Tukiwa
tupo ndani ya Mwezi wa kuhamasisha uelewa wa matumizi salama ya mitandao,
Marufu kama “NATIONAL CYBERSECURITY AWARENESS MONTH” nimeona si vibaya
tukajikumbusha matukio muhimu matano ya kiuhalifu mtandao yaliyojiri mwaka huu.
Huku
mataifa mbali mbali yakiendelea kujipanga katika mapambano dhidi ya uhalifu
mtandao, bado matukio ya kiuhalifu mtandao yameendelea kuitikisa dunia. Yafuatayo
ni matukio matano niliyo chagua kuyajadili siku ya leo.
NEIMAN MARCUS
Mwezi
wa pili mwaka huu wa 2014, Kampuni ya Neiman Markus ilitengeneza vichwa vya
habari baada ya kuingiliwa na wadukuzi wa mitandao waliofanikiwa kuchukua
taarifa za wateja wake na kufanikiwa kuzima kila kiashiria ambacho kingeonyesha
hali isiyo ya kawaida katika kampuni hiyo.
Awali
taarifa zilionyesha ni wateja milioni moja na nukta moja ndio walio athirika taarifa za kiuchunguzi ambazo zimeandikwa na “BUSSINESSWEEK” zimefafanua tukio hili.
APPLE
Kampuni
ya Apple nayo haikubakishwa salama. Moja ya matukio makubwa yaliyojadiliwa na wana
usalama mitandao ni pamoja na tukio la wadukuzi mitandao kuingilia, kuchukua na
kuzisambaza picha mbaya za watu maarufu kutoka Hollywood ambao walikua
wamezihifadhi katika moja ya huduma za Apple maarufu kama iCloud.
Hili
halikua tukio zuri kwa Apple pakizingatiwa liliambatana na uzinduzi wa simu
zake za iphone 6. Apple walipolizungumzia hili walisema udukuzi ulilengwa moja
kwa moja kwa baadhi ya watu maarufu wa Hollywood na si udukuzi wa jumla ambao
ungeathiri watumiaji wengi. Kiundani taarifa ya tukio la Apple inapatikana "HAPA"
TARGET
Wadukuzi
mitandao waliingilia kampuni ya taget pia ambapo kwa mijibu wa taarifa
inayosomeka "HAPA" imeonyesha athari kubwa iliyoikumba kampuni hiyo ambapo
udukuzi huo umeigharimu kiasi cha Dola milioni Miamoja na Arobaini na nane.
WAL-MART
Wal-Mart
ni moja ya kampuni yenye kuaminika na bahati mbaya wadukuzi walifanikiwa
kuingilia na kuiba taarifa ambazo baadae zilipatikana zikisafirishwa kwenda
ulaya ya mashariki. Uhalifu huu Wal-Mart walisisitiza kutouzungumzia na mkuu
wake wa kitengo cha usalama mitandao kuanisha katika maelezo yake kuwa
wanafanya jitihada za dhati kuongeza usalama wa taarifa zake ili kuzuia
chochote kinachoweza kuathiri mitandao yake.
HOME DEPOT
Utakumbuka
kupitia taarifa inayosomeka "HAPA" nilizungumzia kwa kina tukio la kuingiliwa
kwa moja ya kampuni ya kimarekani ambapo ilitengeneza vichwa vya habari baada
ya kungundulika wadukuzi mtandao walifanikiwa kuendeleza uhalifu huo kwa miezi
mitano hadi walipoweza kugundulika.
Kwa kumalizia, Si
vibaya tukaliangalia hili lililozungumziwa Al-hamisi ya tarehe mbili ya mwezi
huu wa kumi kama inavyosomeka "HAPA" yakuwa taarifa za majina, namba za simu na
mengineyo ya watu zaidi ya Milioni 76 yameweza kuibiwa na wadukuzi kutoka
katika kampuni ya J.P Morgan Chase. Tukio hili limeelezewa kuwa nitukio kubwa
la aina yake
No comments:
Post a Comment