwa wazi limekua
likisisitizwa liweze kufanyiwa kazi na kubainishwa kupitia ripoti za mwaka za
nchi moja moja ambazo baadae zinaweza kujumuishwa kwenye ripoti za mwaka za
kimataifa ambazo zitatoa fursa ya kutambua maeneo hatarishi ili kuweza
kukabiliwa kwa haraka na kupatiwa nguvu ya muunganiko.
Aidha,
Kupitia Tovuti maalum zinazojihusisha na mapambano dhidi ya uhalifu mtandao au
za serikali za nchi moja moja pia zimeonekana kuwa na nafasi katika hili huku
nchi ya "SIRILANKA" kuonyesha mfano kwenye hili pamoja na Nchi nyingine kadhaa.
CYBERSECURITY FRAMEWORK:
Hili limekua ni la muhim sana chini ya mwamvuli wa umoja ni nguvu na utengano
ni udahifu. Mapambano ya uhalifu mtandao ni magumu sana endapo nchi moja moja
itachukua dhamana binafsi bila kushirikiana na nyingine kwa ukaribu kwa
kuunganisha nguvu.
Hili
linatokana na uhalisia wa uhalifu mtandao mbali na kua na uharibifu mkubwa sana
katika mataifa mbali mbali bali pia hauna mipaka. Hapa naamanisha mhalifu
mtandao hana ulazima wakua katika eneo la tukio au kua katika nchi anayo
tegemea kuifanyia uhalifu, Maana yake Mhalifu aliye nchi moja anaweza kuleta
madhara makubwa sana katika nchi nyingi pasi nayeye kuwai kufika katika nchi
hiyo.
Kwa
kuliona hili Nchi za Umoja Wa Ulaya (EU) Walifanikiwwa kuja na makubaliano yao
yapamoja yaliyo unganisha nguvu nchi zote wanachama pamoja na kuwa na kituo
mama kinachoshughulikia maswala yao ya usalama mtandao na takwimu zinaonyesha
wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika mapambano baada ya kuanzishwa kwa umoja
huo wa kushughulikia maswala ya usalama mitandao ambapo walipata kusifiwa
kufuatia hatua yao hiyo kupitia taarifa inayosomeka "HAPA"
No comments:
Post a Comment