Kumekua
na wimbi la ukuaji wa teknolojia kila kukicha, Ukuaji huu wa teknolojia umepelekea
matumizi makubwa ya mitandao maeneo mengi na hili linaenda sambamba na ukuaji
wa kasi wa uhalifu mtandao hivi sasa. Mbali na "MIWANI" pamoja na "MAGARI YASIYO NA DEREVA" kutoka
Google, pia kumekua na aina nyingine ya miwani maarufu kama “Spy glasses” ambayo awali iliaminika inatumiwa zaidi na
wahalifu ( wadukuzi) wa taarifa za watu.
Miongoni
mwa maswala yaliyo umiza vichwa wataalam wa maswala ya usalama mitandao katika
mijadala ni pamoja na kupima athari za miwani hii ya kisasa ambayo inakua
imeambatanishwa na kifaa chenye uwezo wa kuona, na kusafirisha taarifa upande
wa pili huku pande zote mbili kuweza kusafirisha sauti kupitia mawani hiyo.
Aina
tatu za mawani hizi za kisasa ziliweza kuangaziwa macho na wataalam wa maswala
ya usalama mitandao ili kujua ni athari kiasi gani zinaweza kuleta kwa jamii na
badae katika kampeni ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao kwa msaada wa tasnia ya uigizaji, Hollywood kupitia Tamthilia ya "NIKITA" kwenye kipengele chake cha mwisho sehemu ya kwanza naya tatu
walitolea ufafanuzi aina mbili za miwani na uwezo wake.
Aina
hiyo ya mawani sasa imeonekana kuchukua sura mpya pale Polisi nchini uchina
kukamata wanafunzi waliyokuwa wakitumia miwani hiyo wakati wakifanya mitihani ilikuwasiliana na walio nje kupatiwa majibu ya mtihani. Uchunguzi huo uliambatana na tahadhari kuwa
miwani hiyo iko kawaida sana na kwa haraka haraka si rahisi kuitambua hivyo
wasimamizi mitihani kutakiwa kuwa makini sana kwa wavaaji miwani.
Aidha,
aina hii ya miwani pia imehofiwa kuenea zaidi ambapo inaaminiwa kwa kushirikiana
na teknolojia ya simu zinazo tumiwa na wahalifu kufatilia watu kwa pamoja
zinategemewa kutumiwa vibaya na hatimae kusababisha wimbi la uhalifu mtandao
lililoboreshwa zaidi kuleta madhara makubwa kwa mataifa mbali mbali.
No comments:
Post a Comment